HADITHI YA 40

الحديث الأربعون
"كن في الدنيا كأنك غريب أو عابر سبيل"
عن ابنِ عُمَرَ رضي اللهُ عنهما قال: أَخَذَ رسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم بِمَنْكِبيَّ فقال : ((كُنْ في الدُّنْيا كأنَّكَ غَرِيبٌ، أو عابرُ سبِيلٍ)).
        وكانَ ابنُ عُمَرَ رَضي اللهُ عنهما يقولُ: إذا أمْسَيْتَ فلا تَنْتظِرِ الصبَّاحَ، وإذا أصْبَحْتَ فلا تَنْتَظِرِ الَمسَاءَ، وخُذْ مِنْ صِحَّتِكَ لِمَرضِكَ، ومِنْ حَياتِكَ لِمَوْتِكَ.

رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ  
HADITHI YA  40
KUWA DUNIANI KAMA VILE MGENI AU MPITA NJIA

Kutoka kwa Ibn 'Umar  رضي الله عنهما  ambaye alisema:
Mtume صلى الله عليه وسلم  alinishika bega na akasema:  Kuwa (ishi) duniani kama vile mgeni au mpita njia.
Naye Ibn 'Umar  رضي الله عنه  alikuwa akisema : Ukishinda hadi jioni usitaraji kuishi mpaka asubuhi, na ukiamka asubuhi usitaraji  kuishi mpaka jioni, chukua uzima wako kwa ugonjwa wako (yaani fanya yale yote mema uwezayo wakati bado una afya nzuri kwani siku ukiumwa hutoweza kuyafanya), na uhai wako kwa kifo chako (tumia maisha yako vizuri kwa kufanya amali njema maana ukishafariki hakuna tena uwezalo kulifanya).

Imesimuliwa na Al-Bukhari