Nuwh (71)


سُورَةُ  النُّوح
Nuwh (71)
(Imeteremka Makka)
  Sura hii tukufu imefafanua kisa cha Nuh'u a.s. pamoja na kaumu yake. Ikasimulia khabari za wito wake kwa dhaahiri, kisha kwa siri na kwa dhaahiri. Na ikaeleza mashtaka yake kumshtakia Mwenyezi Mungu juu ya walivyo mpuuza, na inda walio mfanyia, na ikasajili kukakamia kwao kuyaabudu masanamu mpaka wakastahiki kupata adhabu ya Mwenyezi Mungu. Nuh'u alipo kata tamaa nao kuukubali wito wake, aliwaapiza wahiliki na waangamie, na akajiombea nafsi yake, na wanawe, Waumini wanaume, na Waumini wanawake, wapate msamaha.



 
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

إِنَّا أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ أَنْ أَنذِرْ قَوْمَكَ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١﴾

1. Hakika Sisi Tumemtuma Nuwh kwa watu wake kwamba: waonye watu wako kabla haijawafikia adhabu iumiazyo.

قَالَ يَا قَوْمِ إِنِّي لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٢﴾

2. (Nuwh) Akasema: “Enyi watu wangu! Hakika mimi kwenu ni mwonyaji bayana.

أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاتَّقُوهُ وَأَطِيعُونِ ﴿٣﴾

3. “Kwamba muabuduni Allaah, na mcheni, na mnitii.

يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرْكُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ إِنَّ أَجَلَ اللَّـهِ إِذَا جَاءَ لَا يُؤَخَّرُ ۖ لَوْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٤﴾

4. “(Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakuakhirisheni mpaka wakati maalumu uliopangwa. Hakika ajali (iliyopangwa na) Allaah itakapokuja haitoakhirishwa, lau kama mtakuwa mnajua.”

قَالَ رَبِّ إِنِّي دَعَوْتُ قَوْمِي لَيْلًا وَنَهَارًا ﴿٥﴾

5. (Nuwh) Akasema: “Rabb (Mola) wangu! Hakika mimi nimewalingania watu wangu usiku na mchana.

فَلَمْ يَزِدْهُمْ دُعَائِي إِلَّا فِرَارًا ﴿٦﴾

6. “Lakini haikuwazidishia wito wangu isipokuwa kukimbia.

وَإِنِّي كُلَّمَا دَعَوْتُهُمْ لِتَغْفِرَ لَهُمْ جَعَلُوا أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِمْ وَاسْتَغْشَوْا ثِيَابَهُمْ وَأَصَرُّوا وَاسْتَكْبَرُوا اسْتِكْبَارًا ﴿٧﴾

7. “Na hakika mimi kila nilipowaita ili Uwaghufurie; huweka vidole vyao masikioni mwao (ili wasisikie), na wakagubika nguo zao, na wakashikilia (kukanusha) wakatakabari kwa kutakabari kukubwa mno.


ثُمَّ إِنِّي دَعَوْتُهُمْ جِهَارًا ﴿٨﴾

8. “Kisha hakika mimi niliwalingania kwa jahari (waziwazi).

ثُمَّ إِنِّي أَعْلَنتُ لَهُمْ وَأَسْرَرْتُ لَهُمْ إِسْرَارًا ﴿٩﴾

9. “Kisha hakika mimi nikawatangazia na nikawasemesha kwa siri.

فَقُلْتُ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا ﴿١٠﴾

10. Nikasema: “Ombeni maghfirah kwa Rabb (Mola) wenu; hakika Yeye ni Ghaffaaraa (Mwingi wa kughufuria).

يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا ﴿١١﴾

11. “Atakutumieni mawingu (mvua) tele ya kuendelea.

وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَارًا ﴿١٢﴾

12. “Na Atakuongezeeni mali na wana, na Atakujaalieni mabustani na Atakujaalieni mito mingi.”

مَّا لَكُمْ لَا تَرْجُونَ لِلَّـهِ وَقَارًا ﴿١٣﴾

13. Mna nini (nyie, hata mkawa) hamtaraji kwa Allaah heshima?

وَقَدْ خَلَقَكُمْ أَطْوَارًا ﴿١٤﴾

14. Na hali Amekuumbeni hatua baada ya hatua?

أَلَمْ تَرَوْا كَيْفَ خَلَقَ اللَّـهُ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا ﴿١٥﴾

15. Je, hamuoni vipi Allaah Ameumba mbingu saba tabaka tabaka?

وَجَعَلَ الْقَمَرَ فِيهِنَّ نُورًا وَجَعَلَ الشَّمْسَ سِرَاجًا ﴿١٦﴾

16. Na Akaufanya mwezi ndani yake (wenye) nuru, na Akalifanya jua (kuwa ni) taa ya mwanga mkali.

وَاللَّـهُ أَنبَتَكُم مِّنَ الْأَرْضِ نَبَاتًا ﴿١٧﴾

17. Na Allaah Amekuotesheni katika ardhi muotesho (kama mimea).


ثُمَّ يُعِيدُكُمْ فِيهَا وَيُخْرِجُكُمْ إِخْرَاجًا ﴿١٨﴾

18. Kisha Atakurudisheni humo (ardhini), na Atakutoeni (tena) mtoke  (kuwa hai Siku ya kufufuliwa).

وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ بِسَاطًا ﴿١٩﴾

19. Na Allaah Amekufanyieni ardhi kuwa (kama) busati.

لِّتَسْلُكُوا مِنْهَا سُبُلًا فِجَاجًا ﴿٢٠﴾

20. Ili mfuate humo njia pana.

قَالَ نُوحٌ رَّبِّ إِنَّهُمْ عَصَوْنِي وَاتَّبَعُوا مَن لَّمْ يَزِدْهُ مَالُهُ وَوَلَدُهُ إِلَّا خَسَارًا ﴿٢١﴾

21. Nuwh Akasema: “Rabb (Mola) wangu! Hakika wao wameniasi, na wakafuata yule ambaye mali yake na auladi wake hawakumzidishia isipokuwa khasara.

وَمَكَرُوا مَكْرًا كُبَّارًا ﴿٢٢﴾

22. “Na wakapanga njama kubwa.

وَقَالُوا لَا تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلَا سُوَاعًا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا ﴿٢٣﴾

23. Wakasema: “Msiwaache miungu yenu; na wala msimwache Waddaa, na wala Su’waa’a, na wala Yaghuwtha, na Ya’uwqa, na Nasraa.

وَقَدْ أَضَلُّوا كَثِيرًا ۖ وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا ضَلَالًا ﴿٢٤﴾

24. “Na wamekwishawapoteza (watu) wengi; (ee Rabb wangu!) Na wala Usiwazidishie madhalimu isipokuwa upotofu.”

مِّمَّا خَطِيئَاتِهِمْ أُغْرِقُوا فَأُدْخِلُوا نَارًا فَلَمْ يَجِدُوا لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ أَنصَارًا ﴿٢٥﴾

25. Kutokana na makosa yao; walizamishwa, kisha wakaingizwa Motoni, basi hawakupata mwenye kuwanusuru yeyote yule badala ya Allaah.

وَقَالَ نُوحٌ رَّبِّ لَا تَذَرْ عَلَى الْأَرْضِ مِنَ الْكَافِرِينَ دَيَّارًا ﴿٢٦﴾

26. Na Nuwh akasema (tena): “Rabb (Mola) wangu! Usimwache juu ya ardhi mkaazi yeyote yule kati ya makafiri.

إِنَّكَ إِن تَذَرْهُمْ يُضِلُّوا عِبَادَكَ وَلَا يَلِدُوا إِلَّا فَاجِرًا كَفَّارًا ﴿٢٧﴾

27. “Hakika Wewe Ukiwaacha, watawapoteza waja Wako, na wala hawatozaa isipokuwa muovu kafiri.

رَّبِّ اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيْتِيَ مُؤْمِنًا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا تَبَارًا ﴿٢٨﴾

28. “Rabb (Mola) wangu! Nighufurie, na wazazi wangu wawili, na kila aliyeingia nyumbani mwangu mwenye kuamini, na Waumini wa kiume na Waumini wa kike, na wala Usiwazidishie madhalimu isipokuwa maangamizi.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com