Al-‘Adiyaat (100)


سُورَةُ  الْعَادِيَات
Al-‘Adiyaat (100)

(Imeteremka Makka)

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameapa katika kifungulio cha Sura hii kwa farasi wa Jihadi, kwamba hakika mwanaadamu bila ya shaka ni mwingi wa kuikufuru neema ya Mola wake Mlezi. Na kwamba juu ya hivyo katika Akhera bila ya shaka atakuwa ni shahidi dhidi ya nafsi yake kwa aliyo kuwa nayo. Na kwamba bila ya shaka yeye kwa kuyapenda mali ni bakhili na mwenye choyo juu yake. Na khatimaye ametaja khabari za kufufuliwa, na akazindua kuwa ipo hisabu na malipo.

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

وَالْعَادِيَاتِ ضَبْحًا ﴿١﴾

1. Naapa kwa farasi waendao mbio sana wakipumua.

فَالْمُورِيَاتِ قَدْحًا ﴿٢﴾

2. Na (Naapa kwa) watoa cheche za moto kwa kupiga kwato zao.


فَالْمُغِيرَاتِ صُبْحًا ﴿٣﴾

3. Na (Naapa kwa) washambuliao (nyakati za) asubuhi.

فَأَثَرْنَ بِهِ نَقْعًا ﴿٤﴾

4. Huku wakitimua mavumbi makubwa.

فَوَسَطْنَ بِهِ جَمْعًا ﴿٥﴾

5. Kisha wakapenya katikati (ya maadui) wote.


إِنَّ الْإِنسَانَ لِرَبِّهِ لَكَنُودٌ ﴿٦﴾

6. Hakika insani kwa Rabb (Mola) wake bila shaka ni mkanushaji.

وَإِنَّهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٌ ﴿٧﴾

7. Na hakika yeye juu ya hayo bila shaka ni shahidi.

وَإِنَّهُ لِحُبِّ الْخَيْرِ لَشَدِيدٌ ﴿٨﴾

8. Na hakika kwa kupenda kheri bila shaka ni shadidi.


أَفَلَا يَعْلَمُ إِذَا بُعْثِرَ مَا فِي الْقُبُورِ ﴿٩﴾

9. Je, hajui vitakapofukuliwa vile vilivyomo kaburini?

وَحُصِّلَ مَا فِي الصُّدُورِ ﴿١٠﴾

10. Na yatapodhihirishwa yale yaliyomo vifuani?

إِنَّ رَبَّهُم بِهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّخَبِيرٌ ﴿١١﴾

11. Hakika Rabb (Mola) wao kwao siku hiyo bila shaka ni Khabiyr (Mjuzi wa vilivyodhahiri na vilivyofichikana).





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com