الحديث الثلاثون
"إن الله تعالى فرض فرائض فلا تضيعوها"
عَنْ أَبيِ
ثَعْلَبَةَ الخُشَنِيِّ جُرْثُومِ بْن نَاشرٍ
رضي الله عنه
عَنْ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ:
(( إنّ اللهَ
تَعَالى فَرَضَ فَرَائِضَ فَلاَ تُضَيّعوهاَ وَحَدَّ حُدُودَاً فَلاتَعْتَدُوهَا
وَحَرّمَ أَشْياءَ فَلاَتَنْتَهِكُوهَا وَسَكَتَ عَنْ أَشْيَاءَ رَحْمَةً لَكُمْ
غَيْرَ نِسْيانٍ فَلا تَبْحَثُوا عَنْهَا ))
حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ
الدَّارَقُطْنِيّ وَغَيْرُهُ
HADITHI YA 30
ALLAAH AMEFARIDHISHA MAMBO YA DINI
TUSIYAPUUZE
Kutoka kwa Abu
Tha'alaba Al-Khushani Jurthuum Ibn Naashib رضي الله عنه naye kapokea kwa Mtume صلى الله عليه وسلم :
Allaah سبحانه وتعالى amefaridhisha mambo ya dini kwa hivyo
usiyapuuze. Vile vile kaweka mipaka usiikiuke. Amekataza
baadhi ya mambo kwa hivyo usifanye. Yale aliyoyanyamazia ni kwa
ajili ya huruma zake kwako wala hakusahau kwa hivyo usiyadadisi.
Imesimuliwa na
Daaraqutni na wengineo . Hadithi Hasan