020 - Hadiyth Ya 20: Waumini Ni Kama Jengo Hutiliana Nguvu
عَنْ
أَبِي مُوسَى (رضي الله عنه) قال: قال رَسُولُ الله (صلى الله عليه و آله
وسلم): ((الْمُؤْمِنَ لِلْمُؤْمِنِ كَالْبُنْيَانِ يَشُدُّ بَعْضُهُ
بَعْضاً)) وَشَبَّكَ أَصَابِعَهُ - متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa Abu Muwsa (رضي الله عنه) kwamba Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Muumin kwa Muumin mwenziwe ni kama jengo, baadhi yake hutilia nguvu baadhi nyingine)). Akaviumanisha vidole vyake.[1]
Mafunzo Na Hidaaya:
- Waumini wa kweli ni wenye kuungana katika kila jambo lao.
وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ
Na Waumini wanaume na Waumini wanawake ni marafiki walinzi wao wa kwao[2]
- Waumini ni ndugu, hivyo inawapasa kutilia nguvu umoja wao. [Aal ‘Imraan 3: 200].
- Umoja unatia nguvu kama jengo linavyokuwa imara, na hakuna faida kutengana, kwani jengo halitokuwa na faida pindi linapokosa kushikana. [Asw-Swaff 61: 4].
- Umoja unasababisha mapenzi baina ya Waislamu na kupendeleana kheri za kila aina. [Rejea Hadiyth namba 21, 22, 80].
- Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ni mwalimu bora kabisa kwa kutoa mifano mizuri ya hikma na busara katika kuonyesha au kuelezea jambo. [Al-Ahzaab 33: 21].
- Ni mbinu nzuri ya Da‘wah au ufundishaji kwa Daa‘iyyah au mwalimu kwa kuonyesha kitu kwa vitendo. Na kufanya hivyo kunamfanya msikilizaji kuelewa na kufahamu zaidi.