At-Tawbah: 9

التَّوْبَة
At-Tawbah: 9

(Imeteremka Madina)


Suratut Tawba iliteremka Madina katika mwaka wa tisa wa Hijra, yaani miaka tisa baada ya Mtume s.a.w. kuhamia Madina. Akaichukua Sura hii Ali bin Abi Talib r.a. kuwapelekea Waislamu katika Hija na akawasomea. Na amir, yaani mwongozi, wa Hija hiyo alikuwa Abu Bakr Assidiq r.a. Na Aya zake ni 129. Imeanzia kwa kujitenga Mwenyezi Mungu Mtukufu na washirikina. Na kwa hivyo ikaitwa pia Sura ya Baraa-ah, yaani kujitenga, kutokuwa na dhima, kutokuwa na jukumu. Na baada ya hayo ikataja utakatifu wa miezi mitakatifu, na ahadi za washirikina, na ipasavyo kutimiza ahadi nao ikiwa wao hawajaivunja. Na mwenye kuvunja ahadi yapasa kupigana naye. Na baada ya hayo ikabainisha kuwa kiini cha kutaka kumkaribia Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kumuamini Yeye. Na Imani haikamiliki ila akiwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapendwa na Waumini kuliko kila kitu. Naye Subhanahu ametaja kuwa kujiona una nguvu ndio kunapelekea kuwa mbali ushindi, na akaashiria mfano wa vita vya Hunayni.  Katika Sura hii wamepigiwa marfuku washirikina wasiingie katika Msikiti Mtakatifu wa Makka, kwa kuwa wao ni najisi!
Na katika Sura hii imetajwa kupasa kuwapiga vita Mayahudi na Wakristo mpaka watoe jizya, kodi ya kichwa, na imebainishwa idadi ya miezi mitakatifu. Na humu imebainishwa dharura ya kutoka kwenda vitani kila vikinadiwa bila ya kulegalega. Na humo imeashiriwa hukumu ya wanao bakia nyuma, na walemevu wasio weza kwenda kupigana, na imebainishwa hali ya wanaafiki ambao wanatafuta fitna kila wakati vinapo nadiwa vita. Na Mwenyezi Mungu akataja wanaafiki wanavyo watendea Waumini wakati wa salama na vita.
Katika Sura hii iko amri ya kukata iliyo tangazwa kuwatia adabu wanaafiki. Nayo ni kuwa Mtume s.a.w. asimsalie yeyote katika wanaafiki akifa.  Naye Subhanahu ametaja udhuru unao mstahikia mtu kubaki nyuma asende vitani. Na pia Subhanahu ameeleza hali ya wale mabedui walio dhihirisha kuingia katika Uislamu, au wakafuata hukumu zake, baada ya kuwa Uislamu umepata nguvu. Na akaeleza kuwa hao mabedui wako kando kando ya Madina.
Na baada ya hayo ametaja hali za watu kwa mnasaba wa Imani. Na akataja khabari ya Msikiti wa Madhara walio ujenga wanaafiki ili upuuzwe  Msikiti alio ujenga Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w. Kisha Subhanahu akataja sifa za Waumini walio wakweli katika Imani yao, na toba ya wale walio mkhalifu Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w., na Mwenyezi Mungu akakubali toba hiyo, kama alivyo taja Subhanahu wa Taa'la hali za watu katika kuzipokea Aya za Qur'ani zinapo teremka. Na Subhanahu wa Taala akakhitimisha Sura hii kwa kusema kuwa hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amemteua Muhammad kwa kumpa Utume, na kwamba yeye hawatakii shida hao alio tumwa kwao, na kwamba yeye ni mpole na mwenye huruma kwao, na kwamba ikiwa wakigeuka basi Mwenyezi Mungu anamtosheleza. (Angalia: Sura hii peke yake ndiyo haianzii kwa Bismillahi, Kwa Jina la Mwenyezi Mungu.)
 




بَرَاءَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ إِلَى الَّذِينَ عَاهَدتُّم مِّنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١﴾
1. (Hili ni tangazo la) Kujitoa katika dhima kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa washirikina.


فَسِيحُوا فِي الْأَرْضِ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِي اللَّـهِ ۙ وَأَنَّ اللَّـهَ مُخْزِي الْكَافِرِينَ﴿٢﴾
2. Basi tembeeni (kwa uhuru enyi makafiri) katika ardhi miezi minne; na jueni kwamba nyinyi hamuwezi kushinda kumwepuka Allaah na kwamba Allaah ni Mwenye kuwahizi makafiri.


وَأَذَانٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ إِلَى النَّاسِ يَوْمَ الْحَجِّ الْأَكْبَرِ أَنَّ اللَّـهَ بَرِيءٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ ۙ وَرَسُولُهُ ۚ فَإِن تُبْتُمْ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِي اللَّـهِ ۗ وَبَشِّرِ الَّذِينَ كَفَرُوا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣﴾
3. Na ni tangazo kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake kwa watu siku ya Hajj kubwa, kwamba Allaah Hana dhima na washirikina na Rasuli Wake (pia hana dhima). Basi mkitubu, hiyo ni kheri kwenu; na mkikengeuka, basi jueni kwamba nyinyi hamuwezi kushinda kumwepuka Allaah. Na wabashirie wale waliokufuru kwa adhabu iumizayo. 


إِلَّا الَّذِينَ عَاهَدتُّم مِّنَ الْمُشْرِكِينَ ثُمَّ لَمْ يَنقُصُوكُمْ شَيْئًا وَلَمْ يُظَاهِرُوا عَلَيْكُمْ أَحَدًا فَأَتِمُّوا إِلَيْهِمْ عَهْدَهُمْ إِلَىٰ مُدَّتِهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ﴿٤﴾
4. Isipokuwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa washirikina, kisha hawakukupunguzieni chochote na wala hawakumsaidia yeyote dhidi yenu, basi watimizieni ahadi yao mpaka muda wao (umalizike). Hakika Allaah Anapenda wenye taqwa.


فَإِذَا انسَلَخَ الْأَشْهُرُ الْحُرُمُ فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ وَخُذُوهُمْ وَاحْصُرُوهُمْ وَاقْعُدُوا لَهُمْ كُلَّ مَرْصَدٍ ۚ فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٥﴾
5. Itapomalizika miezi mitukufu, basi waueni washirikina popote muwakutapo, na wachukueni (mateka) na wahusuruni, na wakalieni katika kila sehemu ya uvamizi. Lakini wakitubu, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah, basi iacheni njia yao (huru, waachieni). Hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ أَبْلِغْهُ مَأْمَنَهُ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْلَمُونَ﴿٦﴾
6. Na ikiwa mmoja wa washirikina akikuomba umlinde, basi mlinde mpaka asikie Maneno ya Allaah (Qur-aan), kisha mfikishe mahali pake pa amani. Hivyo kwa kuwa wao ni watu wasiojua.


كَيْفَ يَكُونُ لِلْمُشْرِكِينَ عَهْدٌ عِندَ اللَّـهِ وَعِندَ رَسُولِهِ إِلَّا الَّذِينَ عَاهَدتُّمْ عِندَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۖ فَمَا اسْتَقَامُوا لَكُمْ فَاسْتَقِيمُوا لَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ﴿٧﴾
7. Vipi iweko ahadi na washirikina mbele ya Allaah na mbele ya Rasuli Wake isipokuwa wale mlioahidiana mbele ya Al-Masjidil-Al-Haraam. Basi wakikunyokeeni (kwa uzuri), nanyi wanyokeeni (kwa uzuri). Hakika Allaah Anapenda wenye taqwa.


كَيْفَ وَإِن يَظْهَرُوا عَلَيْكُمْ لَا يَرْقُبُوا فِيكُمْ إِلًّا وَلَا ذِمَّةً ۚ يُرْضُونَكُم بِأَفْوَاهِهِمْ وَتَأْبَىٰ قُلُوبُهُمْ وَأَكْثَرُهُمْ فَاسِقُونَ﴿٨﴾
8. Vipi (mtashikamana na mkataba) hali wakikushindeni hawachungi kwenu udugu wa damu wala ahadi ya himaya?  Wanakuridhisheni kwa midomo yao, na hali nyoyo zao zinakataa; na wengi wao ni mafasiki.


اشْتَرَوْا بِآيَاتِ اللَّـهِ ثَمَنًا قَلِيلًا فَصَدُّوا عَن سَبِيلِهِ ۚ إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩﴾
9. Wamebadili Aayaat za Allaah kwa thamani ndogo, na wakazuilia (watu) njia Yake. Hakika ni maovu waliyokuwa wakitenda.


لَا يَرْقُبُونَ فِي مُؤْمِنٍ إِلًّا وَلَا ذِمَّةً ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُعْتَدُونَ﴿١٠﴾
10. Hawachungi kwa Muumini udugu wa damu wala ahadi ya himaya. Na hao ndio wenye kutaadi.


فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ ۗ وَنُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ﴿١١﴾
11. Wakitubu, na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa Zakaah; basi ni ndugu zenu katika Dini. Na Tunafasili Aayaat kwa watu wanaojua.


وَإِن نَّكَثُوا أَيْمَانَهُم مِّن بَعْدِ عَهْدِهِمْ وَطَعَنُوا فِي دِينِكُمْ فَقَاتِلُوا أَئِمَّةَ الْكُفْرِ ۙ إِنَّهُمْ لَا أَيْمَانَ لَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَنتَهُونَ﴿١٢﴾
12. Na wakivunja viapo vyao baada ya ahadi yao, na wakatukana Dini yenu, basi wapigeni vita viongozi wa ukafiri. Hakika viapo vyao havina maana. (Piganeni nao) ili wapate kukoma (maovu).


أَلَا تُقَاتِلُونَ قَوْمًا نَّكَثُوا أَيْمَانَهُمْ وَهَمُّوا بِإِخْرَاجِ الرَّسُولِ وَهُم بَدَءُوكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۚ أَتَخْشَوْنَهُمْ ۚ فَاللَّـهُ أَحَقُّ أَن تَخْشَوْهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١٣﴾
13. Je, hamtopigana na watu waliovunja viapo vyao, na wakafanya hima kumtoa Rasuli, nao ndio waliokuanzeni mara ya kwanza? Je, mnawaogopa?  Basi Allaah Anastahiki zaidi mumwogope ikiwa nyinyi ni Waumini.


قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللَّـهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ﴿١٤﴾
14. Piganeni nao, Allaah Atawaadhibu kwa mikono yenu, na Atawahizi na Atakunusuruni dhidi yao, na Atapozesha vifua vya Waumini.  


وَيُذْهِبْ غَيْظَ قُلُوبِهِمْ ۗ وَيَتُوبُ اللَّـهُ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿١٥﴾
15. Na Ataondosha ghaidhi za nyoyo zao (Waumini); na Allaah Anapokea tawbah kwa Amtakaye, na Allaah ni ‘Aliymun-Hakiym (Mjuzi wa yote – Mwenye hikmah wa yote).


أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تُتْرَكُوا وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّـهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنكُمْ وَلَمْ يَتَّخِذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَا رَسُولِهِ وَلَا الْمُؤْمِنِينَ وَلِيجَةً ۚ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴿١٦﴾
16. Je, mmedhani kuwa mtaachwa na hali Allaah Hakuwadhihirisha wale waliofanya jihaad miongoni mwenu; na hawakufanya rafiki mwandani isipokuwa Allaah na Rasuli Wake na Waumini (wenzao)? Na Allaah ni Khabiyr (Mjuzi wa yaliyodhahiri na yaliyofichikana) kwa yale myatendayo.


مَا كَانَ لِلْمُشْرِكِينَ أَن يَعْمُرُوا مَسَاجِدَ اللَّـهِ شَاهِدِينَ عَلَىٰ أَنفُسِهِم بِالْكُفْرِ ۚ أُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ وَفِي النَّارِ هُمْ خَالِدُونَ﴿١٧﴾
17. Haiwi kwa washirikina kuamirisha Misikiti ya Allaah hali wanajishuhudia nafsi zao kwa ukafiri. Hao zimebatilika ‘amali zao na katika Moto wao ni wenye kudumu.


إِنَّمَا يَعْمُرُ مَسَاجِدَ اللَّـهِ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَلَمْ يَخْشَ إِلَّا اللَّـهَ ۖ فَعَسَىٰ أُولَـٰئِكَ أَن يَكُونُوا مِنَ الْمُهْتَدِينَ﴿١٨﴾
18. Hakika wanaoamirisha Misikiti ya Allaah ni (wale) wanaomwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah na hawamkhofu (yeyote) isipokuwa Allaah. Basi huenda hao wakawa miongoni mwa walioongoka.


أَجَعَلْتُمْ سِقَايَةَ الْحَاجِّ وَعِمَارَةَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ كَمَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَجَاهَدَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ لَا يَسْتَوُونَ عِندَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿١٩﴾
19. Je, mmefanya (‘amali ya) kunywesha maji mahujaji na kuamirisha Al-Masjid Al-Haraam kama (ni sawa na ‘amali za) anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na akafanya jihaad katika njia ya Allaah? (Hapana!) Hawawi sawa mbele ya Allaah. Na Allaah Haongoi watu madhalimu.


الَّذِينَ آمَنُوا وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ أَعْظَمُ دَرَجَةً عِندَ اللَّـهِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَائِزُونَ﴿٢٠﴾
20. Wale walioamini na wakahajiri na wakafanya jihaad katika njia ya Allaah kwa mali zao na nafsi zao; wana daraja kuu kwa Allaah. Na hao ndio waliofuzu.


يُبَشِّرُهُمْ رَبُّهُم بِرَحْمَةٍ مِّنْهُ وَرِضْوَانٍ وَجَنَّاتٍ لَّهُمْ فِيهَا نَعِيمٌ مُّقِيمٌ﴿٢١﴾
21. Rabb (Mola) wao Anawabashiria kwa Rahmah kutoka Kwake na Radhi (Zake) na Jannaat watapata humo neema (za kila aina) zenye kudumu.


خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ﴿٢٢﴾
22. Ni wenye kudumu humo abadi. Hakika Allaah Kwake kuna ujira adhimu.


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا آبَاءَكُمْ وَإِخْوَانَكُمْ أَوْلِيَاءَ إِنِ اسْتَحَبُّوا الْكُفْرَ عَلَى الْإِيمَانِ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿٢٣﴾
23. Enyi mlioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu awliyaa (wandani, walinzi) ikiwa wanapendelea ukafiri badala ya Iymaan. Na yeyote miongoni mwenu atakayewafanya awliyaa (wandani, walinzi) basi hao ndio madhalimu.


قُلْ إِن كَانَ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ وَإِخْوَانُكُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَالٌ اقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَارَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَاكِنُ تَرْضَوْنَهَا أَحَبَّ إِلَيْكُم مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَجِهَادٍ فِي سَبِيلِهِ فَتَرَبَّصُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴿٢٤﴾
24. Sema: “Ikiwa baba zenu na watoto wenu na ndugu zenu na wake (au waume) zenu na jamaa zenu na mali mliyoichuma na biashara mnayoikhofia kuharibika kwake, na majumba mnayoridhika nayo, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Allaah na Rasuli Wake na kufanya jihaad katika njia Yake; basi ngojeeni mpaka Allaah Alete Amri Yake (ya adhabu). Na Allaah Haongoi watu mafasiki.


لَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّـهُ فِي مَوَاطِنَ كَثِيرَةٍ ۙ وَيَوْمَ حُنَيْنٍ ۙ إِذْ أَعْجَبَتْكُمْ كَثْرَتُكُمْ فَلَمْ تُغْنِ عَنكُمْ شَيْئًا وَضَاقَتْ عَلَيْكُمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ ثُمَّ وَلَّيْتُم مُّدْبِرِينَ﴿٢٥﴾
25. Kwa yakini Amekunusuruni Allaah katika maeneo mengi, na Siku ya (vita vya) Hunayn (pia); ulipokupendezeni wingi wenu (kwa kujigamba), lakini haukukufaeni chochote; na ardhi ikawa dhiki juu yenu juu ya upana wake, kisha mkageuka na kurudi nyuma (mkakimbia).


ثُمَّ أَنزَلَ اللَّـهُ سَكِينَتَهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ وَعَلَى الْمُؤْمِنِينَ وَأَنزَلَ جُنُودًا لَّمْ تَرَوْهَا وَعَذَّبَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْكَافِرِينَ﴿٢٦﴾
26. Kisha Allaah Akateremsha utulivu Wake kwa Rasuli Wake na kwa Waumini, na Akateremsha majeshi (ya Malaika) msiyoyaona; na Akawaadhibu wale waliokufuru. Na hivyo ndio jazaa ya makafiri.


ثُمَّ يَتُوبُ اللَّـهُ مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٢٧﴾
27. Kisha Allaah Anapokea tawbah baada ya hapo kwa Amtakaye. Na Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَـٰذَا ۚ وَإِنْ خِفْتُمْ عَيْلَةً فَسَوْفَ يُغْنِيكُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ إِن شَاءَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٢٨﴾
28. Enyi mlioamini!  Hakika washirikiana ni najisi, basi wasikaribie Al-Masjid Al-Haraam baada ya mwaka wao huu. Na mkikhofu umasikini basi Allaah Atakutajirisheni kutokana na fadhila Zake Akitaka. Hakika Allaah ni ‘Aliymun-Hakiym (Mjuzi wa yote – Mwenye hikmah wa yote).


قَاتِلُوا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَلَا يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَلَا يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حَتَّىٰ يُعْطُوا الْجِزْيَةَ عَن يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ﴿٢٩﴾
29. Piganeni na wale wasiomwamini Allaah na wala Siku ya Mwisho, na wala hawaharamishi Aliyoyaharamisha Allaah na Rasuli Wake, na wala hawafuati Dini ya haki miongoni mwa wale waliopewa Kitabu, (piganeni nao) mpaka watoe jizyah (kodi) kwa khiyari, na hali wamerudi chini (kutii amri).


وَقَالَتِ الْيَهُودُ عُزَيْرٌ ابْنُ اللَّـهِ وَقَالَتِ النَّصَارَى الْمَسِيحُ ابْنُ اللَّـهِ ۖ ذَٰلِكَ قَوْلُهُم بِأَفْوَاهِهِمْ ۖ يُضَاهِئُونَ قَوْلَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَبْلُ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّـهُ ۚ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ﴿٣٠﴾
30. Na Mayahudi wanasema: “‘Uzayr ni mwana wa Allaah”; na Manaswara wanasema: “Al-Masiyh (‘Iysaa) ni mwana wa Allaah.” Hiyo ni kauli yao kwa midomo yao. Wanaiga kauli ya wale waliokufuru kabla. Allaah Awaangamize! Basi namna gani wanavyoghilibiwa?


اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٣١﴾
31. Wamewafanya Ahbaar wao (Wanavyuoni mafuqahaa wa dini) na Ruhbaan  wao (Wamonaki - watawa) kuwa ni miungu badala ya Allaah, na (pia wamemfanya) Al-Masiyh mwana wa Maryam (kuwa ni mungu); na hali hawakuamrishwa isipokuwa kumwabudu Ilaah (Muabudiwa wa haki) Mmoja (Pekee). Hapana ilaaha ila Yeye. Subhaanah! (Utakasifu ni Wake!) kutokana na yale yote wanayomshirkisha nayo.  


يُرِيدُونَ أَن يُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّـهُ إِلَّا أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ﴿٣٢﴾
32. Wanataka kuzima nuru ya Allaah kwa midomo yao; lakini Allaah Anakataa isipokuwa Atimize nuru Yake, japo watakirihika makafiri.


هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿٣٣﴾
33. Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina.


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ كَثِيرًا مِّنَ الْأَحْبَارِ وَالرُّهْبَانِ لَيَأْكُلُونَ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۗ وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣٤﴾
34. Enyi mlioamini! Hakika wengi katika al-Ahbaar (Wanavyuoni mafuqahaa wa dini) na ar-Ruhbaan (Wamonaki - watawa) wanakula mali za watu kwa batili, na wanazuilia (watu) njia ya Allaah. Na wale wanaorundika (hazina za) dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika njia ya Allaah, basi wabashirie adhabu iumizayo. 


يَوْمَ يُحْمَىٰ عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنُوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ ۖ هَـٰذَا مَا كَنَزْتُمْ لِأَنفُسِكُمْ فَذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَكْنِزُونَ﴿٣٥﴾
35. Siku (mali zao) zitakapopashwa katika Moto wa Jahannam, kisha kwa hayo vikachomwa Moto vipaji vyao, na mbavu zao, na migongo yao (huku wakiambiwa): “Haya ndiyo mliyoyarundika kwa ajili ya nafsi zenu. Basi onjeni yale mliyokuwa mkiyarundika.


إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِندَ اللَّـهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِي كِتَابِ اللَّـهِ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ ۚ فَلَا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ ۚ وَقَاتِلُوا الْمُشْرِكِينَ كَافَّةً كَمَا يُقَاتِلُونَكُمْ كَافَّةً ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ﴿٣٦﴾
36. Hakika idadi ya miezi mbele ya Allaah ni kumi na mbili katika hukmu ya makadirio ya Allaah, (tangu) siku Aliyoumba mbingu na ardhi. Kati ya hiyo, (iko miezi) minne mitukufu. Hivyo ndiyo Dini iliyo nyoofu. Basi msijidhulumu humo nafsi zenu (kwa kufanya maasi), na piganeni vita na washirikina wote kama wao wanavyokupigeni vita nyote. Na jueni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa.


إِنَّمَا النَّسِيءُ زِيَادَةٌ فِي الْكُفْرِ ۖ يُضَلُّ بِهِ الَّذِينَ كَفَرُوا يُحِلُّونَهُ عَامًا وَيُحَرِّمُونَهُ عَامًا لِّيُوَاطِئُوا عِدَّةَ مَا حَرَّمَ اللَّـهُ فَيُحِلُّوا مَا حَرَّمَ اللَّـهُ ۚ زُيِّنَ لَهُمْ سُوءُ أَعْمَالِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ﴿٣٧﴾
37. Hakika kuahirisha (au kuizuia miezi mitukufu) ni kuzidi katika kufuru. Hupotezwa kwayo wale waliokufuru, wanauhalalisha (mwezi mtukufu) mwaka na wanauharamisha mwaka (mwingine) ili kuusawazisha na idadi ya (miezi) Aliyoitukuza Allaah. Basi huhalalisha Alivyoviharamisha Allaah. Wamepambiwa uovu wa ‘amali zao. Na Allaah Haongoi watu makafiri.


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ ۚ أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ ۚ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ﴿٣٨﴾
38. Enyi mlioamini! Mna nini mnapoambiwa tokeni mwende (mkapigane) katika njia ya Allaah, mnajitia uzito katika ardhi. Je, mmeridhika na uhai wa dunia kwa ya Aakhirah? Basi starehe za uhai wa dunia kulinganisha na Aakhirah ni chache.


إِلَّا تَنفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَيَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئًا ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٣٩﴾
39. Msipotoka kwenda (kupigana), Atakuadhibuni (Allaah) adhabu iumizayo, na Atabadilisha watu wasiokuwa nyinyi, na wala hamtomdhuru chochote. Na Allaah juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza).


إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدْ نَصَرَهُ اللَّـهُ إِذْ أَخْرَجَهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ثَانِيَ اثْنَيْنِ إِذْ هُمَا فِي الْغَارِ إِذْ يَقُولُ لِصَاحِبِهِ لَا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّـهَ مَعَنَا ۖ فَأَنزَلَ اللَّـهُ سَكِينَتَهُ عَلَيْهِ وَأَيَّدَهُ بِجُنُودٍ لَّمْ تَرَوْهَا وَجَعَلَ كَلِمَةَ الَّذِينَ كَفَرُوا السُّفْلَىٰ ۗ وَكَلِمَةُ اللَّـهِ هِيَ الْعُلْيَا ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٤٠﴾
40. Msipomnusuru (Rasuli), basi Allaah Amekwishamnusuru, pale walipomtoa (Makkah) wale waliokufuru akiwa wa pili katika wawili; walipokuwa (yeye na Abu Bakr) katika pango, alipomwambia swahibu yake: “Usihuzunike, hakika Allaah Yu Pamoja nasi.” Basi Allaah Akamteremshia utulivu Wake, na Akamsaidia kwa majeshi msiyoyaona (Malaika), na Akajaalia neno la waliokufuru (kuwa) chini. Na Neno la Allaah (kuwa) ndilo lililo juu. Na Allaah ni ‘Aziyzun-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika - Mwenye hikmah wa yote).


انفِرُوا خِفَافًا وَثِقَالًا وَجَاهِدُوا بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿٤١﴾
41. Tokeni mwende (vitani) mkiwa wepesi na (mkiwa) wazito, na fanyeni jihaad kwa mali zenu na nafsi zenu katika njia ya Allaah.  Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua.


لَوْ كَانَ عَرَضًا قَرِيبًا وَسَفَرًا قَاصِدًا لَّاتَّبَعُوكَ وَلَـٰكِن بَعُدَتْ عَلَيْهِمُ الشُّقَّةُ ۚ وَسَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَوِ اسْتَطَعْنَا لَخَرَجْنَا مَعَكُمْ يُهْلِكُونَ أَنفُسَهُمْ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ﴿٤٢﴾
42. Kama ingelikuwa pato la karibu (ghanima za vita) na safari ya wastani (nyepesi ya karibu) basi (wanafiki) wangelikufuata; lakini imekuwa ni ya masafa ya mbali kwao na ina mashaka. Na watakuapia kwa Jina la Allaah: “Lau tungeliweza, bila shaka tungelitoka pamoja nanyi.” Wanaangamiza nafsi zao (kubakia nyuma na viapo vya uongo); na Allaah Anajua kwamba wao bila shaka ni waongo.


عَفَا اللَّـهُ عَنكَ لِمَ أَذِنتَ لَهُمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكَ الَّذِينَ صَدَقُوا وَتَعْلَمَ الْكَاذِبِينَ﴿٤٣﴾
43. Allaah Akusamehe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Kwanini umewapa ruhusa (kubakia nyuma)? (Usingelifanya hivyo) Mpaka wakubainikie wale waliosadikishana uwajue waliokadhibisha.


لَا يَسْتَأْذِنُكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ أَن يُجَاهِدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالْمُتَّقِينَ﴿٤٤﴾
44. Hawakuombi ruhusa (ya kubakia nyuma) wale waliomwamini Allaah na Siku ya Mwisho wasifanye jihaad kwa mali zao na nafsi zao. Na Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi) kwa wenye taqwa.


إِنَّمَا يَسْتَأْذِنُكَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَارْتَابَتْ قُلُوبُهُمْ فَهُمْ فِي رَيْبِهِمْ يَتَرَدَّدُونَ﴿٤٥﴾
45. Hakika wanaokuomba ruhusa (ya kubakia nyuma) ni wale ambao hawamwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na nyoyo zao zina shaka, basi wao katika shaka zao wanasitasita.


وَلَوْ أَرَادُوا الْخُرُوجَ لَأَعَدُّوا لَهُ عُدَّةً وَلَـٰكِن كَرِهَ اللَّـهُ انبِعَاثَهُمْ فَثَبَّطَهُمْ وَقِيلَ اقْعُدُوا مَعَ الْقَاعِدِينَ﴿٤٦﴾
46. Na lau wangelitaka kutoka (kwenda vitani), wangeliandaa maandalizi yake, lakini Allaah Amekirihika kutoka kwao, basi Akawazuia na ikasemwa: “Kaeni (mbakie majumbani) pamoja na wanaokaa.”


لَوْ خَرَجُوا فِيكُم مَّا زَادُوكُمْ إِلَّا خَبَالًا وَلَأَوْضَعُوا خِلَالَكُمْ يَبْغُونَكُمُ الْفِتْنَةَ وَفِيكُمْ سَمَّاعُونَ لَهُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ﴿٤٧﴾
47. Lau wangelitoka nanyi, wasingelikuzidishieni isipokuwa machafuko (vurugu, rabsha) na wangeliharakia huku na huku baina yenu kukutakieni fitnah (kukugombanisheni); na miongoni mwenu wako wanaowasikiliza kwa makini (kwa ujasusi). Na Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi) kwa madhalimu.


لَقَدِ ابْتَغَوُا الْفِتْنَةَ مِن قَبْلُ وَقَلَّبُوا لَكَ الْأُمُورَ حَتَّىٰ جَاءَ الْحَقُّ وَظَهَرَ أَمْرُ اللَّـهِ وَهُمْ كَارِهُونَ﴿٤٨﴾
48. Walikwishataka kabla (kukuleteeni) fitnah, na wakakupindulia mambo (chini juu) mpaka ikaja haki na ikadhihirika amri ya Allaah; nao ni wenye kukirihika.


وَمِنْهُم مَّن يَقُولُ ائْذَن لِّي وَلَا تَفْتِنِّي ۚ أَلَا فِي الْفِتْنَةِ سَقَطُوا ۗ وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمُحِيطَةٌ بِالْكَافِرِينَ﴿٤٩﴾
49. Na miongoni mwao yuko anayesema: “Niruhusu (nisiende vitani) na wala usinifitinI”. Tanabahi! Wamekwishaanguka katika fitnah. Na hakika (Moto wa) Jahannam bila shaka utawazunguka makafiri.


إِن تُصِبْكَ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ ۖ وَإِن تُصِبْكَ مُصِيبَةٌ يَقُولُوا قَدْ أَخَذْنَا أَمْرَنَا مِن قَبْلُ وَيَتَوَلَّوا وَّهُمْ فَرِحُونَ﴿٥٠﴾
50. Linapokusibu zuri lolote lile linawachukiza. Na unapokusibu msiba wowote ule, wanasema: “Tumechukua (tahadhari) jambo letu kabla (hatukufikwa na balaa),” na wanageuka (kwenda zao) na huku wanafurahia.


قُل لَّن يُصِيبَنَا إِلَّا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَنَا هُوَ مَوْلَانَا ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ﴿٥١﴾
51. Sema: “Halitusibu (lolote) isipokuwa lile Alilotukidhia Allaah. Yeye ni Mawlaa (Mola, Mlinzi) wetu.” Basi kwa Allaah (Pekee) watawakali Waumini.


قُلْ هَلْ تَرَبَّصُونَ بِنَا إِلَّا إِحْدَى الْحُسْنَيَيْنِ ۖ وَنَحْنُ نَتَرَبَّصُ بِكُمْ أَن يُصِيبَكُمُ اللَّـهُ بِعَذَابٍ مِّنْ عِندِهِ أَوْ بِأَيْدِينَا ۖ فَتَرَبَّصُوا إِنَّا مَعَكُم مُّتَرَبِّصُونَ﴿٥٢﴾
52.  Sema: “Je, mnalo la kungojea kututazamia isipokuwa mojawapo ya mazuri mawili (kushinda vita au tukafa mashahidi)? Na sisi tunangojea kukutazamieni kwamba Allaah Atakusibuni kwa adhabu kutoka Kwake au kutokana na mikono yetu. Basi ngojeeni, nasi tuko pamoja nanyi tunangojea.”


 قُلْ أَنفِقُوا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا لَّن يُتَقَبَّلَ مِنكُمْ ۖ إِنَّكُمْ كُنتُمْ قَوْمًا فَاسِقِينَ﴿٥٣﴾
53. Sema: (kuwaambia wanafiki): “Toeni (mali zenu) kwa khiari au kutokupenda haitokubaliwa kwenu. Hakika nyinyi mmekuwa ni watu mafasiki.”


وَمَا مَنَعَهُمْ أَن تُقْبَلَ مِنْهُمْ نَفَقَاتُهُمْ إِلَّا أَنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّـهِ وَبِرَسُولِهِ وَلَا يَأْتُونَ الصَّلَاةَ إِلَّا وَهُمْ كُسَالَىٰ وَلَا يُنفِقُونَ إِلَّا وَهُمْ كَارِهُونَ﴿٥٤﴾
54. Na haikuwazuilia ikubaliwe kwao michango yao isipokuwa kwa kuwa wao walimkufuru Allaah na Rasuli Wake, na wala hawafiki katika Swalaah isipokuwa wao huwa katika hali ya uvivu, na wala hawatoi isipokuwa wakiwa wamekirihika.


فَلَا تُعْجِبْكَ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُمْ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُعَذِّبَهُم بِهَا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَتَزْهَقَ أَنفُسُهُمْ وَهُمْ كَافِرُونَ﴿٥٥﴾
55. Basi zisikupendezee mali zao, na wala auladi wao. Hakika Allaah Anataka kuwaadhibu kwayo katika uhai wa dunia, na zitokelee mbali nafsi zao na hali wakiwa makafiri.


وَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ إِنَّهُمْ لَمِنكُمْ وَمَا هُم مِّنكُمْ وَلَـٰكِنَّهُمْ قَوْمٌ يَفْرَقُونَ﴿٥٦﴾
56. Na wanaapa kwa Jina la Allaah kwamba wao bila shaka ni miongoni mwenu. Na wala wao si katika nyinyi, lakini wao (wanafiki) ni watu    wanaoogopa mno. 


لَوْ يَجِدُونَ مَلْجَأً أَوْ مَغَارَاتٍ أَوْ مُدَّخَلًا لَّوَلَّوْا إِلَيْهِ وَهُمْ يَجْمَحُونَ﴿٥٧﴾
57. Lau wangelipata mahali pa kukimbilia, au mapango, au mahali pa kuingilia (na kujificha), wangeliyaelekea, nao huku wanakimbilia haraka.


وَمِنْهُم مَّن يَلْمِزُكَ فِي الصَّدَقَاتِ فَإِنْ أُعْطُوا مِنْهَا رَضُوا وَإِن لَّمْ يُعْطَوْا مِنْهَا إِذَا هُمْ يَسْخَطُونَ﴿٥٨﴾
58. Na miongoni mwao wako wanaokufedhehesha kwa ishara, vitendo na lawama katika (ugawaji wa) Swadaqah. Wakipewa humo (chochote) wanaridhika, na wasipopewa humo, tahamaki wao wanaghadhibika.


وَلَوْ أَنَّهُمْ رَضُوا مَا آتَاهُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّـهُ سَيُؤْتِينَا اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ وَرَسُولُهُ إِنَّا إِلَى اللَّـهِ رَاغِبُونَ﴿٥٩﴾
59. Na lau wangeliridhiya yale Aliyowapa Allaah na Rasuli Wake, na wakasema: “Anatutosheleza Allaah, karibuni Allaah Atatupa katika fadhila Zake na Rasuli Wake (pia); hakika sisi kwa Allaah tuna raghba”.  


إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۖ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٦٠﴾
60. Hakika Swadaqah (Zakaah) ni kwa ajili ya mafakiri na masikini na wanaozitumikia, na wanaotiwa nguvu nyoyo zao (katika Uislamu) na kuwakomboa watumwa, na (kuwasaidia) wenye deni na katika njia ya Allaah na msafiri (aliyeharibikiwa). Ni faradhi itokayo kwa Allaah. Na Allaah ni ‘Aliymun-Hakiym (Mjuzi wa yote – Mwenye hikmah wa yote).


وَمِنْهُمُ الَّذِينَ يُؤْذُونَ النَّبِيَّ وَيَقُولُونَ هُوَ أُذُنٌ ۚ قُلْ أُذُنُ خَيْرٍ لَّكُمْ يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَيُؤْمِنُ لِلْمُؤْمِنِينَ وَرَحْمَةٌ لِّلَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ ۚ وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ رَسُولَ اللَّـهِ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٦١﴾
61. Na miongoni mwao (wako) wale wanaomuudhi Nabiy, na wanasema: “Yeye ni (mtegaji) sikio tu”. Sema: “Sikio la kheri kwenu (yeye) anamwamini Allaah na anawaamini Waumini, na ni Rahmah kwa wale walioamini miongoni mwenu. Na wale wanaomuudhi Rasuli wa Allaah watapata adhabu iumizayo.  


يَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَكُمْ لِيُرْضُوكُمْ وَاللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَحَقُّ أَن يُرْضُوهُ إِن كَانُوا مُؤْمِنِينَ﴿٦٢﴾
62. Wanakuapieni kwa Jina la Allaah ili wakuridhisheni, na hali Allaah na Rasuli Wake ana haki zaidi kuwa (wao) wamridhishe, ikiwa walikuwa Waumini.


أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّهُ مَن يُحَادِدِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَأَنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدًا فِيهَا ۚ ذَٰلِكَ الْخِزْيُ الْعَظِيمُ﴿٦٣﴾
63. Je, hawajui kwamba yeyote mwenye kumpinga Allaah na Rasuli Wake kwamba atapata Moto wa Jahannam, ni mwenye kudumu humo. Hiyo ni hizaaya kuu.


يَحْذَرُ الْمُنَافِقُونَ أَن تُنَزَّلَ عَلَيْهِمْ سُورَةٌ تُنَبِّئُهُم بِمَا فِي قُلُوبِهِمْ ۚ قُلِ اسْتَهْزِئُوا إِنَّ اللَّـهَ مُخْرِجٌ مَّا تَحْذَرُونَ﴿٦٤﴾
64. Wanafiki wanatahadhari isije kuteremshwa Suwrah itakayowajulisha yaliyomo nyoyoni mwao. Sema: “Fanyeni istihzai; hakika Allaah Atayatoa yale mnayotahadhari nayo.”


وَلَئِن سَأَلْتَهُمْ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلْعَبُ ۚ قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ﴿٦٥﴾
65. Na ukiwauliza, bila shaka watasema: “Hakika tulikuwa tunaporoja na tunacheza.” Sema:  Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayaat Zake na Rasuli    Wake?”


لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ ۚ إِن نَّعْفُ عَن طَائِفَةٍ مِّنكُمْ نُعَذِّبْ طَائِفَةً بِأَنَّهُمْ كَانُوا مُجْرِمِينَ﴿٦٦﴾
66. Msitoe udhuru. Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu. Tukilisamehe kundi miongoni mwenu, Tutaliadhibu kundi (jingine), kwa kuwa wao walikuwa wahalifu.


الْمُنَافِقُونَ وَالْمُنَافِقَاتُ بَعْضُهُم مِّن بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمُنكَرِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمَعْرُوفِ وَيَقْبِضُونَ أَيْدِيَهُمْ ۚ نَسُوا اللَّـهَ فَنَسِيَهُمْ ۗ إِنَّ الْمُنَافِقِينَ هُمُ الْفَاسِقُونَ﴿٦٧﴾
67. Wanafiki wanaume na wanafiki wanawake, wao kwa wao. Wanaamrisha munkari na wanakataza ma’-ruwf (mema) na wanafumba mikono yao (hawatoi katika njia ya Allaah); wamemsahau Allaah, basi Naye Amewasahau. Hakika wanafiki wao ndio mafasiki.


وَعَدَ اللَّـهُ الْمُنَافِقِينَ وَالْمُنَافِقَاتِ وَالْكُفَّارَ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ هِيَ حَسْبُهُمْ ۚ وَلَعَنَهُمُ اللَّـهُ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّقِيمٌ﴿٦٨﴾
68. Allaah Amewaahidi wanafiki wanaume na wanafiki wanawake na makafiri Moto wa Jahannam, ni wenye kudumu humo; unawatosheleza (kuwaadhibu vilivyo)! Na Allaah Amewalaani, na watapata adhabu ya kudumu.


كَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ كَانُوا أَشَدَّ مِنكُمْ قُوَّةً وَأَكْثَرَ أَمْوَالًا وَأَوْلَادًا فَاسْتَمْتَعُوا بِخَلَاقِهِمْ فَاسْتَمْتَعْتُم بِخَلَاقِكُمْ كَمَا اسْتَمْتَعَ الَّذِينَ مِن قَبْلِكُم بِخَلَاقِهِمْ وَخُضْتُمْ كَالَّذِي خَاضُوا ۚ أُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿٦٩﴾
69. (Makafiri nyinyi ni) Kama wale wa kabla yenu, walikuwa wana nguvu zaidi kuliko nyinyi, na wana mali na auladi zaidi. Basi walistarehe kwa fungu lao (katika anasa za dunia), nanyi mnastarehe kwa fungu lenu, kama walivyostarehe kwa fungu lao wale wa kabla yenu; na mkatumbukia (katika maovu) kama walivyotumbukia katika maovu. Hao zimebatilika ‘amali zao duniani na Aakhirah. Na hao ndio waliokhasirika.


أَلَمْ يَأْتِهِمْ نَبَأُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ وَقَوْمِ إِبْرَاهِيمَ وَأَصْحَابِ مَدْيَنَ وَالْمُؤْتَفِكَاتِ ۚ أَتَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ ۖ فَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴿٧٠﴾
70. Je, haikuwafikia habari ya wale wa kabla yao; kaumu ya Nuwh, na ‘Aad na Thamuwd, na kaumu ya Ibraahiym, na watu ya Madyan, na (watu wa) miji iliyopinduliwa juu chini (watu wa Luwtw)? Rasuli wao waliwafikia kwa hoja bayana. Na Allaah Hakuwa Mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao wenyewe.


وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ اللَّـهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٧١﴾
71. Na Waumini wanaume na Waumini wanawake ni awliyaa (marafiki walinzi) wao kwa wao, wanaamrisha ma-aruwf na wanakataza munkari na wanasimamisha Swalaah na wanatoa Zakaah na wanamtii Allaah na Rasuli Wake. Hao Allaah Atawarehemu. Hakika Allaah ni ‘Aziyzun-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika - Mwenye hikmah wa yote).


وَعَدَ اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ۚ وَرِضْوَانٌ مِّنَ اللَّـهِ أَكْبَرُ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٧٢﴾
72. Allaah Amewaahidi Waumini wanaume na Waumini wanawake Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo na makazi mazuri katika Jannaat za ‘Adn. Na Radhi kutoka kwa Allaah ndio kubwa zaidi. Huko ndiko kufuzu adhimu.


يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ جَاهِدِ الْكُفَّارَ وَالْمُنَافِقِينَ وَاغْلُظْ عَلَيْهِمْ ۚ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿٧٣﴾
73.  Ee Nabiy! Fanya jihaad (kwa kupambana na) makafiri na wanafiki na kuwa mgumu kwao. Na makazi yaoni (Moto wa) Jahannam, na ubaya ulioje mahali pa kuishia.


يَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ مَا قَالُوا وَلَقَدْ قَالُوا كَلِمَةَ الْكُفْرِ وَكَفَرُوا بَعْدَ إِسْلَامِهِمْ وَهَمُّوا بِمَا لَمْ يَنَالُوا ۚ وَمَا نَقَمُوا إِلَّا أَنْ أَغْنَاهُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ مِن فَضْلِهِ ۚ فَإِن يَتُوبُوا يَكُ خَيْرًا لَّهُمْ ۖ وَإِن يَتَوَلَّوْا يُعَذِّبْهُمُ اللَّـهُ عَذَابًا أَلِيمًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَمَا لَهُمْ فِي الْأَرْضِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ﴿٧٤﴾
74. Wanaapa kwa Jina la Allaah (kwamba) hawakusema (neno la kufuru), na hali wamekwishasema neno la kufuru, na wakakufuru baada ya Uislamu wao. Na wakaazimia yale ambayo hawakuweza kuyafikia. Na hawakuchukia isipokuwa kwa kuwa Allaah na Rasuli Wake Amewatajirisha kwa fadhila Zake. Basi wakitubia, itakuwa ni kheri kwao. Na wakikengeuka, Allaah Atawaadhibu adhabu iumizayo duniani na Aakhirah. Na hawatopata katika ardhi mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru.


وَمِنْهُم مَّنْ عَاهَدَ اللَّـهَ لَئِنْ آتَانَا مِن فَضْلِهِ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ الصَّالِحِينَ﴿٧٥﴾
75.  Na miongoni mwao (hao wanafiki) wako waliomuahidi Allaah (kuwa): “Akitupa katika fadhila Zake, bila shaka tutatoa swadaqah, na bila shaka tutakuwa miongoni mwa Swalihina.


فَلَمَّا آتَاهُم مِّن فَضْلِهِ بَخِلُوا بِهِ وَتَوَلَّوا وَّهُم مُّعْرِضُونَ﴿٧٦﴾
76. Alipowapa katika fadhila Zake; walizifanyia ubakhili, na wakakengeuka huku wakipuuza.


فَأَعْقَبَهُمْ نِفَاقًا فِي قُلُوبِهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ يَلْقَوْنَهُ بِمَا أَخْلَفُوا اللَّـهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ﴿٧٧﴾
77. Basi Akawapatilizia unafiki katika nyoyo zao mpaka Siku watakayokutana Naye (Allaah) kwa vile walivyomkhalifu kwao Allaah kwa waliyomuahidi, na kwa yale waliyokuwa wakikadhibisha.  


أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُمْ وَأَنَّ اللَّـهَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ﴿٧٨﴾
78. Je, hawajui kwamba Allaah Anajua siri zao na minong’ono yao; na kwamba Allaah ni ‘Allaamu (Mjuzi) wa ghayb.


الَّذِينَ يَلْمِزُونَ الْمُطَّوِّعِينَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ فِي الصَّدَقَاتِ وَالَّذِينَ لَا يَجِدُونَ إِلَّا جُهْدَهُمْ فَيَسْخَرُونَ مِنْهُمْ ۙ سَخِرَ اللَّـهُ مِنْهُمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٧٩﴾
79. Wale wanaowafedhehesha wenye kujitolea kwa hiari katika kutoa swadaqah miongoni mwa Waumini, na (pia) wale wasiopata (kitu cha kutoa) isipokuwa juhudi zao, wanawafanyia dhihaki, Allaah Analipiza dhihaki zao na watapata adhabu iumizayo.


اسْتَغْفِرْ لَهُمْ أَوْ لَا تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ إِن تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ سَبْعِينَ مَرَّةً فَلَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَهُمْ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴿٨٠﴾
80. Waombee maghfirah (ee, Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), au usiwaombee maghfirah, hata ukiwaombea maghfirah mara sabiini, Allaah Hatowaghufurilia. Hivyo kwa kuwa wao wamemkufuru Allaah na Rasuli Wake. Na Allaah Haongoi watu mafasiki.


فَرِحَ الْمُخَلَّفُونَ بِمَقْعَدِهِمْ خِلَافَ رَسُولِ اللَّـهِ وَكَرِهُوا أَن يُجَاهِدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَقَالُوا لَا تَنفِرُوا فِي الْحَرِّ ۗ قُلْ نَارُ جَهَنَّمَ أَشَدُّ حَرًّا ۚ لَّوْ كَانُوا يَفْقَهُونَ﴿٨١﴾
81. Waliobaki nyuma (kutokwenda vitani) walifurahi kwa kule kukaa kwao (majumbani) baada ya Rasuli wa Allaah (kutoka); na walikirihika kufanya jihaad kwa mali zao na nafsi zao katika njia ya Allaah; na wakasema: “Msitoke kwenda (vitani) katika joto.” Sema: “Moto wa Jahannam ni mkali zaidi lau wangelifahamu”.


فَلْيَضْحَكُوا قَلِيلًا وَلْيَبْكُوا كَثِيرًا جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٨٢﴾
82. Basi na wacheke kidogo (duniani), na watalia sana (Aakhirah); jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.



فَإِن رَّجَعَكَ اللَّـهُ إِلَىٰ طَائِفَةٍ مِّنْهُمْ فَاسْتَأْذَنُوكَ لِلْخُرُوجِ فَقُل لَّن تَخْرُجُوا مَعِيَ أَبَدًا وَلَن تُقَاتِلُوا مَعِيَ عَدُوًّا ۖ إِنَّكُمْ رَضِيتُم بِالْقُعُودِ أَوَّلَ مَرَّةٍ فَاقْعُدُوا مَعَ الْخَالِفِينَ﴿٨٣﴾
83. Basi Allaah Akikurejesha (kutoka vita vya Tabuwk) kwa kundi miongoni mwao na wakakutaka idhini ya kutoka (kwenda vitani vitakavyotokea); basi sema: “Hamtotoka pamoja nami abadani, na wala hamtopigana na maadui pamoja nami. Hakika nyinyi mliridhika kukaa (msiende vitani) mara ya kwanza; basi kaeni pamoja na wanaobakia nyuma.


وَلَا تُصَلِّ عَلَىٰ أَحَدٍ مِّنْهُم مَّاتَ أَبَدًا وَلَا تَقُمْ عَلَىٰ قَبْرِهِ ۖ إِنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَمَاتُوا وَهُمْ فَاسِقُونَ﴿٨٤﴾
84. Na wala usimswalie yeyote abadani miongoni mwao akifa; na wala usisimame kaburini kwake. Hakika wao wamemkufuru Allaah na Rasuli Wake, na wakafa hali wao ni mafasiki. 


وَلَا تُعْجِبْكَ أَمْوَالُهُمْ وَأَوْلَادُهُمْ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُعَذِّبَهُم بِهَا فِي الدُّنْيَا وَتَزْهَقَ أَنفُسُهُمْ وَهُمْ كَافِرُونَ﴿٨٥﴾
85. Na wala isikupendezee mali zao, na auladi wao. Hakika Allaah Anataka kuwaadhibu kwayo duniani, na zitokelee mbali nafsi zao (katika mauti), na huku wao ni makafiri.


وَإِذَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ أَنْ آمِنُوا بِاللَّـهِ وَجَاهِدُوا مَعَ رَسُولِهِ اسْتَأْذَنَكَ أُولُو الطَّوْلِ مِنْهُمْ وَقَالُوا ذَرْنَا نَكُن مَّعَ الْقَاعِدِينَ﴿٨٦﴾
86. Na inapoteremshwa Suwrah (inayosema): “Muaminini Allaah, na fanyeni jihaad pamoja na Rasuli Wake,” wanakuomba idhini wale (wanafiki) wenye utajiri miongoni mwao, na husema: “Tuache (tusiende vitani) tuwe pamoja na wanaokaa.”


رَضُوا بِأَن يَكُونُوا مَعَ الْخَوَالِفِ وَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَفْقَهُونَ﴿٨٧﴾
87. Wameridhika kuwa pamoja na waliokaa nyuma, na zikapigwa chapa nyoyo zao, basi wao hawafahamu.


لَـٰكِنِ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ جَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۚ وَأُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْخَيْرَاتُ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿٨٨﴾
88. Lakini Rasuli na wale walioamini pamoja naye, walifanya jihaad kwa mali zao na nafsi zao. Na hao watapata kheri nyingi. Na hao ndio wenye kufaulu.


أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٨٩﴾
89. Allaah Amewaandalia Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo. Huko ndiko kufuzu adhimu.


وَجَاءَ الْمُعَذِّرُونَ مِنَ الْأَعْرَابِ لِيُؤْذَنَ لَهُمْ وَقَعَدَ الَّذِينَ كَذَبُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ سَيُصِيبُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٩٠﴾
90. Na wakaja wenye nyudhuru katika Mabedui ili waruhusiwe (wasiende vitani), na wakakaa (bila ya kuomba idhini) wale waliomkadhibisha Allaah na Rasuli Wake. Itawasibu wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo.


لَّيْسَ عَلَى الضُّعَفَاءِ وَلَا عَلَى الْمَرْضَىٰ وَلَا عَلَى الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ مَا يُنفِقُونَ حَرَجٌ إِذَا نَصَحُوا لِلَّـهِ وَرَسُولِهِ ۚ مَا عَلَى الْمُحْسِنِينَ مِن سَبِيلٍ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٩١﴾
91. Hapana lawama (kwa kutokwenda vitani) juu ya wale walio dhaifu (wa umbo), na wala (hapana lawama) juu ya walio wagonjwa, na wala (hapana lawama pia) juu ya wale wasiopata cha kutoa (katika jihaad), madamu wakimsafia niyyah Allaah na Rasuli Wake. Hapana njia ya kuwalaumu wafanyao ihsaan. Na Allaah ni Ghafuwrun-Haliym (Mwingi wa kughufuria - Mpole wa kuwavumilia waja).


وَلَا عَلَى الَّذِينَ إِذَا مَا أَتَوْكَ لِتَحْمِلَهُمْ قُلْتَ لَا أَجِدُ مَا أَحْمِلُكُمْ عَلَيْهِ تَوَلَّوا وَّأَعْيُنُهُمْ تَفِيضُ مِنَ الدَّمْعِ حَزَنًا أَلَّا يَجِدُوا مَا يُنفِقُونَ﴿٩٢﴾
92. Na wala (hakuna lawama) juu ya wale ambao wanapokujia ili uwapatie kipando (cha kwendea vitani); Ukasema: “Sina cha kukupandisheni juu yake.” Wamegeuka nyuma (kurudi) na huku macho yao yanamiminika machozi kwa huzuni ya kukosa kupata cha kutoa mchango.


إِنَّمَا السَّبِيلُ عَلَى الَّذِينَ يَسْتَأْذِنُونَكَ وَهُمْ أَغْنِيَاءُ ۚ رَضُوا بِأَن يَكُونُوا مَعَ الْخَوَالِفِ وَطَبَعَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٩٣﴾
93. Hakika sababu ya kulaumu ni juu ya wale wanaokuomba idhini na hali wao ni matajiri. Wameridhia kuwa pamoja na waliobakia nyuma; na Allaah Akapiga chapa juu ya nyoyo zao, basi wao hawajui. 


يَعْتَذِرُونَ إِلَيْكُمْ إِذَا رَجَعْتُمْ إِلَيْهِمْ ۚ قُل لَّا تَعْتَذِرُوا لَن نُّؤْمِنَ لَكُمْ قَدْ نَبَّأَنَا اللَّـهُ مِنْ أَخْبَارِكُمْ ۚ وَسَيَرَى اللَّـهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٩٤﴾
94. (Wanafiki) Watakutoleeni udhuru mtakaporejea kwao. Sema: “Msitoe udhuru, hatutokuaminini! Allaah Amekwishatujulisha kuhusu habari zenu. Na hivi karibuni Allaah Ataona ‘amali zenu na Rasuli Wake (pia ataona). Kisha mtarudishwa kwa ‘Aalimi (Mjuzi) wa ghayb na dhahiri, Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.”


سَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَكُمْ إِذَا انقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ لِتُعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ فَأَعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ إِنَّهُمْ رِجْسٌ ۖ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٩٥﴾
95. Watakuapieni kwa Allaah, mtakaporudi kwao ili muwapuuze. Basi wapuuzeni; hakika wao nirijs (uchafu) na makazi yao ni (Moto wa) Jahannam. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.


يَحْلِفُونَ لَكُمْ لِتَرْضَوْا عَنْهُمْ ۖ فَإِن تَرْضَوْا عَنْهُمْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يَرْضَىٰ عَنِ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ﴿٩٦﴾
96. Watakuapieni ili muwaridhie. Mkiwaridhia, basi hakika Allaah Haridhii watu mafasiki.


الْأَعْرَابُ أَشَدُّ كُفْرًا وَنِفَاقًا وَأَجْدَرُ أَلَّا يَعْلَمُوا حُدُودَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٩٧﴾
97. Mabedui wamezidi zaidi kufuru na unafiki, na wameelekea zaidi kwamba wasijue mipaka ya (shariy’ah) Alizoteremsha Allaah juu ya Rasuli Wake. Na Allaah ni ‘Aliymun-Hakiym (Mjuzi wa yote– Mwenye hikmah wa yote).


وَمِنَ الْأَعْرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغْرَمًا وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ الدَّوَائِرَ ۚ عَلَيْهِمْ دَائِرَةُ السَّوْءِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿٩٨﴾
98. Na katika Mabedui, wako wanaochukulia yale wanayoyatoa kuwa ni gharama (hasara tupu), na wanakungojeleeni migeuko ya misiba. Misiba mibaya itawafika wao. Na Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye kusikia yote – Mjuzi wa yote).


وَمِنَ الْأَعْرَابِ مَن يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ قُرُبَاتٍ عِندَ اللَّـهِ وَصَلَوَاتِ الرَّسُولِ ۚ أَلَا إِنَّهَا قُرْبَةٌ لَّهُمْ ۚ سَيُدْخِلُهُمُ اللَّـهُ فِي رَحْمَتِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٩٩﴾
99. Na katika Mabedui, wako wanaomwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na wanachukulia yale wanayoyatoa kuwa ni njia ya makurubisho (yao) mbele ya Allaah, na kupata du’aa ya Rasuli. Tanabahi! Hakika hayo ni njia ya kikurubisho kwao. Allaah Atawaingiza katika Rahmah Yake. Hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu)


وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١٠٠﴾
100. Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhaajiriyn (wa Makkah), na Answaar (wa Madiynah), na wale waliowafuata kwa ihsaan; Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Na Amewaandalia Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo abadi. Huko ndiko kufuzu adhimu.


وَمِمَّنْ حَوْلَكُم مِّنَ الْأَعْرَابِ مُنَافِقُونَ ۖ وَمِنْ أَهْلِ الْمَدِينَةِ ۖ مَرَدُوا عَلَى النِّفَاقِ لَا تَعْلَمُهُمْ ۖ نَحْنُ نَعْلَمُهُمْ ۚ سَنُعَذِّبُهُم مَّرَّتَيْنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَىٰ عَذَابٍ عَظِيمٍ﴿١٠١﴾
101. Na katika Mabedui wanaokaa pembezoni mwenu (wako) wanafiki. Na katika watu wa Madiynah (pia) walibobea katika unafiki. Huwajui (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Sisi Tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili; kisha watarudishwa katika adhabu kuu.


وَآخَرُونَ اعْتَرَفُوا بِذُنُوبِهِمْ خَلَطُوا عَمَلًا صَالِحًا وَآخَرَ سَيِّئًا عَسَى اللَّـهُ أَن يَتُوبَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٠٢﴾
102. Na wengineo wamekiri madhambi yao; wamechanganya ‘amali njema na nyinginezo ovu; huenda Allaah Apokee tawbah zao. Hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّ صَلَاتَكَ سَكَنٌ لَّهُمْ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿١٠٣﴾
103. Chukua (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika mali zao Swadaqah, uwatwaharishe na uwatakase kwazo na waombee (du’aa na maghfirah). Hakika du’aa yako ni utulivu kwao. Allaah ni Samiy’un-‘Aliym (Mwenye kusikia yote – Mjuzi wa yote).


أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ هُوَ يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَأْخُذُ الصَّدَقَاتِ وَأَنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ﴿١٠٤﴾
104. Je hawajui kwamba Allaah Ndiye Anayepokea tawbah ya waja Wake, na Anapokea Swadaqaat; na kwamba Allaah Ndiye Tawwaabur-Rahiym (Mwingi wa kupokea tawbah – Mwenye kurehemu).


وَقُلِ اعْمَلُوا فَسَيَرَى اللَّـهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ ۖ وَسَتُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿١٠٥﴾
105. Na sema (uwaambie):  Fanyeni (mtakavyo). Allaah Ataona ‘amali zenu na Rasuli Wake, na Waumini (pia wataona). Na mtarudishwa kwa ‘Aalimi (Mjuzi) wa ghayb na dhahiri; kisha Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.


وَآخَرُونَ مُرْجَوْنَ لِأَمْرِ اللَّـهِ إِمَّا يُعَذِّبُهُمْ وَإِمَّا يَتُوبُ عَلَيْهِمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿١٠٦﴾
106. Na wengineo wamengojeshewa kwa Amri ya Allaah. Ama Atawaadhibu au Atawapokelea tawbah zao.Na Allaah ni ‘Aliymun-Hakiym (Mjuzi wa yote – Mwenye hikmah wa yote).


وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مَسْجِدًا ضِرَارًا وَكُفْرًا وَتَفْرِيقًا بَيْنَ الْمُؤْمِنِينَ وَإِرْصَادًا لِّمَنْ حَارَبَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ مِن قَبْلُ ۚ وَلَيَحْلِفُنَّ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا الْحُسْنَىٰ ۖ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ﴿١٠٧﴾
107. Na wale (wanafiki) waliojenga msikiti kwa ajili ya kuleta madhara na kufuru na kufarikisha baina ya Waumini na (kuufanya mahali) pa kuvizia waliompiga vita Allaah na Rasuli Wake (hapo) kabla.  Na bila shaka wanaapa (kwa kusema): “Hatukukusudia ila jambo zuri” Na Allaah Anashuhudia kwamba hakika wao ni waongo. 


لَا تَقُمْ فِيهِ أَبَدًا ۚ لَّمَسْجِدٌ أُسِّسَ عَلَى التَّقْوَىٰ مِنْ أَوَّلِ يَوْمٍ أَحَقُّ أَن تَقُومَ فِيهِ ۚ فِيهِ رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَن يَتَطَهَّرُوا ۚ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُطَّهِّرِينَ﴿١٠٨﴾
108. Usisimame (msikitini) humo abadani.  Bila shaka msikiti ulioasisiwa juu ya taqwa tokea siku ya kwanza unastahiki zaidi usimame humo. Humo mna watu wanaopenda kujitwaharisha. Na Allaah Anapenda wanaojitwaharisha.


أَفَمَنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىٰ تَقْوَىٰ مِنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانٍ خَيْرٌ أَم مَّنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىٰ شَفَا جُرُفٍ هَارٍ فَانْهَارَ بِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿١٠٩﴾
109. Je, yule aliyeasisi jengo lake juu ya taqwa kutokana na Allaah (na kutafuta) Radhi, ni bora au yule aliyeasisi jengo lake juu ya ukingo wa bonde lenye ufa lenye kuburugunyika likaporomoka pamoja naye katika Moto wa Jahannam?  Na Allaah Haongozi watu madhalimu.


لَا يَزَالُ بُنْيَانُهُمُ الَّذِي بَنَوْا رِيبَةً فِي قُلُوبِهِمْ إِلَّا أَن تَقَطَّعَ قُلُوبُهُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿١١٠﴾
110.  Halitoacha (litaendelea) jengo lao hilo walolijenga kuwa ni sababu ya kuwatia shaka katika nyoyo zao mpaka nyoyo zao zikatike katike (wafe); na Allaah ni ‘Aliymun-Hakiym (Mjuzi wa yote– Mwenye hikmah wa yote).


إِنَّ اللَّـهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ ۚ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ ۖ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ ۚ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّـهِ ۚ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١١١﴾
111. Hakika Allaah Amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwamba watapata (badala yake) Jannah. Wanapigana katika njia ya Allaah, wanaua na wanauawa. Hii ni ahadi ya haki Aliyojiwekea (Allaah kuitimiza) katika Tawraat na Injiyl na Qur-aan. Na nani atimizae zaidi ahadi yake kuliko Allaah?  Basi furahieni kwa biashara yenu mliyouziana Naye. Na huko ndiko kufuzu adhimu. 


التَّائِبُونَ الْعَابِدُونَ الْحَامِدُونَ السَّائِحُونَ الرَّاكِعُونَ السَّاجِدُونَ الْآمِرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَالنَّاهُونَ عَنِ الْمُنكَرِ وَالْحَافِظُونَ لِحُدُودِ اللَّـهِ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ﴿١١٢﴾
112. (Waumini hao ni;) At-Taaibuwn (wanaotubia), Al-‘Aabiduwn (wanaofanya ibada), Al-Haamiduwn (wanaomsifu na kumshukuru Allaah), As-Saaihuwn (wanaofunga swiyaam au wanaotoka kwa ajili ya jihaad katika njia ya Allaah), Ar-Raaki’uwn (wanaorukuu), As-Saajiduwn (wanaosujudu), wanaoamrisha ma’-ruwf (mema) na wanaokataza munkari, na wanohifadhi mipaka ya Allaah. Na wabashirie Waumini.


مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ﴿١١٣﴾
113. Haimpasi Nabiy na wale walioamini kuwaombea maghfirah washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa (Moto wa) Al-Jahiym.


وَمَا كَانَ اسْتِغْفَارُ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوْعِدَةٍ وَعَدَهَا إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ عَدُوٌّ لِّلَّـهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ ۚ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَأَوَّاهٌ حَلِيمٌ﴿١١٤﴾
114. Na haikuwa Ibraahiym kumuombea maghfirah baba yake isipokuwa kwa sababu ya ahadi aliyoahidiana naye. Lakini ilipombainikia kwamba yeye (huyo baba yake) ni adui wa Allaah, alijiepusha naye. Hakika Ibraahiym ni mwenye huruma mno na mvumilivu.


وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِلَّ قَوْمًا بَعْدَ إِذْ هَدَاهُمْ حَتَّىٰ يُبَيِّنَ لَهُم مَّا يَتَّقُونَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴿١١٥﴾
115. Na haiwi kwa Allaah Awapotoze watu baada ya kuwa Amewaongoa mpaka Awabainishie ya kujikinga nayo. Hakika Allaah kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi).


إِنَّ اللَّـهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۚ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ﴿١١٦﴾
116. Hakika Allaah Anao ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na Anafisha. Nanyi hamna pasi na Allaah mlinzi wala mnusuraji yeyote.


لَّقَد تَّابَ اللَّـهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ الْعُسْرَةِ مِن بَعْدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٍ مِّنْهُمْ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّهُ بِهِمْ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١١٧﴾
117. Kwa yakini Allaah Amepokea tawbah ya Nabiy na Al-Muhaajiriyn (wa Makkah) na Al-Answaar (wa Madiynah) ambao wamemfuata (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) katika saa ya dhiki (walipokwenda vita vya Tabuwk kupigana na Warumi) baada ya nyoyo za kundi miongoni mwao zilikaribia kuelemea (mbali na haki), kisha (Allaah) Akapokea tawbah yao. Hakika Yeye kwao ni Rauwfur-Rahiym (Mwenye huruma mno - Mwenye kurehemu).


وَعَلَى الثَّلَاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا حَتَّىٰ إِذَا ضَاقَتْ عَلَيْهِمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ وَضَاقَتْ عَلَيْهِمْ أَنفُسُهُمْ وَظَنُّوا أَن لَّا مَلْجَأَ مِنَ اللَّـهِ إِلَّا إِلَيْهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ لِيَتُوبُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ﴿١١٨﴾
118. Na (pia Allaah Akapokea tawbah) ya wale watatu waliobaki nyuma (kutokwenda vita vya Tabuwk; wakajuta mno) mpaka ardhi ikadhikika kwao juu ya kuwa ni pana na zikadhikika nafsi zao, na wakatambua kwamba hakuna pa kumkimbia Allaah isipokuwa (kuelekea) Kwake; kisha (Allaah) Akapokea tawbah yao, ili watubie. Hakika Allaah Yeye Ndiye Tawwaabur-Rahiym (Mwingi wa kupokea tawbah – Mwenye kurehemu).


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ﴿١١٩﴾
119. Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli.


مَا كَانَ لِأَهْلِ الْمَدِينَةِ وَمَنْ حَوْلَهُم مِّنَ الْأَعْرَابِ أَن يَتَخَلَّفُوا عَن رَّسُولِ اللَّـهِ وَلَا يَرْغَبُوا بِأَنفُسِهِمْ عَن نَّفْسِهِ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ لَا يُصِيبُهُمْ ظَمَأٌ وَلَا نَصَبٌ وَلَا مَخْمَصَةٌ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَطَئُونَ مَوْطِئًا يَغِيظُ الْكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنْ عَدُوٍّ نَّيْلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُم بِهِ عَمَلٌ صَالِحٌ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ﴿١٢٠﴾
120. Haikuwapasa watu wa Madiynah na Mabedui walio pembezoni mwao kwamba wabakie nyuma ya Rasuli wa Allaah (kwa kutokwenda vitani pamoja naye), wala (haipasi) wajipendelee nafsi zao kuliko nafsi yake (Rasuli). Hivyo ni kwa kuwa wao haiwasibu kiu wala machofu, wala njaa kali katika njia ya Allaah, na wala hawakanyagi njia inayowaghadhibisha makafiri, na wala hawawasibu maadui msiba wowote ila wanaadikiwa kwayo ‘amali njema. Hakika Allaah Hapotezi ujira wa wafanyao ihsaan.


وَلَا يُنفِقُونَ نَفَقَةً صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً وَلَا يَقْطَعُونَ وَادِيًا إِلَّا كُتِبَ لَهُمْ لِيَجْزِيَهُمُ اللَّـهُ أَحْسَنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٢١﴾
121. Na wala hawatoi mchango wowote mdogo au mkubwa (kwa ajili ya Dini ya Allaah) na wala hawavuki bonde (wakiwa vitani) isipokuwa wameandikiwa ili Allaah Awalipe mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wanayatenda.


وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا كَافَّةً ۚ فَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَائِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ﴿١٢٢﴾
122.  Na haiwapasi Waumini watoke wote pamoja kwenda (kupigana vita vya jihaad). Basi kwanini lisitoke katika kila kundi miongoni mwao, kundi (moja tu) wajifunze (Dini); na ili waonye watu wao watakaporejea kwao ili wapate kutahadhari (maovu waepuke adhabu za Allaah).


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قَاتِلُوا الَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ الْكُفَّارِ وَلْيَجِدُوا فِيكُمْ غِلْظَةً ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ﴿١٢٣﴾
123. Enyi Mlioamini! Piganeni (jihaad) na wale makafiri walio karibu nanyi na waukute kwenu ukali. Na jueni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa.


وَإِذَا مَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ فَمِنْهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمْ زَادَتْهُ هَـٰذِهِ إِيمَانًا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَزَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَهُمْ يَسْتَبْشِرُونَ﴿١٢٤﴾
124. Na inapoteremshwa Suwrah, basi miongoni mwao (wanafiki) wako wanaosema: “Nani kati yenu (Suwrah) hii imemzidishia iymaan?” Ama wale walioamini huwazidishia iymaan nao wanafurahia.


وَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَتْهُمْ رِجْسًا إِلَىٰ رِجْسِهِمْ وَمَاتُوا وَهُمْ كَافِرُونَ﴿١٢٥﴾
125. Na ama wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi, huwazidishia rijs (unafiki, shaka n.k) juu ya rijs yao, na wakafa hali wao ni makafiri.


أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٍ مَّرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُونَ﴿١٢٦﴾
126. Je, hawaoni kwamba wao wanatahiniwa katika kila mwaka mara moja au mara mbili; kisha hawatubii na wala wao hawakumbuki?


وَإِذَا مَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ نَّظَرَ بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ هَلْ يَرَاكُم مِّنْ أَحَدٍ ثُمَّ انصَرَفُوا ۚ صَرَفَ اللَّـهُ قُلُوبَهُم بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ﴿١٢٧﴾
127. Na inapoteremshwa Suwrah (wanafiki) wanatazamana wenyewe kwa wenyewe (wakisema:) “Je, kuna mmoja yeyote anayekuoneni?” Kisha wanageuka kuondokea mbali. Allaah Amewagezua nyoyo zao kwa kuwa wao ni watu wasiofahamu.


لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١٢٨﴾
128. Kwa yakini amekujieni Rasuli anayetokana na nyinyi wenyewe, ni yanamtia mashaka (na huzuni) yanayokutaabisheni, anakujalini (muongoke) mwenye huruma kwa Waumini ni rauwfur-rahiym (mwenye huruma mno - mwenye rehma).


فَإِن تَوَلَّوْا فَقُلْ حَسْبِيَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ ۖ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ﴿١٢٩﴾
129. Na wakikengeuka, basi sema: “Amenitosheleza Allaah; Hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye. Kwake nimetawakali. Naye ni Rabb (Mola) wa ‘Arsh adhimu.


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com