Hapa
tutasita katika mlango wa elimu kabla ya kauli na amali katika kitabu cha
sahihi Bukhari.
Imam
Bukhari ameuita mlango huu kuwa ni elimu kabla ya kauli na amali – vitendo. Muislamu
hutakiwa kwanza ajifunze kabla ya kutenda au kusema jambo lolote linalohusu
dini yetu na tutachukua baadhi ya aya na hadithi zinazoonesha umuhimu huu.
Anasema Allah
Subhaanahu Wata’ala katika Qur’aan Al Mujaadalah /11
يَرْفَعِ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا
الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ
Allah
atawainua walioamini miongoni mwenu, na walio pewa elimu daraja za juu. Na
Allah anazo khabari za mnayoyatenda
Na anasema
katika Suuraatu Muhammad/19
فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا
إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ
Basi
jua ya kwamba hapana Mungu ila Allah
وأن العلماء هم ورثة الأنبياء، ورثوا العلم، من أخذه أخذه بحظ وافر،
ومن سلك
يطلب به علما سهل الله له طريقا إلى الجنة
Hakika Maulamaa ni warithi wa Mitume kwani wamerithi elimu na
mwenye kuichukua basi ameichukua akiwa na bahati nzuri . Na
atakaenyoosha njia kutafuta ndani yake elimu basi Allah humuwepesishia njia
ya kwenda peponi.
Katika
Suuratu Faatir/28
إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ
الْعُلَمَاء
Kwa hakika wanao mcha Allah miongoni mwa waja wake ni Wanazuoni -
Maulamaa
Al
Ankaboot /43
وَمَا
يَعْقِلُهَا إِلَّا الْعَالِمُونَ
Na hawaifahamu ila wenye elimu
Al Mulk/10
وَقَالُوا لَوْ كُنَّا نَسْمَعُ أَوْ نَعْقِلُ مَا كُنَّا فِي أَصْحَابِ
السَّعِيرِ
Na watasema: Lau kuwa tungelisikia, au tungelikuwa na akili,
tusingelikuwa katika watu wa Motoni!
Azzumar/9
قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ
Sema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua?
وقال النبي صلى الله عليه وسلم: (من يرد الله به خيرا يفقهه في الدين)
Mwenye kutakiwa kheri na Allah basi humpa maarifa na upeo katika
dini.
و(إنما العلم بالتعلم).
Hakika ya elimu ni kwa kujifundisha
Mwisho wa
kunukuu kutoka kitabu cha sahihi Bukhari.
Pia Anasema
Mtume Salla Allahu ‘Alayhi Wasallam katika hadithi maarufu kwamba :
: ( طَلَبُ الْعِلْمِ فَرِيضَةٌ عَلَى كُلِّ
مُسْلِمٍ ) وصححه الألباني في صحيح سنن ابن ماجة
“Kutafuta
elimu ni wajibu kwa kila muislamu.”
Ameisahihisha
Sh Albani katika Sahihi za sunnan Ibnu Majah
Kutafuta
elimu ni ibada. Allah Subhaanahu Wata’ala anaabudiwa pia kwa kutafuta elimu.
Na hizi tulizozitaja ni fadhila chache tu za mwenye kufanya hima katika kutafuta
elimu.
Tumuombe
Allah Subhaanahu Wata’ala atujaalie miongoni mwa wanaoitafuta elimu ya dini
yetu tuweze kuijua na kuifahamu kama walivyoifahamu waliokuwa kabla yetu.
Tumuombe Allah Subhaanahu Wata’ala atupe hima na hamu ya kusoma na kuifahamu
vyema elimu ya dini yetu.
Amin!.
|
Fadhila za Mwenye Kutafuta Elimu
Subscribe to:
Posts (Atom)