Hadiyth Ya 5 Mja Wangu Anaadhini Na Anaswali Na Ananiogopa



Hadiyth Ya 5



Mja Wangu Anaadhini Na Anaswali Na Ananiogopa


  
عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: (( يَعْجَبُ رَبُّكَ مِنْ رَاعِي غَنَمٍ فِي رَأْسِ شَظِيَّةِ الْجَبَلِ يُؤَذِّنُ بِالصَّلَاةِ وَيُصَلِّي فَيَقُولُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلّ :َ انْظُرُوا إِلَى عَبْدِي هَذَا يُؤَذِّنُ وَيُقِيمُ الصَّلَاةَ يَخَافُ مِنِّي قَدْ غَفَرْتُ لِعَبْدِي وَأَدْخَلْتُهُ الْجَنَّةَ)) النسائي بسند صحيح

Kutoka kwa 'Uqbah Ibn 'Aamirرضي الله عنه    ambaye alisema: "Nilimsikia Mjumbe wa Allaah صلى الله عليه وسلم akisema: ((Mola wenu Anafurahi kwa mchunga, juu ya kilele cha mlima anapoadhini na akaswali. Allaah عَزَّ وَجَلّ Husema: Angalia huyu ni mja Wangu anaadhini na anaswali; ananiogopa. Nimemsamehe mja wangu na nitamtia peponi)) [An-Nasaaiy ikiwa na isnaad nzuri]