الحديث السابع والعشرون
"البر حسن الخلق"
عن النّوَّاسِ بْنِ سَمْعَانَ رضيَ اللهُ عَنْهُ عن النَّبي
صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((الْبِرُّ حُسْنُ الْخُلُقِ، وَالإِثْمُ مَا حاكَ في
نَفْسِكَ وَكَرِهْتَ أَنْ يَطَّلِعَ عَلَيْهِ النَّاسُ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ .
وعن وَابصَةَ بْنِ مَعْبَدٍ رضي اللهُ عَنْهُ
قالَ: قالَ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ((جِئْتَ
تَسأَلُ عَنِ الْبِرِّ؟)) . قُلْتُ: نَعَمْ. قَالَ: ((اسْتَفْتِ
قَلْبَكَ، الْبِرُّ مَا اطْمَأَنَّتْ إلَيْهِ النَّفْسُ وَاطْمَأَنَّ إلَيْهِ
الْقَلْبُ، وَالإِثْمُ مَا حاكَ في النَّفْسِ وَتَردَّدَ في الصَّدْرِ وَإنْ
أَفْتَاكَ النّاسُ وَأَفْتَوْكَ))
حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَيْنَاهُ في مُسْنَدَي الْإِمَامَيْنِ أَحْمَدَ
بْنِ حَنْبَلٍ وَالدَّارِمِيّ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ.
HADITHI
YA 27
UADILIFU
NI TABIA NZURI
Kutoka kwa
An-Nawwaas Ibn Sam'aan رضي الله عنه ambaye alisema kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم kasema:
Uadilifu ni
tabia nzuri na udhalimu ni kile kitu ambacho huyumbayumba (chenye mashaka)
katika nafsi yako na hupendelei watu kukitambua.
Imesimuliwa na
Muslim
Na kutoka kwa
Waabisah Ibn Ma'abad رضي الله عنه ambaye
alisema:
Nilikuja kwa Mtume صلى الله عليه وسلم naye akasema:
Umekuja
kuuliza juu uadilifu? Nikasema: Ndio . Akasema: Ushaurishe
moyo wako. Uadilifu ni kile ambacho nafsi yako inakihisi shwari na moyo wako
pia unahisi shwari, na udhalimu ni kile kinachoyumbayumba katika nafsi na
kwenda na kurudi kifuani ijapokuwa watu wamekupa shauri lao la kisheria
(kukipendelea).