الحديث السادس والعشرون
"كل سلامى من الناس عليه صدقة"
عن أَبي هُرَيْرَةَ رَضي اللهُ عنه قال: قالَ رسُولُ الله صلى الله
عليه وسلم: ((كُلُّ سُلامَى مِنَ النَّاسِ عليه صَدَقَةٌ، كُلُّ يَوْمٍ تَطْلُعُ
فِيهِ الشَّمْسُ: تَعْدِلُ بَيْنَ اثْنَيْنِ صَدَقَةٌ، وتُعينُ الرَّجُلَ في
دَابَّتِهِ فَتَحْمِلُهُ عَلَيْها أو تَرْفَعُ لهُ عَلَيْها متَاَعَهُ صَدَقَةٌ،
والْكَلِمةُ الطَّيِّبةُ صَدَقَةٌ، وبكُلِّ خَطْوَةٍ تَمشِيها إلى الصَّلاةِ
صَدَقَةٌ، وتُمِيطُ الأَذَى عنِ الطَّرِيِق صَدَقَةٌ))
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ
HADITHI YA 26
KILA KIUNGO CHA MTU LAZIMA KITOLEWE SADAKA
Kutoka kwa Abu
Hurayra رضي الله عنه ambaye
alisema : Mtume صلى الله عليه وسلم
kasema :
Kila kiungo cha mtu
lazima kitolewe sadaka kila siku jua inapochomoza, kufanya haki
(uadilifu) baina ya watu wawili ni sadaka, kumsaidia mtu kupanda (mnyama) kwa
kumsaidia kumnyanyua au kumnyanyulia mizigo yake ni sadaka,
neno jema ni sadaka, kila hatua unayokwenda kuswali ni sadaka, kuondosha dhara
katika njia ni sadaka.
Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim