At-Twaariq (86)


سُورَةُ  الطَّارَق
At-Twaariq (86) 

(Imeteremka Makka)

Sura hii imeanzia kwa kiapo cha kuashiria dalili za kudra ya Mwenyezi Mungu, na inatilia mkazo kuwa kila nafsi ina mlinzi wake na muangalizi, na inamtaka mtu ajifikirie kuumbwa kwake, na ya kwamba yeye kaumbwa na maji yenye kutoka kwa kasi, ili ipatikane hoja kwamba Mwenye kuumba hivi ni Mweza wa kumrejeza tena baada ya kufa kwake.Tena ikaapa mara ya pili kwamba Qur'ani ni kauli ya kufafanua wala si maneno ya maskhara. Na juu ya kuwa hivyo makafiri bila ya shaka wameshughulika kuikanya na kuipangia njama. Na Mwenyezi Mungu amezirudi njama zao kwa njama kali kuliko zao. Kisha Sura imekhitimisha kwa kutaka wapewe muhula makafiri.


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

وَالسَّمَاءِ وَالطَّارِقِ ﴿١﴾

1. Naapa kwa mbingu na kinachokuja usiku.

وَمَا أَدْرَاكَ مَا الطَّارِقُ ﴿٢﴾

2. Na nini kitakachokujulisha nini kinachokuja usiku?

النَّجْمُ الثَّاقِبُ ﴿٣﴾

3.  Ni nyota in’gaayo sana.

إِن كُلُّ نَفْسٍ لَّمَّا عَلَيْهَا حَافِظٌ ﴿٤﴾

4. Hakuna nafsi yeyote isipokuwa inayo mlinzi juu yake (Malaika aandikaye ‘amali).

فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ مِمَّ خُلِقَ ﴿٥﴾

5. Basi na ajitazame insani ameumbwa kutoka na kitu gani?

خُلِقَ مِن مَّاءٍ دَافِقٍ ﴿٦﴾

6. Ameumbwa kutokana na maji yatokayo kwa kuchupa.

يَخْرُجُ مِن بَيْنِ الصُّلْبِ وَالتَّرَائِبِ ﴿٧﴾

7. Yanatoka baina ya uti wa mgongo na mbavu.

إِنَّهُ عَلَىٰ رَجْعِهِ لَقَادِرٌ ﴿٨﴾

8. Hakika Yeye (Allaah) juu ya kumrudisha kwake (katika uhai) bila shaka ni Qaadir (Muweza).

يَوْمَ تُبْلَى السَّرَائِرُ ﴿٩﴾

9. Siku siri zitakapodhihirishwa.

فَمَا لَهُ مِن قُوَّةٍ وَلَا نَاصِرٍ ﴿١٠﴾

10. Basi (insani) hatakuwa na nguvu yoyote (ile) na wala mwenye kunusuru (msaidizi) yeyote.

وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الرَّجْعِ ﴿١١﴾

11. Naapa kwa mbingu inayorejesha (mvua).

وَالْأَرْضِ ذَاتِ الصَّدْعِ ﴿١٢﴾

12. Na (kwa) ardhi inayopasuka (kutoa mimea).

إِنَّهُ لَقَوْلٌ فَصْلٌ ﴿١٣﴾

13. Hakika hii (Qur-aan) ni kauli ya kupambanua (haki na batili).

وَمَا هُوَ بِالْهَزْلِ ﴿١٤﴾

14. Na wala hiyo si mzaha.

إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًا ﴿١٥﴾
15. Hakika wao wanapanga njama.


وَأَكِيدُ كَيْدًا ﴿١٦﴾

16. Nami napanga mipango (ya kuvunja na kupindua njama zao).

فَمَهِّلِ الْكَافِرِينَ أَمْهِلْهُمْ رُوَيْدًا ﴿١٧﴾

17. Basi wape makafiri muhula, waache wangojee kidogo.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com