At-Taghaabun (64)


سُورَةُ  التَّغَابُن
At-Taghaabun (64)

(Imeteremka Madina)

Imeanzia Sura hii kwa kueleza kuwa kila kiliomo katika mbingu na katika ardhi kinamtakasa Mwenyezi Mungu na kisio laiki na utukufu wake, na kwamba Yeye ndiye Mwenye Ufalme na Mwenye sifa njema zote, na kwamba Yeye ni Muweza wa kila kitu. Kisha hayo yakafuatilizwa na kutajwa baadhi ya dalili za utimilivu wa uweza wake na ujuzi wake. Kisha Sura ikatupa macho kuwaangalia makafiri walio kuwa kabla ya hawa, na wakawaasi Mitume wa Mola wao Mlezi, na kwamba wao walionja matokeo maovu ya vitendo vyao. Na hayo yalikuwa hivyo kwa sababu Mitume wao walipo kuwa wakiwajia kwa hoja, waliwakataa na wakawapuuza! Sura tena ikaingia baada ya hayo kuvunja madai ya makafiri kwamba wao ati hawatafufuliwa. Na ikawataka watu wamuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Nuru iliyo teremshwa juu yake. Na ikawahadharisha na Siku ya Mkusanyo, siku kutapo dhihiri kupunjana kwa watu. Kwani wale walio amini na wakatenda mema watapata kufuzu kukubwa, na walio kufuru ndio watakuwa watu wa Motoni, na hayo ndiyo marudio maovu. Na hakika masaibu yatakuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na hakika mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu ndio anauongoa moyo wake.
Sura inawataka watu wamt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Wakipuuza, basi hakika Mtume hana juu yake ila kufikisha Ujumbe. Na inawaambia Waumini kuwa mali yao na watoto wao ni fitna, majaribio. Basi isiwe kuyashughulikia hayo kukawapelekea kuacha waliyo amrishwa. Kisha ikawaamrisha wamche Mwenyezi Mungu kwa kadri wawezavyo. Na Sura ikakhitimisha kwa kuwakhusisha Waumini watoe katika njia za kheri, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushukuru, Mpole, Mjuzi wa yaliyo fichikana na yanayo onekana. Basi atawalipa kwa mali yao wanayo yatumia. Na kwamba Yeye ni Mwenye nguvu asiye shindika, Mwenye hikima, hafanyi upuuzi.

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

يُسَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١﴾

1. Kinamsabbih Allaah Pekee (kila) kilichokuweko katika mbingu na katika ardhi, ufalme ni Wake Pekee na Sifa njema ni Zake Pekee. Naye juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza).

هُوَ الَّذِي خَلَقَكُمْ فَمِنكُمْ كَافِرٌ وَمِنكُم مُّؤْمِنٌ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢﴾

2. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni, basi miongoni mwenu (yuko) kafiri na miongoni mwenu (yuko) Muumini. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona).

خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ ۖ وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ ﴿٣﴾

3. Ameumba mbingu na ardhi kwa haki, na Akakutengenezeni sura, kisha Akafanya nzuri sana sura zenu, na Kwake (Pekee) ndio marejeo ya mwisho.

يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَيَعْلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعْلِنُونَ ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٤﴾

4. Anajua yale (yote) yaliyomo mbinguni na ardhini, na Anayajua yale (yote) mnayofanya siri na mnayoyatangaza. Na Allaah ni ‘Aliym (Mjuzi) kwa yaliyomo vifuani.

أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَبَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَبْلُ فَذَاقُوا وَبَالَ أَمْرِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٥﴾

5. Je, haijakufikieni habari ya wale waliokufuru kabla wakaonja matokeo ya uovu wao, na watapata adhabu iumizayo.

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُ كَانَت تَّأْتِيهِمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَقَالُوا أَبَشَرٌ يَهْدُونَنَا فَكَفَرُوا وَتَوَلَّوا ۚ وَّاسْتَغْنَى اللَّـهُ ۚ وَاللَّـهُ غَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴿٦﴾

6. Hivyo kwa kuwa ilikuwa ikiwafikia Rasuli wao kwa hoja bayana wakasema: “Ah! Mtu ndio atuongoe?” Basi wakakufuru na wakakengeuka; na Allaah Akawa hana haja nao, na Allaah ni Ghaniyyun- Hamiyd (Mkwasi - Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote daima).

زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن لَّن يُبْعَثُوا ۚ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ ۚ وَذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿٧﴾

7. Waliokufuru wamedai kwamba hawatofufuliwa kamwe. Sema: Bali hapana! Naapa kwa Rabb (Mola) wangu, bila shaka mtafufuliwa, kisha mtajulishwa kwa yale (yote) mliyoyatenda, na hayo kwa Allaah ni mepesi.

فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَالنُّورِ الَّذِي أَنزَلْنَا ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٨﴾

8. Basi muaminini Allaah na Rasuli Wake na (ifuateni) Nuru (Qur-aan) Tuliyoiteremsha, na Allaah kwa myatendayo ni Khabiyr (Mjuzi wa vilivyodhahiri na vilivyofichikana).

يَوْمَ يَجْمَعُكُمْ لِيَوْمِ الْجَمْعِ ۖ ذَٰلِكَ يَوْمُ التَّغَابُنِ ۗ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ وَيَعْمَلْ صَالِحًا يُكَفِّرْ عَنْهُ سَيِّئَاتِهِ وَيُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿٩﴾

9. Siku Atakayokukusanyeni kwa ajili ya Siku ya mkusanyiko. Hiyo ndio Siku ya At-Taghaabun (kupata na kukosa; Waumini kupata Jannah, na makafiri kukosa Jannah na kuingia Motoni). Basi yeyote (yule) anayemuamini Allaah na akatenda (‘amali) nzuri (Allaah) Atamfutia maovu yake na Atamuingiza Jannaat zipitazo chini yake mito ni wenye kudumu humo abadi. Hayo ni mafanikio makubwa mno.


وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ خَالِدِينَ فِيهَا ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿١٠﴾

10. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat (na ishara) Zetu hao ndio watu wa Motoni ni wenye kudumu humo, na mahali pabaya mno pa kuishia.

مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ يَهْدِ قَلْبَهُ ۚ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١١﴾

11. Hausibu msiba wowote (ule) isipokuwa kwa idhini ya Allaah. Na yeyote (yule) anayemuamini Allaah, (Allaah) Huuongoa moyo wake. Na Allaah kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi).

وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ ۚ فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَإِنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ ﴿١٢﴾

12. Na mtiini Allaah na mtiini Rasuli na mkikengeuka, basi hakika ni juu ya Rasuli Wetu ni ubalighisho (wa ujumbe) bayana.

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٣﴾

13. Allaah, hakuna ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye. Na kwa Allaah watawakali Waumini.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ مِنْ أَزْوَاجِكُمْ وَأَوْلَادِكُمْ عَدُوًّا لَّكُمْ فَاحْذَرُوهُمْ ۚ وَإِن تَعْفُوا وَتَصْفَحُوا وَتَغْفِرُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤﴾

14. Enyi mlioamini! Hakika miongoni mwa wake zenu na auladi wenu (wamo) maadui kwenu, basi tahadharini nao. Na mkisamehe na mkapuuza na mkayafutilia mbali, basi hakika Allaah ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).

إِنَّمَا أَمْوَالُكُمْ وَأَوْلَادُكُمْ فِتْنَةٌ ۚ وَاللَّـهُ عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿١٥﴾

15. Hakika mali zenu na auladi wenu ni jaribio. Na kwa Allaah kuna ujira mkubwa mno.

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ وَاسْمَعُوا وَأَطِيعُوا وَأَنفِقُوا خَيْرًا لِّأَنفُسِكُمْ ۗ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٦﴾

16. Basi mcheni Allaah muwezavyo, na sikilizeni; na tiini na toeni (kwa ajili ya Allaah) ni kheri kwa (ajili ya) nafsi zenu. Na yeyote (yule) anayeepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.

إِن تُقْرِضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا يُضَاعِفْهُ لَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ شَكُورٌ حَلِيمٌ ﴿١٧﴾

17. Mkimkopesha Allaah karadhi mzuri, Atakuzidishieni maradufu, na Atakughufurieni. Na Allaah ni Shakuwrun-Haliym (Mwenye kupokea shukurani – Mpole wa kuwavumilia waja).


عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾

18. ‘Aalimu (Mjuzi) wa ghayb na dhahiri, Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).



Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com