At-Tiyn (95)


سُورَةُ  التِّين
At-Tiyn (95)

(Imeteremka Makka)

Mwenyezi Mungu anaapa katika Sura hii kwa matunda mawili yenye baraka, na pahala pawili pazuri, ya kwamba Yeye hakika amemuumba mtu kwa njia kunjufu kabisa, kwa kumkamilishia akili, na uwezo wa kutaka na kutotaka, na mengineyo katika sifa za ukamilifu. Kisha Aya zikataja kuwa mtu hakusimama kwa mujibu wa alivyo umbiwa, bali akateremka kwa daraja mpaka akawa wa chini kabisa, isipo kuwa walio amini na wakatenda mema kati yao. Hao Mwenyezi Mungu amewakunjulia vipawa.  Kisha Sura imewageukia kuwakemea wanao kadhibisha kufufuliwa baada ya kudhihiri dalili zote za uweza wa Mwenyezi Mungu na khabari za hikima yake.

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ ﴿١﴾

1. Naapa kwa tiyn na zaytuun.

وَطُورِ سِينِينَ ﴿٢﴾

2. Na (Naapa kwa) mlima wa Sinai

وَهَـٰذَا الْبَلَدِ الْأَمِينِ ﴿٣﴾

3. Na (Naapa kwa) mji huu wa amani (Makkah).

لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ ﴿٤﴾

4. Kwa yakini Tumemuumba insani katika umbo zuri kabisa.

ثُمَّ رَدَدْنَاهُ أَسْفَلَ سَافِلِينَ ﴿٥﴾

5. Kisha Tukamrudisha (kuwa) chini kabisa ya wali ochini.

إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَلَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ ﴿٦﴾

6. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mazuri; hao watapata ujira usiokatika.

فَمَا يُكَذِّبُكَ بَعْدُ بِالدِّينِ ﴿٧﴾

7. Basi lipi bado litakalokukadhibisha Malipo?

أَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَحْكَمِ الْحَاكِمِينَ ﴿٨﴾

8. Je, kwani Allaah si Mbora wa wanaohukumu?





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com