Ad-Dukhaan: 44

  الدُّخان
Ad-Dukhaan: 44

(Imeteremka Makka)


Sura hii imeanza kwa kusimulia khabari za Qur'ani, ya kwamba imeteremka kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika usiku wa Lailatul Qadri ulio barikiwa, kwa ajili ya kuonya na Tawhid, Imani ya Mwenyezi Mungu Mmoja. Na kwamba hii Qur'ani ni Haki, Kweli tupu. Hali kadhaalika Sura imesimulia khabari za kufufuliwa, na kwamba hayo hayana shaka ndani yake, na imezibisha hoja za wanao yakanya hayo, na ikawarudi washirikina. Ikalinganisha baina ya washirikina wa Makka na wenzao walio watangulia, nao ni kaumu ya Firauni. Ikaeleza mapatilizo ya Mwenyezi Mungu yaliyo washukia hao. Tena ikatilia mkazo kwamba Siku ya Kiyama ndiyo siku iliyo pangwa ya kuutenga ukafiri na upotovu wote. Na ikasimulia malipo ya wakosefu kwa siku hiyo na malipo ya walio ongoka. Na ikamalizika kama ilivyo anzia kwa mazungumzo juu ya Qur'ani, na kwa kuwaonya wanao kadhibisha Ujumbe wa Mtume s.a.w. kuwa nao wangojee balaa na masaibu yatakayo washukia.



بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

حم﴿١﴾
1. Haa Miym.


وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ﴿٢﴾
2. Na Kitabu kinachobainisha.


إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ ۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ﴿٣﴾
3. Hakika Sisi Tumeiteremsha (Qur-aan) katika usiku uliobarikiwa,   hakika Sisi Tumekuwa Wenye kuonya.


فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ﴿٤﴾
4.  Humo (Laylatul-Qadr) hupambanuliwa kila jambo la hikmah.


أَمْرًا مِّنْ عِندِنَا ۚ إِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ﴿٥﴾
5. (Kila) Jambo (Tulokadiria) kutoka Kwetu, hakika Sisi ndio Wenye kutuma (Wajumbe).


رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿٦﴾
6. Ni Rahmah kutoka kwa Rabb (Mola) wako, hakika Yeye Ndiye As-Samiy’ul-‘Aliym (Mwenye kusikia yote - Mjuzi wa yote).


رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ﴿٧﴾
7. Rabb (Mola) wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, mkiwa ni wenye yakini.



لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ﴿٨﴾
8. Hakuna ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye, Anahuisha na Anafisha; Rabb (Mola) wenu na Rabb wa baba zenu wa awali.


بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ يَلْعَبُونَ﴿٩﴾
9. Bali wao wamo katika shaka wanacheza.


فَارْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُّبِينٍ﴿١٠﴾
10. Basi ngojea uangaze siku mbingu zitakapoleta moshi bayana.



يَغْشَى النَّاسَ ۖ هَـٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١١﴾
11. Utawafunika watu. Hii ni adhabu iumizayo.



رَّبَّنَا اكْشِفْ عَنَّا الْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ﴿١٢﴾
12. (Watasema): “Rabb (Mola) wetu! Tuondoshee adhabu, hakika sisi wenye kuamini”.


أَنَّىٰ لَهُمُ الذِّكْرَىٰ وَقَدْ جَاءَهُمْ رَسُولٌ مُّبِينٌ﴿١٣﴾
13. Kutoka wapi watapata ukumbusho (mawaidha), na hali amekwishawajia Rasuli bayana.


ثُمَّ تَوَلَّوْا عَنْهُ وَقَالُوا مُعَلَّمٌ مَّجْنُونٌ﴿١٤﴾
14. Kisha wakamkengeuka na wakasema: “Amefunzwa (hii Qur-aan, na pia ni) majnuni.”


إِنَّا كَاشِفُو الْعَذَابِ قَلِيلًا ۚ إِنَّكُمْ عَائِدُونَ﴿١٥﴾
15. Hakika Sisi Tutaiondosha adhabu kidogo, lakini nyinyi hakika mtarudia (ukafirini).


يَوْمَ نَبْطِشُ الْبَطْشَةَ الْكُبْرَىٰ إِنَّا مُنتَقِمُونَ﴿١٦﴾
16. Siku Tutayoteka kwa nguvu mnyakuo mkubwa (wa adhabu) hakika Sisi ni Wenye kulipiza


وَلَقَدْ فَتَنَّا قَبْلَهُمْ قَوْمَ فِرْعَوْنَ وَجَاءَهُمْ رَسُولٌ كَرِيمٌ﴿١٧﴾
17. Na kwa yakini Tuliwatia mtihanini kabla yao watu wa Fir’awn, na aliwajia Rasuli mtukufu.


أَنْ أَدُّوا إِلَيَّ عِبَادَ اللَّـهِ ۖ إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ﴿١٨﴾
18. (Akiwaambia): “Nikabidhini waja wa Allaah, hakika mimi kwenu ni Rasuli mwaminifu.


وَأَن لَّا تَعْلُوا عَلَى اللَّـهِ ۖ إِنِّي آتِيكُم بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ﴿١٩﴾
19. “Na kwamba msitakabari mbele ya Allaah; hakika mimi nakuleteeni dalili bayana.


وَإِنِّي عُذْتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُمْ أَن تَرْجُمُونِ﴿٢٠﴾
20. “Na hakika mimi nimejikinga kwa Rabb (Mola) wangu na Rabb wenu msije kunirajimu.


وَإِن لَّمْ تُؤْمِنُوا لِي فَاعْتَزِلُونِ﴿٢١﴾
21. “Na ikiwa hamtoniamini basi nitengeni mbali”


فَدَعَا رَبَّهُ أَنَّ هَـٰؤُلَاءِ قَوْمٌ مُّجْرِمُونَ﴿٢٢﴾
22. Akamuomba Rabb (Mola) wake kwamba: “Hawa watu ni wahalifu.”


فَأَسْرِ بِعِبَادِي لَيْلًا إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ﴿٢٣﴾
23. (Allaah Akasema): “Basi ondoka kisiri na waja Wangu usiku, hakika nyinyi ni wenye kufuatwa.”


وَاتْرُكِ الْبَحْرَ رَهْوًا ۖ إِنَّهُمْ جُندٌ مُّغْرَقُونَ﴿٢٤﴾
24. “Na acha bahari ikiwa imetulia, hakika wao ni jeshi lenye kugharikishwa.”


كَمْ تَرَكُوا مِن جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ﴿٢٥﴾
25. Ngapi wameacha katika mabustani na chemchemu.


وَزُرُوعٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ﴿٢٦﴾
26. Na mimea na makazi mazuri mno.


وَنَعْمَةٍ كَانُوا فِيهَا فَاكِهِينَ﴿٢٧﴾
27. Na neema walikuwa humo wenye kuzifurahia.


كَذَٰلِكَ ۖ وَأَوْرَثْنَاهَا قَوْمًا آخَرِينَ﴿٢٨﴾
28. Hivyo ndivyo (ilivyo). Na Tukawarithisha watu wengineo.


فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ وَمَا كَانُوا مُنظَرِينَ﴿٢٩﴾
29. Na hazikuwalilia mbingu na ardhi, na wala hawakua wa kupewa muhula.


وَلَقَدْ نَجَّيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنَ الْعَذَابِ الْمُهِينِ﴿٣٠﴾
30. Na kwa yakini Tuliwaokoa wana wa Israaiyl kutokana na adhabu ya kudhalilisha.


مِن فِرْعَوْنَ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَالِيًا مِّنَ الْمُسْرِفِينَ﴿٣١﴾
31. Kutoka kwa Fir’awn, hakika yeye alikuwa mwenye kibri miongoni wenye kupindukia mipaka.


وَلَقَدِ اخْتَرْنَاهُمْ عَلَىٰ عِلْمٍ عَلَى الْعَالَمِينَ﴿٣٢﴾
32. Na kwa yakini Tuliwakhitari (wana wa Israaiyl) kwa elimu kuliko walimwengu (wowote).


وَآتَيْنَاهُم مِّنَ الْآيَاتِ مَا فِيهِ بَلَاءٌ مُّبِينٌ﴿٣٣﴾
33. Na Tukawapa miongoni mwa Aayaat (miujiza, ishara) zilizokuwemo mitihani bayana.


إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ لَيَقُولُونَ﴿٣٤﴾
34. Hakika hawa (Maquraysh) bila shaka wanasema.


إِنْ هِيَ إِلَّا مَوْتَتُنَا الْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُنشَرِينَ﴿٣٥﴾
35. “Haya si chochote isipokuwa ni mauti yetu ya awali, nasi hatutofufuliwa.


فَأْتُوا بِآبَائِنَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٣٦﴾
36. “Basi tuleteeni mababu zetu mkiwa ni wakweli.”


أَهُمْ خَيْرٌ أَمْ قَوْمُ تُبَّعٍ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ أَهْلَكْنَاهُمْ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا مُجْرِمِينَ﴿٣٧﴾
37. “Je, kwani wao ni bora zaidi au kaumu ya Tubba’ (mtawala wa kale Yemen), na wale waliokuwa kabla yao. Tuliwaangamiza. Hakika wao walikuwa wahalifu.


وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَاعِبِينَ﴿٣٨﴾
38. Na Hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake kama wenye kucheza.


مَا خَلَقْنَاهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٣٩﴾
39. Hatukuumba viwili hivyo isipokuwa kwa haki, lakini wengi wao hawajui.


إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ مِيقَاتُهُمْ أَجْمَعِينَ﴿٤٠﴾
40. Hakika Siku ya hukumu ni wakati wao maalumu uliopangwa kwa wote.


يَوْمَ لَا يُغْنِي مَوْلًى عَن مَّوْلًى شَيْئًا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ﴿٤١﴾
41. Siku ambayo jamaa msaidizi hatomfaa jamaa (yake) chochote, na wala wao hawatonusuriwa.


إِلَّا مَن رَّحِمَ اللَّـهُ ۚ إِنَّهُ هُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ﴿٤٢﴾
42. Isipokuwa yule Atakayerehemewa na Allaah.  Hakika Yeye Ndiye Al-’Aziyzur-Rahiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika - Mwenye kurehemu).


إِنَّ شَجَرَتَ الزَّقُّومِ﴿٤٣﴾
43. Hakika mti wa az-zaqquwm.


طَعَامُ الْأَثِيمِ﴿٤٤﴾
44. Ni chakula cha mtendaji mno dhambi.


كَالْمُهْلِ يَغْلِي فِي الْبُطُونِ﴿٤٥﴾
45. Kama masazo ya zebaki nyeusi ziliyoyeyushwa inatokota matumboni.


كَغَلْيِ الْحَمِيمِ﴿٤٦﴾
46. Kama kutokota kwa maji yachemkayo.



خُذُوهُ فَاعْتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَاءِ الْجَحِيمِ﴿٤٧﴾
47. (Itaamrishwa): “Mchukueni (kafiri) na msokomezeni katikati ya (Moto wa) Al-Jahiym.


ثُمَّ صُبُّوا فَوْقَ رَأْسِهِ مِنْ عَذَابِ الْحَمِيمِ﴿٤٨﴾
48. “Kisha mwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yachemkayo.”


ذُقْ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْكَرِيمُ﴿٤٩﴾
49. (Itasemwa): “Onja! Hakika wewe ni mwenye nguvu mheshimiwa.


إِنَّ هَـٰذَا مَا كُنتُم بِهِ تَمْتَرُونَ﴿٥٠﴾
50. “Hakika haya ambayo mlikuwa mkiyatilia shaka.”


إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٍ﴿٥١﴾

51. Hakika wenye taqwa wako katika mahali pa amani.


فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ﴿٥٢﴾
52. Katika Jannaat na chemchemu.


يَلْبَسُونَ مِن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَقَابِلِينَ﴿٥٣﴾
53. Watavaa hariri laini na hariri nzito nyororo wakiwa wamekabiliana.


كَذَٰلِكَ وَزَوَّجْنَاهُم بِحُورٍ عِينٍ﴿٥٤﴾
54. Hivyo ndivyo!  Na Tutawaozesha huwrin ’iyn (wanawake wa Jannah wenye macho ya kupendeza).


يَدْعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَاكِهَةٍ آمِنِينَ﴿٥٥﴾
55. Wataagiza humo kila (aina ya) matunda wakiwa katika amani.


لَا يَذُوقُونَ فِيهَا الْمَوْتَ إِلَّا الْمَوْتَةَ الْأُولَىٰ ۖ وَوَقَاهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ﴿٥٦﴾
56. Hawatoonja humo mauti isipokuwa mauti yale ya awali (ya duniani), na (Allaah) Atawakinga na adhabu ya (Moto wa) Al-Jahiym.


فَضْلًا مِّن رَّبِّكَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٥٧﴾
57. Ni fadhila kutoka kwa Rabb (Mola) wako.  Huko ndiko kufuzu adhimu.


فَإِنَّمَا يَسَّرْنَاهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ﴿٥٨﴾
58. Basi hakika Tumeiwepesisha (Qur-aan) kwenye lisani yako ili wapate kukumbuka.


فَارْتَقِبْ إِنَّهُم مُّرْتَقِبُونَ﴿٥٩﴾
59. Basi ngojea uchunge (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), hakika wao (pia) ni wenye kungojea wakichunga.  





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com