الحديث الحادي والعشرون
"قل آمنت بالله ثم استقم"
عن أبي عَمْرو، وَقِيلَ: أبي عَمْرَةَ، سُفْيَانَ بْنِ عَبْدِ
اللهِ رَضيَ اللهُ عَنْهُ قَال: قُلْتُ: يا رَسُولَ الله، قُلْ لي في
الإِسْلاَمِ قَوْلاً، لاَ أَسْأَلُ عَنْهُ أَحَداً غَيْرَكَ. قَال: ((قُلْ:
آمَنْتُ باللهِ ثُمَّ اسْتَقِمْ)).
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA 21
SEMA NAMUAMINI ALLAH KISHA KUWA MWENYE MSIMAMO
Kutoka kwa Abu 'Amr, vile vile (anajulikana
kama) Abu 'Amra Sufyaan Ibn Abdillah رضي الله عنه ambaye amesema:
Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu,
niambie kitu kuhusu Uislamu ambacho siwezi kumuuliza mtu yeyote ila wewe.
Akasema (Mtume صلى الله عليه وسلم ) : Sema; Namuamini Allaah , kisha kuwa mwenye
kunyooka. (kwa kuendelea kufanya ibada na kuwa na msimamo madhubuti katika
dini)
Imesimuliwa na Muslim.