Al-An’aam: 6

  الأنْعَام
Al-An’aam: 6

(Imeteremka Makka)


SURA hii ni ya Makka isipo kuwa Aya hizi: 20, 23, 91, 93, 114, 141, 151, 152, na 153. Na Aya zake ni 165. Iliteremka baada ya Sura Al-Hijr. Na Sura hii tukufu imekusanya maana zilizo wekwa mbali mbali kama ifuatavyo:
1.     Imewazindua watu wauzingatie ulimwengu na dalili ziliomo ndani yake zenye kuonyesha Ubora wa aliye uumba, na Utukufu wake na Umoja wake wa pekee, na kuwa Yeye hashirikiani na yeyote, la katika kuumba, wala katika kuabudiwa, wala katika dhati yake.
2.     Na imekusanya visa vya baadhi ya Manabii, na ikaanza kwa kisa cha Ibrahim a.s. kwa kubainisha kuwa alichukua maana ya ibada na Tawhidi kwa kuuchungua ulimwengu, na kufuata yaliyomo ndani yake. Naye alianza kwa kupeleleza nyota, kisha mwezi, kisha jua, na akamalizia kwa kufuata ibada ya Mwenyezi Mungu peke yake.
3.     Na ikapelekea macho yaangalie ajabu za uumbaji na vipi mambo yanavyo kuwa. Ikabainisha vipi kilicho hai kinyevu kinatokana na kisicho kuwa na uhai kikavu;  na vipi mbegu inavyo pasuka na ukachipua mmea.
4.     Na Sura hii imezitaja sifa za wapinzani, na vipi wanavyo shikilia ndoto zao zinazo watenga na Haki, na zinazo wapotosha.
5.     Na ndani ya Sura hii umebainishwa uhalali wa vyakula alivyo halalisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na upotovu wa Washirikina walivyo jiharimishia wenyewe bila ya kutegemea dalili yoyote, na vipi wanavyo mnasibishia kuharimisha huko Mwenyezi Mungu Aliye Takasika.
6.     Na ndani yake yamebainishwa mambo haya, ambayo ndio mukhtasari wa Uislamu na tabia njema za kusifika. Mambo yenyewe ni:- kuharimisha ushirikina, uzinzi, kuuwa mtu, kula mali ya yatima, waajibu wa kutimiza vipimo na mizani, kutimiza uadilifu, kutekeleza ahadi, kuwatendea wema wazazi, na kukataza kuwazika watoto wa kike nao wahai.
 




بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَجَعَلَ الظُّلُمَاتِ وَالنُّورَ ۖ ثُمَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ ﴿١
1. AlhamduliLLaahi (Himidi zote Anastahiki Allaah) Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na Akajaalia viza na Nuru; kisha wale ambao wamekufuru wanamsawazisha Rabb (Mola) wao (na wengine).


هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن طِينٍ ثُمَّ قَضَىٰ أَجَلًا ۖ وَأَجَلٌ مُّسَمًّى عِندَهُ ۖ ثُمَّ أَنتُمْ تَمْتَرُونَ ﴿٢
2. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na udongo kisha Akakidhia muda (wa kuishi duniani mpaka kufariki); na muda maalumu uliokadiriwa (maisha ya al-barzakh mpaka kufufuliwa; ujuzi wake) uko Kwake (Allaah) kisha (juu ya haya) nyinyi mnafanya shaka.

وَهُوَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَفِي الْأَرْضِ ۖ يَعْلَمُ سِرَّكُمْ وَجَهْرَكُمْ وَيَعْلَمُ مَا تَكْسِبُونَ ﴿٣
3.  Naye Ndiye Allaah (Anayestahiki kuabudiwa) katika mbingu na ardhi; Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu; na Anajua yale mnayoyachuma.

وَمَا تَأْتِيهِم مِّنْ آيَةٍ مِّنْ آيَاتِ رَبِّهِمْ إِلَّا كَانُوا عَنْهَا مُعْرِضِينَ ﴿٤
4.  Na haiwafikii Aayah (na ishara, dalili, hoja n.k) yoyote ile katika Aayaat za Rabb (Mola) wao isipokuwa huwa ni wenye kuipuuza.

فَقَدْ كَذَّبُوا بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ ۖ فَسَوْفَ يَأْتِيهِمْ أَنبَاءُ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٥
5. Kwa yakini wameikadhibisha haki ilipowajia; basi zitawafikia habari za yale waliyokuwa kwayo wakiyafanyia istihzai.

أَلَمْ يَرَوْا كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّن قَرْنٍ مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ مَا لَمْ نُمَكِّن لَّكُمْ وَأَرْسَلْنَا السَّمَاءَ عَلَيْهِم مِّدْرَارًا وَجَعَلْنَا الْأَنْهَارَ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمْ فَأَهْلَكْنَاهُم بِذُنُوبِهِمْ وَأَنشَأْنَا مِن بَعْدِهِمْ قَرْنًا آخَرِينَ ﴿٦
6.  Je, hawaoni ni karne ngapi Tumeziangamiza kabla yao? Tuliwamakinisha katika ardhi yale ambayo Hatujapata kuwamakinisha (nayo) nyinyi; na Tukawapelekea mvua iendeleayo; na Tukajaalia mito ipitayo chini yao. Tukawaangamiza kwa dhambi zao na Tukaanzisha baada yao karne nyingine.

وَلَوْ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ كِتَابًا فِي قِرْطَاسٍ فَلَمَسُوهُ بِأَيْدِيهِمْ لَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿٧
7. Na lau Tungelikuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu katika karatasi, kisha wakakigusa kwa mikono yao; bila shaka wangelisema wale waliokufuru hii si chochote isipokuwa ni sihiri bayana.

وَقَالُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ مَلَكٌ ۖ وَلَوْ أَنزَلْنَا مَلَكًا لَّقُضِيَ الْأَمْرُ ثُمَّ لَا يُنظَرُونَ ﴿٨
8. Na wakasema: “Mbona hakuteremshiwa Malaika?” Na lau Tungeliteremsha Malaika; basi ingepitishwa amri (ya kuwaangamiza), kisha wasingelipewa muhula (wa kuakhirishwa adhabu).

وَلَوْ جَعَلْنَاهُ مَلَكًا لَّجَعَلْنَاهُ رَجُلًا وَلَلَبَسْنَا عَلَيْهِم مَّا يَلْبِسُونَ ﴿٩
9. Na lau Tungelimfanya Malaika, bila shaka Tungelimfanya (afanane kama) mtu na (hivo basi) Tungeliwatatanishia yale wanayojitatanisha.


وَلَقَدِ اسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَحَاقَ بِالَّذِينَ سَخِرُوا مِنْهُم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿١٠
10. Na kwa yakini walifanyiwa istihzai Rasuli (wengi) kabla yako, lakini (mwishowe) wale waliofanya kejeli, yaliwazunguka yaleyale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.

قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ ثُمَّ انظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ ﴿١١
11. Sema: “Nendeni katika ardhi, kisha mtazame vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha.”

قُل لِّمَن مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ قُل لِّلَّـهِ ۚ كَتَبَ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۚ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٢
12.  Sema: “Ni vya nani vilivyomo mbinguni na ardhini?” Sema: “Ni vya Allaah (Pekee).” Amejiwajibisha Mwenyewe Rahmah. Bila shaka Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah, (Siku hiyo) haina shaka ndani yake; wale ambao wamekhasiri nafsi zao wao hawaamini.

وَلَهُ مَا سَكَنَ فِي اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٣
13. Na ni Vyake Pekee (Allaah) vyote vinavyotulia katika usiku na mchana. Naye ni As-Samiy’ul-‘Aliym (Mwenye kusikia yote – Mjuzi wa yote).

قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَتَّخِذُ وَلِيًّا فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ يُطْعِمُ وَلَا يُطْعَمُ ۗ قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ أَوَّلَ مَنْ أَسْلَمَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٤
14. Sema: “Je, nimfanye asiyekuwa Allaah ndio mlinzi na msaidizi?  Allaah; (Ambaye) Muanzilishi wa mbingu na ardhi; Naye Ndiye Anayelisha na wala halishwi?” Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu, na (nimeamrishwa pia) wala usijekuwa miongoni mwa washirikina”.

قُلْ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٥
15. Sema: “Hakika mimi nakhofu adhabu ya Siku kubwa mno (hiyo) ikiwa nitamuasi Rabb (Mola) wangu.”

مَّن يُصْرَفْ عَنْهُ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمَهُ ۚ وَذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْمُبِينُ ﴿١٦
16. Atakayeepushwa nayo (adhabu) Siku hiyo; basi kwa yakini (Allaah) Amemrehemu. Na huko ndiko kufuzu bayana.

وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يَمْسَسْكَ بِخَيْرٍ فَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٧
17. Na Allaah Akikugusisha dhara, basi hakuna wa kuiondosha isipokuwa Yeye; na Akikugusisha kheri, basi Yeye juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza).

وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿١٨
18. Naye ni Al-Qaahir (Mwenye kudhibiti na kudhalilisha, Mshindi) juu ya waja Wake; Naye ni Al-Hakiymul-Khabiyr (Mwenye hikmah wa yote - Mjuzi wa yaliyodhahiri na yaliyofichikana).


قُلْ أَيُّ شَيْءٍ أَكْبَرُ شَهَادَةً ۖ قُلِ اللَّـهُ ۖ شَهِيدٌ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۚ وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ ۚ أَئِنَّكُمْ لَتَشْهَدُونَ أَنَّ مَعَ اللَّـهِ آلِهَةً أُخْرَىٰ ۚ قُل لَّا أَشْهَدُ ۚ قُلْ إِنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ وَإِنَّنِي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ ﴿١٩
19. Sema (uwaulize): “Kitu gani ushahidi wake ndio mkubwa zaidi?” Sema (ujibu): “Allaah; ni Shahiyd (Mwenye kushuhudia yote) baina yangu na baina yenu. Na nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia. Je, hivi nyinyi hakika mnashuhudia kwamba wako waabudiwa wengine pamoja na Allaah?”  Sema: “Mimi sishuhudii (pamoja nanyi).” Sema: “Hakika Yeye ni Ilaah (Muabudiwa wa haki) Mmoja (Pekee!). Na kwamba hakika mimi sina hatia na hao mnaowashirikisha (Naye).”

الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمُ ۘ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٢٠
20. Wale Tulioewapa Kitabu wanatambua (Uislamu na Tawhiyd na Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kama wanavyotambua watoto wao. Wale waliokhasirika nafsi zao (Aakhirah) hawaamini.

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۗ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ ﴿٢١
21. Na nani mdhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia Allaah uongo au anayekadhibisha Aayaat (na ishara, dalili) Zake? Hakika madhalimu hawatofaulu.

وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا أَيْنَ شُرَكَاؤُكُمُ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٢٢
22. Na (taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Siku Tutakayowakusanya wote pamoja, kisha Tutawaambia wale walioshirikisha: “Wako wapi washirika wenu ambao mlikuwa mnadai (kuwa hao ni miungu)?

ثُمَّ لَمْ تَكُن فِتْنَتُهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا وَاللَّـهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا مُشْرِكِينَ ﴿٢٣
23. Kisha haitokuwa fitnah yao (udhuru) isipokuwa kusema: “Wa-Allaahi Rabb (Mola) wetu hatukuwa washirikina.”

انظُرْ كَيْفَ كَذَبُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ ۚ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٢٤
24. Tazama namna walivyokadhibisha juu ya nafsi zao; na yamewapotea yale waliyokuwa wakiyatunga.

وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ ۖ وَجَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا ۚ وَإِن يَرَوْا كُلَّ آيَةٍ لَّا يُؤْمِنُوا بِهَا ۚ حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوكَ يُجَادِلُونَكَ يَقُولُ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿٢٥
25. Na miongoni mwao (wako) wanaotega sikio kukusikiliza. Na Tumejaalia juu ya nyoyo zao vifuniko wasiyafahamu; na katika masikio yao uziwi. Na wanapoona kila Aayah (ishara, dalili n.k) hawaiamini; hata wanapokujia kukubishia husema wale waliokufuru: “Hizi si chochote ila ni hekaya za watu wa kale.”

وَهُمْ يَنْهَوْنَ عَنْهُ وَيَنْأَوْنَ عَنْهُ ۖ وَإِن يُهْلِكُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٢٦
26. Nao wanazuia (wengine) mbali naye; (wasimfuate Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) nao (wenyewe) wanajiweka mbali naye. Nao hawaangamizi isipokuwa nafsi zao (tu) na hali hawahisi

وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ وُقِفُوا عَلَى النَّارِ فَقَالُوا يَا لَيْتَنَا نُرَدُّ وَلَا نُكَذِّبَ بِآيَاتِ رَبِّنَا وَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢٧
27. Na lau ungeliona watakaposimamishwa kwenye Moto; kisha wakasema: “Laiti tungelirudishwa (duniani) na wala hatutakadhibisha Aayaat za Rabb (Mola) wetu, na tutakuwa miongoni mwa wanaoamini.”


بَلْ بَدَا لَهُم مَّا كَانُوا يُخْفُونَ مِن قَبْلُ ۖ وَلَوْ رُدُّوا لَعَادُوا لِمَا نُهُوا عَنْهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿٢٨
28. Bali yamewadhihirikia yale waliyokuwa wakiyaficha kabla. Na lau wangelirudishwa; kwa yakini wangeyarudia yale waliyokatazwa; na hakika wao ni waongo.

وَقَالُوا إِنْ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ ﴿٢٩
29. Na walisema: “Haya si chochote isipokuwa ni uhai wetu wa dunia tu; na wala sisi hatutofufuliwa.”

وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ وُقِفُوا عَلَىٰ رَبِّهِمْ ۚ قَالَ أَلَيْسَ هَـٰذَا بِالْحَقِّ ۚ قَالُوا بَلَىٰ وَرَبِّنَا ۚ قَالَ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿٣٠
30. Na lau ungeliona watakaposimamishwa mbele ya Rabb (Mola) wao. Atasema (Allaah): “Je, haya si ya kweli?” Watasema: “Ndio, tunaapa kwa Rabb wetu”. Atasema (Allaah): “Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkikufuru”.

قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِلِقَاءِ اللَّـهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءَتْهُمُ السَّاعَةُ بَغْتَةً قَالُوا يَا حَسْرَتَنَا عَلَىٰ مَا فَرَّطْنَا فِيهَا وَهُمْ يَحْمِلُونَ أَوْزَارَهُمْ عَلَىٰ ظُهُورِهِمْ ۚ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ ﴿٣١
31. Kwa yakini wamekhasirika wale waliokadhibisha kukutana na Allaah; hata itakapowajia Saa (ya Qiyaamah) kwa ghafla; watasema: “Ee majuto (makubwa mno) yetu kwa yale tuliyokusuru humo”, na ilhali wao wanabeba mizigo yao (ya dhambi) migongoni mwao. Tanabahi!  Uovu ulioje wanayobeba!

وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَعِبٌ وَلَهْوٌ ۖ وَلَلدَّارُ الْآخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٣٢
32. Na uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni mchezo na pumbao. Na bila shaka nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi kwa wenye taqwa. Je, basi hamtii akilini?

قَدْ نَعْلَمُ إِنَّهُ لَيَحْزُنُكَ الَّذِي يَقُولُونَ ۖ فَإِنَّهُمْ لَا يُكَذِّبُونَكَ وَلَـٰكِنَّ الظَّالِمِينَ بِآيَاتِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ ﴿٣٣
33. Kwa yakini Tunajua (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba yanakuhuzunisha yale wanayoyasema. Basi hakika wao hawakukadhibishi wewe lakini madhalimu wanakanusha Aayaat (na ishara, dalili) za Allaah.

وَلَقَدْ كُذِّبَتْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ فَصَبَرُوا عَلَىٰ مَا كُذِّبُوا وَأُوذُوا حَتَّىٰ أَتَاهُمْ نَصْرُنَا ۚ وَلَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِ اللَّـهِ ۚ وَلَقَدْ جَاءَكَ مِن نَّبَإِ الْمُرْسَلِينَ ﴿٣٤
34. Na kwa yakini walikadhibishwa Rasuli kabla yako, wakasubiri juu ya yale waliyokadhibishwa; na wakaudhiwa hata ilipowafikia nusura Yetu. Na hakuna abadilishaye maneno ya Allaah. Kwa yakini imekujia habari za Rasuli (waliopita).

وَإِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكَ إِعْرَاضُهُمْ فَإِنِ اسْتَطَعْتَ أَن تَبْتَغِيَ نَفَقًا فِي الْأَرْضِ أَوْ سُلَّمًا فِي السَّمَاءِ فَتَأْتِيَهُم بِآيَةٍ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَمَعَهُمْ عَلَى الْهُدَىٰ ۚ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْجَاهِلِينَ ﴿٣٥
35. Na kama imekuwa kukengeuka kwao ni makubwa kwako, basi ukiweza kutafuta upenyo chini kwa chini katika ardhi au ngazi ya (kwendea) mbinguni ili uwaletee Aayah (muujiza, ishara, dalili). Na kama Angetaka Allaah Angeliwakusanya katika uongofu. Basi usiwe miongoni mwa majahili.

إِنَّمَا يَسْتَجِيبُ الَّذِينَ يَسْمَعُونَ ۘ وَالْمَوْتَىٰ يَبْعَثُهُمُ اللَّـهُ ثُمَّ إِلَيْهِ يُرْجَعُونَ ﴿٣٦
36. Hakika wanaitikia wale wanaosikia (kwa moyo mkunjufu). Ama waliokufa (nyoyo zao) Allaah Atawafufua, kisha Kwake watarejeshwa.

وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِّن رَّبِّهِ ۚ قُلْ إِنَّ اللَّـهَ قَادِرٌ عَلَىٰ أَن يُنَزِّلَ آيَةً وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٧
37.  Na walisema: “Kwa nini hakuteremshiwa Aayah (muujiza, ishara n.k) kutoka kwa Rabb (Mola) wake?” Sema: “Hakika Allaah ni Qaadir (Muweza) wa kuteremsha Aayah lakini wengi wao hawajui.”

وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا طَائِرٍ يَطِيرُ بِجَنَاحَيْهِ إِلَّا أُمَمٌ أَمْثَالُكُم ۚ مَّا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِن شَيْءٍ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِمْ يُحْشَرُونَ ﴿٣٨
38. Na hakuna kiumbe chochote kinachotembea katika ardhi na wala ndege anayeruka kwa mbawa zake mbili, isipokuwa ni umati mfano wenu. Hatukusuru katika Kitabu (Lawhum-Mahfudhw) kitu chochote. Kisha kwa Rabb (Mola) wao Pekee watakusanywa.

وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا صُمٌّ وَبُكْمٌ فِي الظُّلُمَاتِ ۗ مَن يَشَإِ اللَّـهُ يُضْلِلْـهُ وَمَن يَشَأْ يَجْعَلْهُ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٣٩
39. Na wale waliokadhibisha Aayaat (na ishara, dalili) Zetu ni viziwi na mabubu katika viza. Yeyote Allaah Amtakaye Humpotoa na yeyote Allaah Amtakaye Humweka juu ya njia iliyonyooka.

قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّـهِ أَوْ أَتَتْكُمُ السَّاعَةُ أَغَيْرَ اللَّـهِ تَدْعُونَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤٠
40. Sema: “Je mnaonaje ikikufikieni adhabu ya Allaah au ikakufikieni Saa (ya Qiyaamah); je, mtamwomba ghairi ya Allaah (akuepusheni) mkiwa ni wakweli?”

بَلْ إِيَّاهُ تَدْعُونَ فَيَكْشِفُ مَا تَدْعُونَ إِلَيْهِ إِن شَاءَ وَتَنسَوْنَ مَا تُشْرِكُونَ ﴿٤١
41. Bali Yeye Pekee Ndiye mtayemwomba, kisha Atakuondoleeni yale mliyomwomba Akitaka; na mtasahau mnayoyashirikisha (pamoja Naye).

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَأَخَذْنَاهُم بِالْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَتَضَرَّعُونَ ﴿٤٢
42. Na kwa yakini Tulipeleka (Rasuli) kwa umati (zilizokuwa) kabla yako; Tukawatia katika mashaka (ufukara, dhiki ya maisha) na madhara (magonjwa, misiba n.k) ili wapate kunyenyekea.

 فَلَوْلَا إِذْ جَاءَهُم بَأْسُنَا تَضَرَّعُوا وَلَـٰكِن قَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٤٣
43. Basi kwa nini ilipowafikia adhabu Yetu wasinyenyekee? Lakini nyoyo zao zimekuwa ngumu na shaytwaan akawapambia yale waliyokuwa wakitenda.

فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ أَبْوَابَ كُلِّ شَيْءٍ حَتَّىٰ إِذَا فَرِحُوا بِمَا أُوتُوا أَخَذْنَاهُم بَغْتَةً فَإِذَا هُم مُّبْلِسُونَ ﴿٤٤
44. Waliposahau yale waliyokumbushwa nayo; Tuliwafungulia milango ya kila kitu (walichotaka), mpaka walipofurahia kwa yale waliyopewa; Tukawachukua ghafla (kawaadhibu), basi mara wao wakawa wenye kukata tamaa.

فَقُطِعَ دَابِرُ الْقَوْمِ الَّذِينَ ظَلَمُوا ۚ وَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٤٥
45. Basi ikakatwa mizizi ya watu waliodhulumu; na AlhamduliLLaahi (Himidi zote Anastahiki Allaah) Rabb (Mola) wa walimwengu.

قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَخَذَ اللَّـهُ سَمْعَكُمْ وَأَبْصَارَكُمْ وَخَتَمَ عَلَىٰ قُلُوبِكُم مَّنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ يَأْتِيكُم بِهِ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ ثُمَّ هُمْ يَصْدِفُونَ ﴿٤٦
46. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) “Mnaonaje ikiwa Allaah Atakuondoleeni kusikia kwenu na kuona kwenu na Akapiga mhuri juu ya nyoyo zenu (zisiinge kheri yoyote); je, ni ilaahu (muabudiwa wa haki) gani ghairi ya Allaah Atakuleteeni tena (Aliyoyachukua kwenu Allaah)?” Tazama namna Tunavyosarifu Aayaat (na ishara, hoja) kisha wao wanakengeuka.

قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّـهِ بَغْتَةً أَوْ جَهْرَةً هَلْ يُهْلَكُ إِلَّا الْقَوْمُ الظَّالِمُونَ ﴿٤٧
47. Sema: “Mnaonaje ikikufikieni adhabu ya Allaah ghafla au kwa dhahiri; kwani (nani) huangamizwa isipokuwa watu madhalimu?”

وَمَا نُرْسِلُ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ ۖ فَمَنْ آمَنَ وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٤٨
48. Na Hatupeleki Rasuli isipokuwa ni wabashiriaji na waonyaji. Basi yeyote atakayeamini na kutengenea; haitakuwa khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.

وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا يَمَسُّهُمُ الْعَذَابُ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿٤٩
49. Na wale waliokadhibisha Aayaat (na hoja, ishara) Zetu itawagusa adhabu kwa yale waliyokuwa wakifanya ufasiki.

قُل لَّا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّـهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ لَكُمْ إِنِّي مَلَكٌ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ ۚ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ ۚ أَفَلَا تَتَفَكَّرُونَ ﴿٥٠
50. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Sikuambieni kuwa mimi nina hazina ya Allaah; na wala (sikuambieni) kwamba najua (mambo ya) ghayb; na wala sikuambieni kuwa mimi ni Malaika. Sifuati ila yale nilofunuliwa Wahy”. Sema: “Je, analingana sawasawa kipofu na mwenye kuona?  Basi hamtafakari?”

وَأَنذِرْ بِهِ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحْشَرُوا إِلَىٰ رَبِّهِمْ ۙ لَيْسَ لَهُم مِّن دُونِهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿٥١
51. Na waonye kwayo (Qur-aan) wale wanaokhofu ya kwamba watakusanywa kwa Rabb (Mola) wao; hawana badala Yake mlinzi wala mwombezi - ili wapate kuwa na taqwa.

وَلَا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ مَا عَلَيْكَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَمَا مِنْ حِسَابِكَ عَلَيْهِم مِّن شَيْءٍ فَتَطْرُدَهُمْ فَتَكُونَ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٢
52. Na wala usiwafukuze wale wanaomwomba Rabb (Mola) wao asubuhi na jioni wanataka Wajihi Wake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, na wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, hata uwafukuze, (kwani ukiwafukuza) utakuja kuwa miongoni mwa madhalimu.

وَكَذَٰلِكَ فَتَنَّا بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لِّيَقُولُوا أَهَـٰؤُلَاءِ مَنَّ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّن بَيْنِنَا ۗ أَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَعْلَمَ بِالشَّاكِرِينَ ﴿٥٣
53. Na hivyo ndivyo Tulivyowafanyia mtihani baadhi yao kwa baadhi ili waseme: “Je, hawa ndio wale Aliowafadhilisha Allaah baina yetu?” Je, kwani Allaah Hajui zaidi wanaoshukuru?”

وَإِذَا جَاءَكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِنَا فَقُلْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ ۖ كَتَبَ رَبُّكُمْ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۖ أَنَّهُ مَنْ عَمِلَ مِنكُمْ سُوءًا بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابَ مِن بَعْدِهِ وَأَصْلَحَ فَأَنَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٥٤
54. Na wanapokujia wale wanaoamini Aayaat (na ishara, hoja) Zetu basi sema: “Salaamun ‘alaykum (amani iwe juu yenu). Rabb (Mola) wenu Amejiwajibisha Mwenyewe Rahmah; kwamba yeyote miongoni mwenu atayetenda ovu kwa ujahili, kisha akatubia baada yake na akatengenea, basi hakika Yeye (Allaah) ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).

وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ وَلِتَسْتَبِينَ سَبِيلُ الْمُجْرِمِينَ ﴿٥٥
55. Na hivyo ndivyo Tunavyofasili Aayaat (hoja, ishara n.k) na ili idhihirike njia ya wahalifu.

قُلْ إِنِّي نُهِيتُ أَنْ أَعْبُدَ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ ۚ قُل لَّا أَتَّبِعُ أَهْوَاءَكُمْ ۙ قَدْ ضَلَلْتُ إِذًا وَمَا أَنَا مِنَ الْمُهْتَدِينَ ﴿٥٦
56. Sema: “Hakika mimi nimekatazwa kuabudu wale mnaowaomba asiyekuwa Allaah.” Sema: “Sifuati hawaa zenu (kwani nikifuata,) kwa yakini nitakuwa nimepotoka, hapo nami sitokuwa miongoni mwa walioongoka.”

قُلْ إِنِّي عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَكَذَّبْتُم بِهِ ۚ مَا عِندِي مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ ۚ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ ۖ يَقُصُّ الْحَقَّ ۖ وَهُوَ خَيْرُ الْفَاصِلِينَ ﴿٥٧
57. Sema: “Hakika mimi niko juu ya hoja bayana kutoka kwa Rabb (Mola) wangu nanyi mumeikadhibisha. Sina yale mnayoyahimiza. Hakuna hukumu isipokuwa ya Allaah Pekee. Anahadithia ya kweli; Naye ni Mbora wa wenye kuamua hukumu”.

قُل لَّوْ أَنَّ عِندِي مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ لَقُضِيَ الْأَمْرُ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِالظَّالِمِينَ ﴿٥٨
58. Sema: “Lau ningelikuwa ninayo yale mnayoyaharakiza, basi bila shaka ingelikidhiwa jambo baina yangu na baina yenu. Na Allaah Anawajua zaidi madhalimu.”

وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٥٩
59. Na Kwake (Allaah) Pekee zipo funguo za ghayb; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Anajua yale yote yaliyomo barani na baharini. Na halianguki jani lolote ila Hulijua, na wala punje katika viza vya ardhi, na wala kilichorutubika na wala  kikavu isipokuwa (kimeandikwa) katika Kitabu kinachobainisha (Lawhum-Mahfuwdhw).

وَهُوَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُم بِاللَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُم بِالنَّهَارِ ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَىٰ أَجَلٌ مُّسَمًّى ۖ ثُمَّ إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ ثُمَّ يُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٦٠
60. Naye Ndiye Anayekufisheni usiku (mnapolala) na Anajua yale yote mnayoyafanya mchana, kisha Anakufufueni humo ili utimizwe muda maalumu uliokadiriwa. Kisha Kwake Pekee ni marejeo yenu, kisha Atakujulisheni kuhusu yale yote mliyokuwa mkiyatenda.

وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۖ وَيُرْسِلُ عَلَيْكُمْ حَفَظَةً حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ تَوَفَّتْهُ رُسُلُنَا وَهُمْ لَا يُفَرِّطُونَ ﴿٦١
61. Naye ni Al-Qaahir (Mwenye kudhibiti na kudhalilisha, Mshindi) juu ya waja Wake, na Anakutumieni Hafadhwah (Malaika wanaohifadhi) hata yanapomfikia mmoja wenu mauti, Wajumbe Wetu humfisha, nao hawafanyi taksiri.

ثُمَّ رُدُّوا إِلَى اللَّـهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ ۚ أَلَا لَهُ الْحُكْمُ وَهُوَ أَسْرَعُ الْحَاسِبِينَ ﴿٦٢
62. Kisha hurudishwa kwa Allaah Mawalaa (Mola) wao wa haki. Tanabahi! Hukumu ni Yake Pekee; Naye ni Mwepesi zaidi kuliko wote wanaohisabu.

قُلْ مَن يُنَجِّيكُم مِّن ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ تَدْعُونَهُ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً لَّئِنْ أَنجَانَا مِنْ هَـٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ ﴿٦٣
63. Sema: “Nani Anakuokoeni kutoka viza vya bara na bahari? (Pale) mnapomuomba kwa kunyenyekea na kwa siri” (Mnamuomba kwa kusema): “Akituokoa kutokana na (janga) hili; bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye kushukuru.”

قُلِ اللَّـهُ يُنَجِّيكُم مِّنْهَا وَمِن كُلِّ كَرْبٍ ثُمَّ أَنتُمْ تُشْرِكُونَ ﴿٦٤
64. Sema: “Allaah Anakuokoeni katika hayo na katika kila janga; kisha nyinyi mnamshirikisha.

قُلْ هُوَ الْقَادِرُ عَلَىٰ أَن يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عَذَابًا مِّن فَوْقِكُمْ أَوْ مِن تَحْتِ أَرْجُلِكُمْ أَوْ يَلْبِسَكُمْ شِيَعًا وَيُذِيقَ بَعْضَكُم بَأْسَ بَعْضٍ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ لَعَلَّهُمْ يَفْقَهُونَ ﴿٦٥
65. Sema: “Yeye ni Al-Qaadir (Muweza) wa kukuleteeni adhabu kutoka juu yenu, au kutoka chini ya miguu yenu, au Akutatanisheni mfarikiane kuwa makundi na Akuonjesheni baadhi yenu (vurugu la) nguvu za wengineo. Tazama namna Tunavyosarifu Aayaat (hoja, ishara n.k) wapate kufahamu.”

وَكَذَّبَ بِهِ قَوْمُكَ وَهُوَ الْحَقُّ ۚ قُل لَّسْتُ عَلَيْكُم بِوَكِيلٍ ﴿٦٦
66. Na wakaikadhibisha (Qur-aan) watu wako na hali ni haki. Sema: “Mimi si mwakilishi juu yenu.”

لِّكُلِّ نَبَإٍ مُّسْتَقَرٌّ ۚ وَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٦٧
67. Kwa kila habari ina wakati (wake) maalumu, na mtakuja kujua.

وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٦٨
68. Na unapowaona wale wanaoshughulika kupiga porojo katika (kukadhibisha) Aayaat Zetu; basi jitenge nao mpaka watumbukie kwenye hadiyth (mazungumzo) mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka, usikae pamoja na watu madhalimu.

وَمَا عَلَى الَّذِينَ يَتَّقُونَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَلَـٰكِن ذِكْرَىٰ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿٦٩
69. Wala si juu wale wenye taqwa, hisabu yao (hao makafiri) kwa lolote, lakini ni ukumbusho huenda wapate kuwa na taqwa.


وَذَرِ الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَهُمْ لَعِبًا وَلَهْوًا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۚ وَذَكِّرْ بِهِ أَن تُبْسَلَ نَفْسٌ بِمَا كَسَبَتْ لَيْسَ لَهَا مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ وَإِن تَعْدِلْ كُلَّ عَدْلٍ لَّا يُؤْخَذْ مِنْهَا ۗ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ أُبْسِلُوا بِمَا كَسَبُوا ۖ لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ ﴿٧٠
70. Na waachilie mbali wale walioichukua Dini yao mchezo na pumbao, na ukawaghuri uhai wa dunia, basi wakumbushe kwayo (Qur-aan watahadhari) isije kila nafsi ikaangamizwa kwa yale iliyoyachuma. Nayo haina pasi na Allaah mlinzi wala mwombezi. Na hata ikitoa fidia ya kila aina haitopokelewa. Hao ndio wale walioangamizwa kwa yale waliyoyachuma; watapata kinywaji cha maji ya moto yachemkayo na adhabu iumizayo kwa yale waliyokuwa wakiyakufuru.

قُلْ أَنَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُنَا وَلَا يَضُرُّنَا وَنُرَدُّ عَلَىٰ أَعْقَابِنَا بَعْدَ إِذْ هَدَانَا اللَّـهُ كَالَّذِي اسْتَهْوَتْهُ الشَّيَاطِينُ فِي الْأَرْضِ حَيْرَانَ لَهُ أَصْحَابٌ يَدْعُونَهُ إِلَى الْهُدَى ائْتِنَا ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّـهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۖ وَأُمِرْنَا لِنُسْلِمَ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٧١
71. Sema: “Je, tuombe asiyekuwa Allaah ambaye (hawezi) kutunufaisha wala (hawezi) kutudhuru, na tuje kurudishwa nyuma juu ya visigino vyetu baada ya kuwa Ameshatuongoza Allaah? Kama (mfano wa) yule ambaye amezubaishwa (kutangatanga) na mashaytwaan katika ardhi    akiwayawaya?” (Huku) Anao marafiki wanamwita katika mwongozo (wakimwambia) “Njoo.” Sema: Hakika Mwongozo wa Allaah ndio Mwongozo na tumeamrishwa tujisalimishe kwa Rabb (Mola) wa walimwengu.

وَأَنْ أَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَاتَّقُوهُ ۚ وَهُوَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٧٢
72. Na (tumeamrishwa): “Simamisheni Swalaah na mcheni Yeye, Naye Ndiye Ambaye Kwake (Pekee) mtakusanywa.”

وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۖ وَيَوْمَ يَقُولُ كُن فَيَكُونُ ۚ قَوْلُهُ الْحَقُّ ۚ وَلَهُ الْمُلْكُ يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ ۚ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿٧٣
73. Naye Ndiye Ambaye Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Na Siku Atakaposema: “Kun” (Kuwa) basi (jambo) litakuwa. Kauli Yake ni haki.  Naye (Pekee) Ana ufalme Siku itakapopulizwa baragumu. ‘Aalimu (Mjuzi) wa ghayb na dhahiri. Naye ni Al-Hakiymul-Khabiyr (Mwenye hikmah wa yote - Mjuzi wa yaliyodhahiri na yaliyofichikana).

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ آزَرَ أَتَتَّخِذُ أَصْنَامًا آلِهَةً ۖ إِنِّي أَرَاكَ وَقَوْمَكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٧٤
74. Na (taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Ibraahiym alipomwambia baba yake Aazar: “Je unachukua masanamu kuwa ni miungu? Hakika mimi nakuona (wewe) na watu wako katika upotofu ulio bayana.”
وَكَذَٰلِكَ نُرِي إِبْرَاهِيمَ مَلَكُوتَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلِيَكُونَ مِنَ الْمُوقِنِينَ ﴿٧٥
75. Na hivyo ndivyo Tulivyomwonyesha Ibraahiym ufalme wa mbingu na ardhi na ili awe miongoni mwa wenye yakini.

فَلَمَّا جَنَّ عَلَيْهِ اللَّيْلُ رَأَىٰ كَوْكَبًا ۖ قَالَ هَـٰذَا رَبِّي ۖ فَلَمَّا أَفَلَ قَالَ لَا أُحِبُّ الْآفِلِينَ ﴿٧٦
76. Na ulipomwingilia usiku akaona nyota (sayari ing’aayo). Akasema: “Huyu ni Rabb (Mola) wangu.” Ilipotoweka akasema: “Hakika mimi sipendi wanaotoweka.”

فَلَمَّا رَأَى الْقَمَرَ بَازِغًا قَالَ هَـٰذَا رَبِّي ۖ فَلَمَّا أَفَلَ قَالَ لَئِن لَّمْ يَهْدِنِي رَبِّي لَأَكُونَنَّ مِنَ الْقَوْمِ الضَّالِّينَ ﴿٧٧
77. (Na) Alipoona mwezi umechomoza akasema: “Huyu ni Rabb (Mola) wangu”. Ulipotoweka akasema: “Asiponiongoza Rabb wangu; bila shaka nitakuwa miongoni mwa watu waliopotea.”

فَلَمَّا رَأَى الشَّمْسَ بَازِغَةً قَالَ هَـٰذَا رَبِّي هَـٰذَا أَكْبَرُ ۖ فَلَمَّا أَفَلَتْ قَالَ يَا قَوْمِ إِنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ ﴿٧٨
78. (Na) Alipoliona jua limechomoza akasema: “Huyu ni Rabb (Mola) wangu, (kwani) huyu ni mkubwa zaidi.” Lilipotoweka akasema: “Enyi watu wangu! Hakika mimi simo katika yale mnayoyashirikisha (na Allaah).”

إِنِّي وَجَّهْتُ وَجْهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ حَنِيفًا ۖ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٧٩
79. “Hakika mimi nimeelekeza uso wangu kwa Ambaye Ameanzisha mbingu na ardhi haniyfaa (nimejiengua na upotofu na kuelemea Dini ya haki) nami si katika washirikina.”

وَحَاجَّهُ قَوْمُهُ ۚ قَالَ أَتُحَاجُّونِّي فِي اللَّـهِ وَقَدْ هَدَانِ ۚ وَلَا أَخَافُ مَا تُشْرِكُونَ بِهِ إِلَّا أَن يَشَاءَ رَبِّي شَيْئًا ۗ وَسِعَ رَبِّي كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا ۗ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ ﴿٨٠
80. Na watu wake wakabishana naye. Akasema: “Je, mnabishana nami kuhusu Allaah na hali Ameniongoa? Na wala sikhofu mnayomshirikisha Naye (na hakuna kitachonisibu) isipokuwa Rabb (Mola) wangu Akitaka lolote (linifike, basi litanifika). Rabb wangu Amezunguka kila kitu kwa Ujuzi. Je, basi hamuwaidhiki?”

وَكَيْفَ أَخَافُ مَا أَشْرَكْتُمْ وَلَا تَخَافُونَ أَنَّكُمْ أَشْرَكْتُم بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَانًا ۚ فَأَيُّ الْفَرِيقَيْنِ أَحَقُّ بِالْأَمْنِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٨١
81. “Na vipi nikhofu yale mnayoyashirikisha, na wala (nyinyi) hamkhofu kwamba mnamshirikisha Allaah kwa ambayo Hakuyateremshia kwenu hoja. Je, basi kundi gani kati ya mawili (nyinyi au mimi) linastahiki zaidi kuwa katika amani kama nyinyi mnajua?”

الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٨٢
82. Wale walioamini na hawakuchanganya iymaan zao na dhulma - hao ndio watakaopata amani nao ndio walioongoka.

وَتِلْكَ حُجَّتُنَا آتَيْنَاهَا إِبْرَاهِيمَ عَلَىٰ قَوْمِهِ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاءُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿٨٣
83. Na hiyo ndio hoja Yetu Tuliyompa Ibraahiym juu ya watu wake.  Tunampandisha cheo Tumtakaye. Hakika Rabb (Mola) wako ni Hakiymun-‘Aliym (Mwenye hikmah wa yote - Mjuzi wa yote).

وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ كُلًّا هَدَيْنَا ۚ وَنُوحًا هَدَيْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِ دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَارُونَ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٤
84. Na Tukamtunukia (Ibraahiym mwana;) Is-haaq, na (mjukuu) Ya’quwb. Wote Tukawaongoa. Na Nuwh Tulimwongoa kabla (ya Nabiy Ibraahiym). Na katika dhuria wake Daawuwd, na Sulaymaan, na Ayyuwb, na Yuwsuf, na Muwsaa, na Haaruwn. Na hivyo ndivyo Tulipavyo wafanyao ihsaan.

وَزَكَرِيَّا وَيَحْيَىٰ وَعِيسَىٰ وَإِلْيَاسَ ۖ كُلٌّ مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٨٥
85. Na Zakariyyaa, na Yahyaa, na ‘Iysaa, na Ilyaas. Wote ni miongoni mwa Swalihina.

وَإِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطًا ۚ وَكُلًّا فَضَّلْنَا عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٨٦
86. Na Ismaa’iyl, na Al-Yasa’a na Yuwnus, na Luwtw. Na wote Tuliwafadhilisha juu ya walimwengu.

وَمِنْ آبَائِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ وَإِخْوَانِهِمْ ۖ وَاجْتَبَيْنَاهُمْ وَهَدَيْنَاهُمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٨٧
87. Na katika baba zao, na dhuriya wao, na ndugu zao. Na Tukawateua na Tukawaongoza kuelekea njia iliyonyooka.

ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚ وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٨
88. Huo ni Mwongozo wa Allaah, kwa huo, Humwongoza Amtakaye kati ya waja Wake. Na kama wangemshirikisha bila shaka yangebatilika yale waliyokuwa wakitenda.

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ۚ فَإِن يَكْفُرْ بِهَا هَـٰؤُلَاءِ فَقَدْ وَكَّلْنَا بِهَا قَوْمًا لَّيْسُوا بِهَا بِكَافِرِينَ ﴿٨٩
89. Hao ndio wale Tuliowapa Kitabu na Hukumu na Unabiy. Wakiyakanusha hawa (makafari) basi kwa yakini Tumekwishayawakilisha kwa watu wasioyakanusha.

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۖ فَبِهُدَاهُمُ اقْتَدِهْ ۗ قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا ۖ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْعَالَمِينَ ﴿٩٠
90. Hao ndio ambao Allaah Amewaongoa. Basi fuata kama kigezo mwongozo wao. Sema: “Sikuombeni ujira kwa hayo. Hayakuwa haya ila ni ukumbusho (mawaidha na kumbukumbu) kwa walimwengu.”


وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ إِذْ قَالُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ عَلَىٰ بَشَرٍ مِّن شَيْءٍ ۗ قُلْ مَنْ أَنزَلَ الْكِتَابَ الَّذِي جَاءَ بِهِ مُوسَىٰ نُورًا وَهُدًى لِّلنَّاسِ ۖ تَجْعَلُونَهُ قَرَاطِيسَ تُبْدُونَهَا وَتُخْفُونَ كَثِيرًا ۖ وَعُلِّمْتُم مَّا لَمْ تَعْلَمُوا أَنتُمْ وَلَا آبَاؤُكُمْ ۖ قُلِ اللَّـهُ ۖ ثُمَّ ذَرْهُمْ فِي خَوْضِهِمْ يَلْعَبُونَ ﴿٩١
91. Na hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiriya, (pale Mayahudi) waliposema: “Allaah Hakuteremsha chochote kwa mtu.” Sema: (uwaulize): “Nani aliyeteremsha Kitabu ambacho amekuja nacho Muwsaa, (chenye) nuru na mwongozo kwa watu. Mnakifanya kurasa kurasa mkizifichua na mkificha mengi. Na mkafunzwa yale mliyokuwa hamuyajui nyinyi na wala baba zenu.” Sema: “Allaah” (Ameiteremsha); kisha waachilie mbali katika shughuliko la porojo lao wakicheza.

وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ مُّصَدِّقُ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَلِتُنذِرَ أُمَّ الْقُرَىٰ وَمَنْ حَوْلَهَا ۚ وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۖ وَهُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ ﴿٩٢
92. Na hiki Kitabu (Qur-aan) Tumekiteremsha chenye baraka kinachosadikisha yale ambayo yaliyokitangulia na ili uwaonye (watu wa) Ummul-Quraa (Mama wa miji – Makkah) na (nchi) ziloizunguka. Na wale wanaoamini Aakhirah wanakiamini. Nao wanahifadhi Swalaah zao.

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ قَالَ أُوحِيَ إِلَيَّ وَلَمْ يُوحَ إِلَيْهِ شَيْءٌ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثْلَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ ۗ وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الظَّالِمُونَ فِي غَمَرَاتِ الْمَوْتِ وَالْمَلَائِكَةُ بَاسِطُو أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوا أَنفُسَكُمُ ۖ الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ وَكُنتُمْ عَنْ آيَاتِهِ تَسْتَكْبِرُونَ ﴿٩٣
93. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemtungia uongo Allaah au akasema: “Nimefunuliwa Wahy” na hali hakufunuliwa Wahy wowote.   Na yule asemaye: “Nitateremsha mfano wa yale Aliyoyateremsha Allaah.” Na lau ungeliona madhalimu pale wakiwa katika mateso makali ya mauti, na Malaika wamenyosha mikono yao (wakiwaambia): “Zitoeni nafsi zenu! Leo mnalipwa adhabu ya kudhalilisha kwa yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Allaah pasi na haki, na (kwa vile) mlivyokuwa mkitakabari kuhusu Aayaat (na ishara, hoja) Zake.

وَلَقَدْ جِئْتُمُونَا فُرَادَىٰ كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَتَرَكْتُم مَّا خَوَّلْنَاكُمْ وَرَاءَ ظُهُورِكُمْ ۖ وَمَا نَرَىٰ مَعَكُمْ شُفَعَاءَكُمُ الَّذِينَ زَعَمْتُمْ أَنَّهُمْ فِيكُمْ شُرَكَاءُ ۚ لَقَد تَّقَطَّعَ بَيْنَكُمْ وَضَلَّ عَنكُم مَّا كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٩٤
94. Na (Wataambiwa): “Kwa yakini mmetujia mmoja mmoja kama Tulivyokuumbeni mara ya kwanza; na mmeyaacha nyuma yenu Tuliyokuruzukuni. Na Hatuwaoni pamoja nanyi waombezi wenu ambao mlidai kwamba wao kwenu ni washirika (wa Allaah). Kwa yakini yamekatika (mahusiano) baina yenu na yamekupoteeni mliyokuwa mkidai.”

إِنَّ اللَّـهَ فَالِقُ الْحَبِّ وَالنَّوَىٰ ۖ يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَمُخْرِجُ الْمَيِّتِ مِنَ الْحَيِّ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٩٥
95. Hakika Allaah ni Mpasuaji wa mbegu na kokwa (zikawa miche). Anatoa kilicho hai kutokana na kilichomfu na Mtoaji kilichomfu kutokana na kilicho hai. Huyo Ndiye kwenu Allaah. Basi wapi mnageuzwa (mbali na haki)?

فَالِقُ الْإِصْبَاحِ وَجَعَلَ اللَّيْلَ سَكَنًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ حُسْبَانًا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ﴿٩٦
96. Mpasuaji wa mapambazuko ya asubuhi, na Akajaalia usiku kuwa ni    utulivu (mapumziko); na jua na mwezi kwenda kwa hisabu. Hivyo ndio ukadiriaji wa ‘Aziyzil-‘Aliym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika – Mjuzi wa yote).

وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ النُّجُومَ لِتَهْتَدُوا بِهَا فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٩٧
97. Na Yeye Ndiye Ambaye Aliyekufanyieni nyota ili muongozwe kwazo (njia) katika viza vya bara na bahari. Kwa yakini Tumezifasili Aayaat (ishara, hoja) kwa watu wanaojua.

وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ فَمُسْتَقَرٌّ وَمُسْتَوْدَعٌ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَفْقَهُونَ ﴿٩٨
98. Na Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja, basi (pako) mahali pa kutulia (tumboni mwa mama au duniani) na (pako) pa kuhifadhiwa (baada ya kufa). Kwa yakini Tumezifasili Aayaat (ishara, hoja n.k) kwa watu wanaofahamu.

وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ نَبَاتَ كُلِّ شَيْءٍ فَأَخْرَجْنَا مِنْهُ خَضِرًا نُّخْرِجُ مِنْهُ حَبًّا مُّتَرَاكِبًا وَمِنَ النَّخْلِ مِن طَلْعِهَا قِنْوَانٌ دَانِيَةٌ وَجَنَّاتٍ مِّنْ أَعْنَابٍ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُشْتَبِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ ۗ انظُرُوا إِلَىٰ ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَيَنْعِهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكُمْ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٩٩
99. Na Yeye Ndiye Ambaye Ameteremsha kutoka mbinguni maji, Tukatoa kwayo mimea ya kila kitu, na Tukatoa kutoka humo mimea ya kijani, Tunatoa kutoka humo punje zinazopandana; na katika mitende (vinatoka) katika makole yake mashada yenye kuning’inia chini kwa chini, na (Anakuotesheeni) mabustani ya mizabibu na zaytuni, na makomamanga, yanayofanana na yasiyofanana. Tazameni matunda yake yanapozaa na na kuiva kwake. Hakika katika hayo mna Aayaat (ishara, dalili, zingatio n.k) kwenu kwa watu wanaoamini.

وَجَعَلُوا لِلَّـهِ شُرَكَاءَ الْجِنَّ وَخَلَقَهُمْ ۖ وَخَرَقُوا لَهُ بَنِينَ وَبَنَاتٍ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٠٠
100. Na (juu ya hivyo) wamemfanyia Allaah majini kuwa ni washirika Wake; na hali (Yeye Ndiye) Aliyewaumba. Na wakamsingizia bila ya ujuzi wowote kuwa ana wana wa kiume na wa kike. Subhaanahu wa Ta’aala (Utakasifu ni Wake na Ametukuka kwa ‘Uluwa) kutokana na yale   wanayoyaelezea.

بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ وَلَدٌ وَلَمْ تَكُن لَّهُ صَاحِبَةٌ ۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٠١
101. Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Inamkinikaje kuwa Yeye Ana waladi na hali hana mke! Naye Ameumba kila kitu, Naye kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi).

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ ﴿١٠٢
102. Huyo kwenu Ndiye Allaah, Rabb (Mola) wenu. Hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye Muumbaji wa kila kitu, basi mwabuduni Yeye Pekee. Naye juu ya kila kitu ni Wakiyl (Mdhamini Anayetegemewa kwa yote).

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٠٣
103. Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote; Naye ni Al-Latwiyful-Khabiyr (Mjuzi wa yaliyofichika - Mjuzi wa yaliyodhahiri na yaliyofichikana).

قَدْ جَاءَكُم بَصَائِرُ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَنْ أَبْصَرَ فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ عَمِيَ فَعَلَيْهَا ۚ وَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِحَفِيظٍ ﴿١٠٤
104. Kwa yakini imekujieni baswaairu (nuru za elimu, umaizi) kutoka kwa Rabb (Mola) wenu. Basi aliyefunua macho (yakampelekea kutambua) ni kwa (faida ya) nafsi yake; na aliyepofuka basi ni kwa dhara yake mwenyewe, (sema ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) “nami si mlinzi kwenu.”

وَكَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ وَلِيَقُولُوا دَرَسْتَ وَلِنُبَيِّنَهُ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿١٠٥
105. Na hivyo ndivyo Tunavyosarifu Aayaat (ishara, dalili, n.k) na wao (makafiri) waseme (kukuambia): “Umesoma” (na umejifunza kutoka Ahlil-Kitaab) na ili Tuibainishe kwa watu wenye kujua.

اتَّبِعْ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٠٦
106. Fuata (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uliyofunuliwa Wahy kutokana na Rabb (Mola) wako: Hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye na jitenge na washirikina.

وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا أَشْرَكُوا ۗ وَمَا جَعَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ۖ وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ ﴿١٠٧
107. Na lau Allaah Angetaka wasingelishirikisha. Na Hatukukufanya wewe uwe mlinzi juu yao, na wewe si mwenye jukumu la kuwakilishwa juu yao.

وَلَا تَسُبُّوا الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ فَيَسُبُّوا اللَّـهَ عَدْوًا بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ كَذَٰلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِم مَّرْجِعُهُمْ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٠٨
108. Na wala msiwatukane wale wanaowaomba asiyekuwa Allaah; wasije (nao) kumtukana Allaah kwa uadui bila ya kujua. Hivyo ndivyo Tumewapambia kila ummah ‘amali zao, kisha kwa Rabb (Mola) wao Pekee yatakuwa marejeo yao, Atawajulisha kwa yale waliyokuwa wakitenda.

وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ لَئِن جَاءَتْهُمْ آيَةٌ لَّيُؤْمِنُنَّ بِهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا الْآيَاتُ عِندَ اللَّـهِ ۖ وَمَا يُشْعِرُكُمْ أَنَّهَا إِذَا جَاءَتْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠٩
109. Na (makafiri) waliapa kwa (jina la) Allaah kwa viapo vya nguvu; kwamba ikiwafikia Aayah (muujiza) bila shaka wataiamini. Sema: “Hakika Aayaat ziko kwa Allaah. Na kitu gani kitakutambulisheni kwamba zitakapokuja (hizo Aayaat) hawataamini?”

وَنُقَلِّبُ أَفْئِدَتَهُمْ وَأَبْصَارَهُمْ كَمَا لَمْ يُؤْمِنُوا بِهِ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَنَذَرُهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١١٠
110. Na Tunazigeuza nyoyo zao na macho yao kama wasivyoiamini mara ya kwanza. Na Tunawaacha katika upindukaji mipaka ya kuasi kwao, wanatangatanga kwa upofu.


وَلَوْ أَنَّنَا نَزَّلْنَا إِلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ الْمَوْتَىٰ وَحَشَرْنَا عَلَيْهِمْ كُلَّ شَيْءٍ قُبُلًا مَّا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ يَجْهَلُونَ ﴿١١١﴾
111. Na lau kama Sisi Tungeliwateremshia Malaika na wakasemeshwa na wafu na Tukawakusanyia kila kitu mbele yao wasingeliamini ila Allaah Atake, lakini wengi wao wamo ujingani.

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا شَيَاطِينَ الْإِنسِ وَالْجِنِّ يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا ۚ وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ ﴿١١٢﴾
112. Na hivyo ndivyo Tulivyojaalia kwa kila Nabiy maadui; (nao ni) mashaytwaan katika wanadamu na majini wakidokezana wenyewe kwa wenyewe maneno ya kupambapamba na ya ghururi. Na lau Angetaka Rabb (Mola) wako wasingeliyafanya (hayo). Basi waachilie mbali na wanayoyatunga.

وَلِتَصْغَىٰ إِلَيْهِ أَفْئِدَةُ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَلِيَرْضَوْهُ وَلِيَقْتَرِفُوا مَا هُم مُّقْتَرِفُونَ ﴿١١٣﴾
113. Na ili zielemee kwayo (hayo maneno yao) nyoyo za wale wasioamini Aakhirah na ili waridhike nayo na ili wachumie (madhambi) wanayoyachumia.

أَفَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْتَغِي حَكَمًا وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ إِلَيْكُمُ الْكِتَابَ مُفَصَّلًا ۚ وَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْلَمُونَ أَنَّهُ مُنَزَّلٌ مِّن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ ﴿١١٤﴾
114. (Sema): “Je, nitafute hakimu ghairi ya Allaah (atuhukumu baina yetu) Naye Ndiye Ambaye Aliyekuteremshieni Kitabu kilichofasiliwa?” Na wale Tuliowapa Kitabu (kabla) wanajua kwamba kimeteremshwa kutoka kwa Rabb (Mola) wako kwa haki. Basi usijekuwa miongoni mwa wanaotia shaka.

وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقًا وَعَدْلًا ۚ لَّا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١١٥﴾
115. Na limetimia neno la Rabb (Mola) wako kwa kweli na uadilifu. Hakuna mwenye kuyabadilisha maneno Yake. Naye ni As-Samiy’ul-‘Aliym (Mwenye kusikia yote – Mjuzi wa yote).

وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ ﴿١١٦﴾
116. Na kama ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, watakupoteza na njia ya Allaah. Hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawakuwa ila wenye kubuni uongo.

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ مَن يَضِلُّ عَن سَبِيلِهِ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿١١٧﴾
117. Hakika Rabb (Mola) wako Anajua zaidi mwenye kupotea na njia Yake. Naye Anajua zaidi wenye kuongoka.

فَكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ إِن كُنتُم بِآيَاتِهِ مُؤْمِنِينَ ﴿١١٨﴾
118. Basi kuleni (nyama) iliyotajwa Jina la Allaah (wakati wa kuchinjwa) mkiwa nyinyi ni wenye kuziamini Aayaat (na hukmu) Zake.


وَمَا لَكُمْ أَلَّا تَأْكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا لَّيُضِلُّونَ بِأَهْوَائِهِم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِالْمُعْتَدِينَ ﴿١١٩﴾
119. Na kwa nini msile (nyama) iliyotajwa Jina la Allaah na ilhali Ameshafasilisha kwenu yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura. Na hakika wengi (ya watu) wanapoteza (wengine) kwa hawaa zao bila ya elimu. Hakika Rabb (Mola) wako Yeye Anajua Zaidi wenye kutaadi.


وَذَرُوا ظَاهِرَ الْإِثْمِ وَبَاطِنَهُ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَكْسِبُونَ الْإِثْمَ سَيُجْزَوْنَ بِمَا كَانُوا يَقْتَرِفُونَ ﴿١٢٠﴾
120. Na acheni dhambi zilizodhihirika na zilizofichika. Hakika wale wanaochuma dhambi watalipwa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.


وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُ لَفِسْقٌ ۗ وَإِنَّ الشَّيَاطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰ أَوْلِيَائِهِمْ لِيُجَادِلُوكُمْ ۖ وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ ﴿١٢١﴾
121. Na wala msile (nyama ya) ambayo haikutajwa Jina la Allaah (wakati wa kuchinjwa), kwani huo ni ufasiki. Na hakika mashaytwaan wanadokeza marafiki wandani wao (kati ya binaadam) wabishane nanyi. Na mtakapowatii hakika mtakuwa washirikina.


أَوَمَن كَانَ مَيْتًا فَأَحْيَيْنَاهُ وَجَعَلْنَا لَهُ نُورًا يَمْشِي بِهِ فِي النَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُ فِي الظُّلُمَاتِ لَيْسَ بِخَارِجٍ مِّنْهَا ۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْكَافِرِينَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٢٢﴾
122. Je, aliyekuwa maiti kisha Tukamhuisha na Tukamjaalia nuru anatembea kwayo kati ya watu, ni sawa na yule ambaye yumo katika viza si mwenye kutoka humo? Hivyo ndivyo walivyopambiwa makafiri yale waliyokuwa wakiyatenda.


وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا فِي كُلِّ قَرْيَةٍ أَكَابِرَ مُجْرِمِيهَا لِيَمْكُرُوا فِيهَا ۖ وَمَا يَمْكُرُونَ إِلَّا بِأَنفُسِهِمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿١٢٣﴾
123. Na hivyo ndivyo Tulivyojaalia katika kila mji wahalifu wao wakuu kabisa ili wafanyie njama humo. Na hawafanyii njama ila nafsi zao, na wala hawahisi.


وَإِذَا جَاءَتْهُمْ آيَةٌ قَالُوا لَن نُّؤْمِنَ حَتَّىٰ نُؤْتَىٰ مِثْلَ مَا أُوتِيَ رُسُلُ اللَّـهِ ۘ اللَّـهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسَالَتَهُ ۗ سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِندَ اللَّـهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ ﴿١٢٤﴾
124. Na inapowajia Aayah (muujiza, hoja) husema: “Hatutoamini mpaka tupewe mfano wa yale waliopewa Rasuli wa Allaah.  Allaah Anajua zaidi wapi Aweke Risaala Yake. Itawasibu wale waliohalifu, udhalilifu mbele ya Allaah na adhabu kali kwa yale waliyokuwa wakifanya njama.


فَمَن يُرِدِ اللَّـهُ أَن يَهْدِيَهُ يَشْرَحْ صَدْرَهُ لِلْإِسْلَامِ ۖ وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُ يَجْعَلْ صَدْرَهُ ضَيِّقًا حَرَجًا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِي السَّمَاءِ ۚ كَذَٰلِكَ يَجْعَلُ اللَّـهُ الرِّجْسَ عَلَى الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٢٥﴾
125. Basi yule ambaye Allaah Anataka kumwongoza, Humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na yule ambaye (Allaah) Anataka kumpotoa, Hufanya kifua chake kuwa na dhiki chenye kubana kama kwamba anapanda kwa tabu mbinguni. Hivyo ndivyo Allaah Anavojaalia ar-rijsa (adhabu, shaywtwaan na kila lisokuwa la kheri) juu ya wale wasioamini.


وَهَـٰذَا صِرَاطُ رَبِّكَ مُسْتَقِيمًا ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ ﴿١٢٦﴾
126. Na hii ni njia ya Rabb (Mola) wako iliyonyooka. Kwa yakini Tumefasili Aayaat (na ishara, dalili) kwa watu wanaokumbuka.


لَهُمْ دَارُ السَّلَامِ عِندَ رَبِّهِمْ ۖ وَهُوَ وَلِيُّهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٢٧﴾
127. Watapata (Jannah ya) Daarus-Salaam kwa Rabb (Mola) wao.  Naye Ndiye Waliyy (Mlinzi, Msaidizi) wao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda.


وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ قَدِ اسْتَكْثَرْتُم مِّنَ الْإِنسِ ۖ وَقَالَ أَوْلِيَاؤُهُم مِّنَ الْإِنسِ رَبَّنَا اسْتَمْتَعَ بَعْضُنَا بِبَعْضٍ وَبَلَغْنَا أَجَلَنَا الَّذِي أَجَّلْتَ لَنَا ۚ قَالَ النَّارُ مَثْوَاكُمْ خَالِدِينَ فِيهَا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿١٢٨﴾
128. Na (taja ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Siku Atakapowakusanya wote (kisha Allaah Awaambie): “Enyi makundi ya majini! Kwa yakini mmetafuta kwa wingi (kuwapoteza) katika wanadamu.” Na watasema marafiki wao wandani na wasaidizi katika wanadamu: “Rabb (Mola) wetu! Tulinufaishana baadhi yetu na wengineo, na tumefikia muda wetu ambao Umetupangia.” (Allaah) Atasema: “Moto ndio makazi yenu, ni wenye kudumu humo, isipokuwa Anavotaka Allaah”. Hakika Rabb wako ni Hakiymun-‘Aliym (Mwenye hikmah wa yote - Mjuzi wa yote).


وَكَذَٰلِكَ نُوَلِّي بَعْضَ الظَّالِمِينَ بَعْضًا بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿١٢٩﴾
129. Na hivyo ndivyo Tunavyowafanya baadhi ya madhalimu kuwa marafiki wandani juu ya wengine, kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.


يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِي وَيُنذِرُونَكُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا ۚ قَالُوا شَهِدْنَا عَلَىٰ أَنفُسِنَا ۖ وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَشَهِدُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَنَّهُمْ كَانُوا كَافِرِينَ ﴿١٣٠﴾
130. (Siku ya Qiyaamah wataambiwa): “Enyi wenzi wa majini na wanadamu! Je hawajakufikieni Rasuli miongoni mwenu wanakusimulieni Aayaat Zangu na Wanakuonyeni (kuhusu) kukutana na Siku yenu hii?” Watasema: “Tumeshuhudia dhidi ya nafsi zetu.” Na uliwaghururi uhai wa dunia; na wameshuhudia dhidi ya nafsi zao kwamba hakika wao walikuwa ni makafiri.

ذَٰلِكَ أَن لَّمْ يَكُن رَّبُّكَ مُهْلِكَ الْقُرَىٰ بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا غَافِلُونَ ﴿١٣١﴾
131. Hivyo ni kwa kuwa Rabb (Mola) wako Hakuwa Mwenye kuangamiza mji kwa dhulma hali wenyewe wameghafilika.


وَلِكُلٍّ دَرَجَاتٌ مِّمَّا عَمِلُوا ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ ﴿١٣٢﴾
132. Na wote wana daraja (mbalimbali) kwa yale waliyoyatenda. Na Rabb (Mola) wako si Mwenye kughafilika na yale waliyoyatenda.


وَرَبُّكَ الْغَنِيُّ ذُو الرَّحْمَةِ ۚ إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَسْتَخْلِفْ مِن بَعْدِكُم مَّا يَشَاءُ كَمَا أَنشَأَكُم مِّن ذُرِّيَّةِ قَوْمٍ آخَرِينَ ﴿١٣٣﴾
133. Na Rabb (Mola) wako ni Al-Ghaniyy (Mkwasi) Mwenye Rahmah. Akitaka Atakuondosheni na Aweke wengine watakaofuatia baada yenu kwa Atakao, kama vile Alivyokuzalisheni kutokana na vizazi vya watu wengine.


إِنَّ مَا تُوعَدُونَ لَآتٍ ۖ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ ﴿١٣٤﴾
134. Hakika mnayoahidiwa yatakuja (tu bila shaka). Na wala nyinyi si wenye kushinda kukwepa (adhabu ya Allaah).


قُلْ يَا قَوْمِ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن تَكُونُ لَهُ عَاقِبَةُ الدَّارِ ۗ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ ﴿١٣٥﴾
135. Sema: “Enyi kaumu yangu! Tendeni (yenu mnayotaka) kwa tamkini yenu, nami (pia) natenda yangu. Mtakuja kujua nani atakayekuwa na hatima (nzuri) ya makazi (ya Aakhirah). Hakika madhalimu hawatofaulu.


وَجَعَلُوا لِلَّـهِ مِمَّا ذَرَأَ مِنَ الْحَرْثِ وَالْأَنْعَامِ نَصِيبًا فَقَالُوا هَـٰذَا لِلَّـهِ بِزَعْمِهِمْ وَهَـٰذَا لِشُرَكَائِنَا ۖ فَمَا كَانَ لِشُرَكَائِهِمْ فَلَا يَصِلُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَمَا كَانَ لِلَّـهِ فَهُوَ يَصِلُ إِلَىٰ شُرَكَائِهِمْ ۗ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ ﴿١٣٦﴾
136. Na wamemfanyia Allaah sehemu katika mimea na wanyama Aliyoumba. Wakasema: Hii ni (sehemu) ya Allaah kwa madai yao, na hii (sehemu nyingine) ni kwa ajili ya tunaowashirikisha (miungu yetu). Basi vile vilokuwa (vimekusudiwa) vya washirika wao havimfikii Allaah. Na vile vilokuwa vya Allaah hufika kwa waliowashirikisha (waungu wao). Uovu ulioje wanayoyahukumu.


وَكَذَٰلِكَ زَيَّنَ لِكَثِيرٍ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ قَتْلَ أَوْلَادِهِمْ شُرَكَاؤُهُمْ لِيُرْدُوهُمْ وَلِيَلْبِسُوا عَلَيْهِمْ دِينَهُمْ ۖ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ ﴿١٣٧﴾
137. Na hivyo ndivyo washirikina wengi walivyopambiwa na washirika wao (wanaowaabudu) kuua auladi wao ili wawateketeze na wawatatanishe dini yao. Na lau Allaah Angetaka, wasingeliyafanya hayo. Basi waachilie mbali na (hayo) wanayoyatunga.


وَقَالُوا هَـٰذِهِ أَنْعَامٌ وَحَرْثٌ حِجْرٌ لَّا يَطْعَمُهَا إِلَّا مَن نَّشَاءُ بِزَعْمِهِمْ وَأَنْعَامٌ حُرِّمَتْ ظُهُورُهَا وَأَنْعَامٌ لَّا يَذْكُرُونَ اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهَا افْتِرَاءً عَلَيْهِ ۚ سَيَجْزِيهِم بِمَا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿١٣٨﴾
138. Na wakasema: “Hawa wanyama (wa mifugo) na mazao ni marufuku; hawatowala ila wale tuwatakao” Kwa madai yao tu. Na (wanasema): “Na wanyama imeharamishwa migongo yao (kuwapanda) na wanyama (wengine) hawalitaji Jina la Allaah juu yao (wanapowachinja), wanamtungia (Allaah). Atawalipa kwa yale aliyokuwa wakiyatunga.”


وَقَالُوا مَا فِي بُطُونِ هَـٰذِهِ الْأَنْعَامِ خَالِصَةٌ لِّذُكُورِنَا وَمُحَرَّمٌ عَلَىٰ أَزْوَاجِنَا ۖ وَإِن يَكُن مَّيْتَةً فَهُمْ فِيهِ شُرَكَاءُ ۚ سَيَجْزِيهِمْ وَصْفَهُمْ ۚ إِنَّهُ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿١٣٩﴾
139. Na wakasema (pia): “Vilivyokuwemo matumboni mwa wanyama hawa ni makhsusi (halaal pekee) kwa wanaume wetu na wameharamishiwa kwa wake zetu.” Lakini wanapokuwa ni nyamafu (pale wanapozaliwa) basi katika hao huwa wanashirikiana (na wanawake wakala). Hakika (Allaah) Atawalipa wasifu wao. Hakika Yeye ni Hakiymun-‘Aliym (Mwenye hikmah wa yote - Mjuzi wa yote).


قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ قَتَلُوا أَوْلَادَهُمْ سَفَهًا بِغَيْرِ عِلْمٍ وَحَرَّمُوا مَا رَزَقَهُمُ اللَّـهُ افْتِرَاءً عَلَى اللَّـهِ ۚ قَدْ ضَلُّوا وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ ﴿١٤٠﴾
140. Kwa yakini wamekhasirika wale waliowaua watoto wao kwa usafihi bila ya ujuzi na wakaharamisha vile Alivyowaruzuku Allaah kwa kumtungia Allaah. Kwa yakini wamepotea wala hawakuwa wenye kuongoka.


وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَ جَنَّاتٍ مَّعْرُوشَاتٍ وَغَيْرَ مَعْرُوشَاتٍ وَالنَّخْلَ وَالزَّرْعَ مُخْتَلِفًا أُكُلُهُ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُتَشَابِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ ۚ كُلُوا مِن ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَآتُوا حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ ۖ وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿١٤١﴾
141. Naye (Allaah) Ndiye Ambaye Aliyezalisha mabustani yanayotambaa (juu ya chanja na ardhini) na yasiyotambaa. Na (Akazalisha) mitende na mimea yakitofautiana vyakula (na ladha) yake, na zaytuni na makomamanga yanayoshabihiana na yasiyoshabihiana. Kuleni katika matunda yake yanapotoa mazao na toeni haki yake (Zakaah) siku ya kuvunwa kwake; na wala msifanye israfu. Hakika Yeye Hapendi wafanyao israfu.


وَمِنَ الْأَنْعَامِ حَمُولَةً وَفَرْشًا ۚ كُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿١٤٢﴾
142. Na katika wanyama (Amekuumbieni) wabebao mzigo na wadogodogo. Kuleni katika Alivyokuruzukuni Allaah na wala msifuate hatua za shaytwaan, hakika yeye ni adui bayana kwenu.


ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ ۖ مِّنَ الضَّأْنِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْمَعْزِ اثْنَيْنِ ۗ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الْأُنثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الْأُنثَيَيْنِ ۖ نَبِّئُونِي بِعِلْمٍ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٤٣﴾
143. (Amekuumbieni) Jozi nane (za wanyama madume na majike) Katika kondoo wawili (dume na jike), na katika mbuzi wawili (dume na jike). Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم uwaambie):  “Je, Ameharamisha wote madume wawili au majike mawili, au viliomo fukoni la uzazi mwa majike yote mawili?  Nijulisheni kwa elimu ikiwa nyinyi mnasema kweli.”



وَمِنَ الْإِبِلِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْبَقَرِ اثْنَيْنِ ۗ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الْأُنثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الْأُنثَيَيْنِ ۖ أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ وَصَّاكُمُ اللَّـهُ بِهَـٰذَا ۚ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا لِّيُضِلَّ النَّاسَ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿١٤٤﴾
144. Na katika ngamia, wawili na katika ng’ombe wawili. Sema (uwaambie): “Je, Ameharamisha madume wawili au majike mawili, au waliomo fukoni la uzazi mwa majike wawili? Au nyinyi mlishuhudia Allaah Alipokuusieni haya?” Basi nani dhalimu zaidi kuliko yute anayemtungia Allaah uongo ili apoteze watu bila elimu. Hakika Allaah Hawaongozi watu madhalimu.


قُل لَّا أَجِدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلَّا أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ أَوْ فِسْقًا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ ۚ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ رَبَّكَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤٥﴾
145. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Sipati katika yale niliyofunuliwa Wahyi kwangu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu (mzoga) au damu inayomwagika au nyama ya nguruwe; kwani hiyo ni rijsun (uchafu, haraam) au ufasiki; kimetajiwa ghairi ya Allaah (katika kuchinja kwake).” Basi atakayefikwa na dharura bila ya kutamani wala kuvuka mipaka, basi hakika Rabb (Mola) wako ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


وَعَلَى الَّذِينَ هَادُوا حَرَّمْنَا كُلَّ ذِي ظُفُرٍ ۖ وَمِنَ الْبَقَرِ وَالْغَنَمِ حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ شُحُومَهُمَا إِلَّا مَا حَمَلَتْ ظُهُورُهُمَا أَوِ الْحَوَايَا أَوْ مَا اخْتَلَطَ بِعَظْمٍ ۚ ذَٰلِكَ جَزَيْنَاهُم بِبَغْيِهِمْ ۖ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ ﴿١٤٦﴾
146. Na kwa wale walio Mayahudi Tuliharamisha kila (mnyama) mwenye kucha. Na katika ng’ombe na mbuzi Tuliwaharamishia shahamu zao isipokuwa iliyobeba migongo yao au utumbo wao au iliyochanganyika na mifupa.  Hivyo ndivyo Tulivyowalipa kwa udhalimu wao. Na bila shaka Sisi ni Wakweli.


فَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل رَّبُّكُمْ ذُو رَحْمَةٍ وَاسِعَةٍ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُهُ عَنِ الْقَوْمِ الْمُجْرِمِينَ ﴿١٤٧﴾
147. Wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم); basi sema: “Rabb (Mola) wenu ni Mwenye Rahmah ya wasaa (nyingi). Na wala haizuiliwi adhabu Yake dhidi ya watu wahalifu.”


سَيَقُولُ الَّذِينَ أَشْرَكُوا لَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا أَشْرَكْنَا وَلَا آبَاؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن شَيْءٍ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ حَتَّىٰ ذَاقُوا بَأْسَنَا ۗ قُلْ هَلْ عِندَكُم مِّنْ عِلْمٍ فَتُخْرِجُوهُ لَنَا ۖ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَخْرُصُونَ ﴿١٤٨﴾
148. Watasema wale walioshirikisha: “Lau Allaah Angetaka, tusingelifanya shirki, wala baba zetu (wasingelishirikisha pia); na wala tusingeliharamisha chochote.” Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale wa kabla yao mpaka walipoonja adhabu Yetu.  Sema: “Je, mna elimu yoyote mtutolee? Hamfuati isipokuwa dhana tu, nanyi si lolote ila mnabuni uongo.”


قُلْ فَلِلَّـهِ الْحُجَّةُ الْبَالِغَةُ ۖ فَلَوْ شَاءَ لَهَدَاكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿١٤٩﴾
149. Sema: “Basi ni Allaah Pekee Mwenye hoja baalighah (timilifu).” Na Angelitaka Angekuongozeni nyote.


قُلْ هَلُمَّ شُهَدَاءَكُمُ الَّذِينَ يَشْهَدُونَ أَنَّ اللَّـهَ حَرَّمَ هَـٰذَا ۖ فَإِن شَهِدُوا فَلَا تَشْهَدْ مَعَهُمْ ۚ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَهُم بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ ﴿١٥٠﴾
150. Sema: “Leteni mashahidi wenu wanaoshuhudia kwamba Allaah Ameharamisha (wanyama) hawa.” Wakishuhudia; basi usishuhudie pamoja nao. Na wala usifuate hawaa za wale wanaokadhibisha Aayaat (na ishara) Zetu, na wale wasioamini Aakhirah, nao wanamsawazisha Rabb (Mola) wao (na viumbe Vyake).


قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۖ وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُم مِّنْ إِمْلَاقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ ۖ وَلَا تَقْرَبُوا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ ۖ وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١٥١﴾
151. Sema: “Njooni nikusomeeni yale Aliyoyaharamisha Rabb (Mola) wenu kwenu. (Anaamrisha) Kwamba msimshirikishe na chochote, na muwafanyie ihsaan wazazi wawili, na wala msiwaue auladi wenu kutokana na umasikini. Sisi Tunakuruzukuni pamoja nao. Na wala msikaribie machafu yaliyo dhahiri na yaliyofichika. Na wala msiue nafsi ambayo Ameiharamisha Allaah (kuiua) isipokuwa kwa haki (ya shariy’ah). Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kutia akilini.”


وَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّىٰ يَبْلُغَ أَشُدَّهُ ۖ وَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ ۖ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۖ وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُوا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۖ وَبِعَهْدِ اللَّـهِ أَوْفُوا ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ ﴿١٥٢﴾
152. “Na wala msiikaribie mali ya yatima (kuila) isipokuwa kwa njia bora zaidi (ya kumtengenezea hicho chake) mpaka afikie kubalege. Na timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu. Hatukalifishi nafsi isipokuwa kadiri ya uwezo wake. Na mnaposema (katika kuhukumu au kushuhudia) basi fanyeni uadilifu japokuwa ni jamaa wa karibu. Na timizeni ahadi ya Allaah.  Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kukumbuka (na kuwaidhika).”

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٥٣﴾
153. “Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia (nyinginezo) zitakufarikisheni na njia Yake. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kuwa na taqwa.”


ثُمَّ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ تَمَامًا عَلَى الَّذِي أَحْسَنَ وَتَفْصِيلًا لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً لَّعَلَّهُم بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ يُؤْمِنُونَ ﴿١٥٤﴾
154. Kisha Tukampa Muwsaa Kitabu kutimiza (neema Zetu) juu ya yule aliyefanya ihsaan kuwa ni fasili ya kila kitu na ni mwongozo na Rahmah wapate kuamini kukutana na Rabb (Mola) wao.


وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ فَاتَّبِعُوهُ وَاتَّقُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٥٥﴾
155. Na hiki Kitabu (Qur-aan) Tumekiteremsha kilichobarikiwa, basi kifuateni na muwe na taqwa mpate kurehemewa.


أَن تَقُولُوا إِنَّمَا أُنزِلَ الْكِتَابُ عَلَىٰ طَائِفَتَيْنِ مِن قَبْلِنَا وَإِن كُنَّا عَن دِرَاسَتِهِمْ لَغَافِلِينَ ﴿١٥٦﴾
156. (Tumeteremsha Qur-aan) Msije (Siku ya Qiyaamah) kusema: “Hakika Kitabu kimeteremshwa juu ya makundi mawili (Mayahudi na Manaswara) kabla yetu; lakini tulikuwa bila ya shaka tumeghafilika kuhusu waliyokuwa wakiyasoma.”

أَوْ تَقُولُوا لَوْ أَنَّا أُنزِلَ عَلَيْنَا الْكِتَابُ لَكُنَّا أَهْدَىٰ مِنْهُمْ ۚ فَقَدْ جَاءَكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ ۚ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَذَّبَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَصَدَفَ عَنْهَا ۗ سَنَجْزِي الَّذِينَ يَصْدِفُونَ عَنْ آيَاتِنَا سُوءَ الْعَذَابِ بِمَا كَانُوا يَصْدِفُونَ ﴿١٥٧﴾
157. Au mkaseme: “Lau tungeliteremshiwa Kitabu basi, bila shaka tungelikuwa waongofu zaidi kuliko wao.” Kwa yakini imekwishakufikieni hoja bayana kutoka kwa Rabb (Mola) wenu na Mwongozo na Rahmah. Hivyo basi nani ni dhalimu zaidi kuliko yule aliyekadhibisha Aayaat (na ishara, dalili) za Allaah na akajitenga nazo? Tutawalipa wale wanaojitenga na Aayaat Zetu adhabu ovu kwa yale waliyokuwa wakijitenga (nayo).


هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ أَوْ يَأْتِيَ بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ ۗ يَوْمَ يَأْتِي بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ لَا يَنفَعُ نَفْسًا إِيمَانُهَا لَمْ تَكُنْ آمَنَتْ مِن قَبْلُ أَوْ كَسَبَتْ فِي إِيمَانِهَا خَيْرًا ۗ قُلِ انتَظِرُوا إِنَّا مُنتَظِرُونَ ﴿١٥٨﴾
158. Je, wanangojea jingine (lolote) isipokuwa wawafikie Malaika (kuwatoa roho) au awafikie Rabb (Mola) wako (kuwahukumu waja) au ziwajie baadhi za Aayaat za Rabb wako (alama kubwa za Qiyaamah)? Siku zitakapokuja baadhi za Aayaat za Rabb wako haitoifaa nafsi iymaan yake, ikiwa haikuamini kabla au haikuchuma katika iymaan yake kheri (yoyote). Sema: “Ngojeeni hakika nasi tunangojea.”


إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَّسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ ۚ إِنَّمَا أَمْرُهُمْ إِلَى اللَّـهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿١٥٩﴾
159. Hakika wale waliofarakisha dini yao na wakawa makundi makundi, huna (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم uhusiano) wa lolote nao. Hakika amri yao iko kwa Allaah, kisha Atawajulisha kwa yale waliyokuwa wakifanya.


مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا ۖ وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦٠﴾
160. Atakayekuja (Siku ya Qiyaamah) kwa ‘amali nzuri basi atapata (thawabu) kumi mfano wa hiyo. Na Atakayekuja kwa ovu basi hatolipwa ila mfano wake, nao hawatodhulumiwa.


قُلْ إِنَّنِي هَدَانِي رَبِّي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ دِينًا قِيَمًا مِّلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۚ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٦١﴾
161. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi, Ameniongoza Rabb (Mola) wangu kuelekea njia iliyonyooka, Dini iliyosimama thabiti, millah ya Ibraahiym haniyfaa (aliyejiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki) na hakuwa miongoni mwa washirikina.”


قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٢﴾
162. Sema: “Hakika Swalaah yangu, na nusukiy (kuchinja kafaara na ‘ibaadah zangu) na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah (Pekee) Rabb wa walimwengu.”


لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ ﴿١٦٣﴾
163. Hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza.


قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْغِي رَبًّا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَيْءٍ ۚ وَلَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ إِلَّا عَلَيْهَا ۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرْجِعُكُمْ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿١٦٤﴾
164. Sema “Je, nitake ghairi ya Allaah kuwa ni Rabb (Mola) na hali Yeye ni Rabb wa kila kitu? Na wala nafsi yoyote haitachuma (kheri au shari) ila juu yake. Na wala habebi mbebaji, mzigo (wa dhambi) wa mwengine. Kisha kwa Rabb wenu ndio marejeo yenu, Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkikhitilafiana nayo.”


وَهُوَ الَّذِي جَعَلَكُمْ خَلَائِفَ الْأَرْضِ وَرَفَعَ بَعْضَكُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِّيَبْلُوَكُمْ فِي مَا آتَاكُمْ ۗ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ الْعِقَابِ وَإِنَّهُ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٦٥﴾
165. Naye (Allaah) Ndiye Aliyekufanyeni warithi wa ardhi (kizazi kwa kizazi) na Akanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja mbali mbali; (rizki, nguvu, afya, khulqa, n.k.) ili Akujaribuni katika yale Aliyokupeni. Hakika Rabb (Mola) wako ni Mwepesi wa kuakibu, na hakika Yeye bila shaka ni Ghafuwrur-Rahiym (Mwingi wa kughufuria - Mwenye kurehemu).


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com