Muhammad: 47

مُحَمَّد
Muhammad: 47

(Imeteremka Madina)


Sura hii imeanza mwanzo wake kubainisha kwamba Mwenyezi Mungu amezibat'ilisha a'mali za makafiri kwa kuwa wamefuata upotovu, na amewafutia Waumini maovu yao kwa kufuata kwao Haki. Kama ilivyo eleza kwa urefu waajibu wa kuitetea Haki.  Na malipo hayo kwa Akhera ni kuingia Peponi. Na ikawahimiza Waumini wainusuru Dini ya Mwenyezi Mungu na wapigane kwa ajili yake. Na imeweka wazi kwamba wapotovu wakiacha Imani hufanya fisadi katika nchi na wakawatupa jamaa zao. Na inahadharisha juu ya wanaafiki kuwa pamoja na Waumini wakapeleleza siri zao wapate kuwavunja moyo. Na inawatishia wanaafiki kuwa yatachanwa mapazia yao wanayo jifichia, na Mtume wa Mwenyezi Mungu adhihirishe chuki zao. Na inawakataza Waumini wasiwe wanyonge katika kupambana na makafiri, na hali wao ndio watakao shinda, na Mwenyezi Mungu yu pamoja nao, na wala hatawanyima malipo ya kazi yao. Kisha Sura imekhitimisha kutaka watu watoe kwa sababu ya Sabili Llah, Njia ya Mwenyezi Mungu, na ikabainisha kwamba mwenye kufanya ubakhili katika hayo basi anajidhuru mwenyewe, na kwamba kuacha kufuata Haki inakuwa ndiyo sababu ya kuhiliki hao wenye kuacha na kuletwa kaumu nyengine zenye kuleta kheri.




بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ أَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ﴿١﴾
1. Wale waliokufuru na wakazuia (watu) njia ya Allaah, Atazipoteza ‘amali zao.


وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَآمَنُوا بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ مُحَمَّدٍ وَهُوَ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۙ كَفَّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَأَصْلَحَ بَالَهُمْ﴿٢﴾
2. Na wale walioamini na wakatenda mema na wakaamini yale aliyoteremshiwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), nayo ni ya haki kutoka kwa Rabb (Mola) wao, Atawafutia maovu yao na Atawatengenezea hali zao.


ذَٰلِكَ بِأَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا اتَّبَعُوا الْبَاطِلَ وَأَنَّ الَّذِينَ آمَنُوا اتَّبَعُوا الْحَقَّ مِن رَّبِّهِمْ ۚ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ اللَّـهُ لِلنَّاسِ أَمْثَالَهُمْ﴿٣﴾
3. Hivyo kwa kuwa wale waliokufuru wamefuata ubatilifu, na kwamba wale walioamini wamefuata haki kutoka kwa Rabb (Mola) wao. Hivyo ndivyo Allaah Anavyowapigia watu mifano yao.


فَإِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا فَضَرْبَ الرِّقَابِ حَتَّىٰ إِذَا أَثْخَنتُمُوهُمْ فَشُدُّوا الْوَثَاقَ فَإِمَّا مَنًّا بَعْدُ وَإِمَّا فِدَاءً حَتَّىٰ تَضَعَ الْحَرْبُ أَوْزَارَهَا ۚ ذَٰلِكَ وَلَوْ يَشَاءُ اللَّـهُ لَانتَصَرَ مِنْهُمْ وَلَـٰكِن لِّيَبْلُوَ بَعْضَكُم بِبَعْضٍ ۗ وَالَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَلَن يُضِلَّ أَعْمَالَهُمْ﴿٤﴾
4. Basi mtapokutana (vitani) na wale waliokufuru wapigeni shingo, mpaka muwashinde kwa kuwajeruhi na kuwaua basi fungeni barabara pingu; kisha ima (wafanyieni) ihsani baada hapo au wajifidie mpaka vita vitue mizigo yake. Hivyo (ndio amri), na lau Allaah Angelitaka Angewalipiza kisasi (Mwenyewe), lakini (Ameamrisha jihaad) ili Akujaribuni nyinyi kwa nyinyi. Na wale waliouliwa katika njia ya Allaah, basi Hatopoteza ‘amali zao.


سَيَهْدِيهِمْ وَيُصْلِحُ بَالَهُمْ﴿٥﴾
5. Atawaongoza na Atatengeneza hali zao.


وَيُدْخِلُهُمُ الْجَنَّةَ عَرَّفَهَا لَهُمْ﴿٦﴾
6. Na Atawaingiza Jannah Aliyoitambulisha kwao.


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّـهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ﴿٧﴾
7. Enyi mloamini! Mkisaidia kunusuru Dini ya Allaah, (Allaah) Atakunusuruni na Ataithibitisha miguu yenu.


وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْسًا لَّهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ﴿٨﴾
8. Na wale waliokufuru, basi ni maangamizo kwao, na Atapoteza ‘amali zao.


ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ﴿٩﴾
9. Hivyo kwa sababu wao wamekirihika ambayo Ameteremsha Allaah, basi Amezibatilisha ‘amali zao.


أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ دَمَّرَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ ۖ وَلِلْكَافِرِينَ أَمْثَالُهَا﴿١٠﴾
10. Je, hawakutembea katika ardhi wakatazama vipi imekuwa hatima ya ambao wa kabla yao? Allaah Amewadamirisha mbali, na kwa makafiri (itakuwa) mfano wa hayo.


ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ مَوْلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَأَنَّ الْكَافِرِينَ لَا مَوْلَىٰ لَهُمْ﴿١١﴾
11. Hivyo ni kwa kuwa Allaah ni Mawlaa (Mlinzi, Msaidizi) wa wale walioamini na kwamba makafiri hawana mlinzi.


إِنَّ اللَّـهَ يُدْخِلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا يَتَمَتَّعُونَ وَيَأْكُلُونَ كَمَا تَأْكُلُ الْأَنْعَامُ وَالنَّارُ مَثْوًى لَّهُمْ﴿١٢﴾
12. Hakika Allaah Atawaingiza wale walioamini na wakatenda mema Jannaat zipitazo chini yake mito. Na wale waliokufuru wanastarehe (duniani) na wanakula kama walavyo wanyama wa mifugo na Moto ndio makazi yao.


وَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ هِيَ أَشَدُّ قُوَّةً مِّن قَرْيَتِكَ الَّتِي أَخْرَجَتْكَ أَهْلَكْنَاهُمْ فَلَا نَاصِرَ لَهُمْ﴿١٣﴾
13. Na miji mingapi iliyokuwa yenye nguvu zaidi kuliko mji wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ambao umekutoa. Tuliwaangamiza basi hawakuwa na wa kuwanusuru.


أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّهِ كَمَن زُيِّنَ لَهُ سُوءُ عَمَلِهِ وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُم﴿١٤﴾
14. Je, basi ambaye alikuwa kwenye hoja bayana kutoka kwa Rabb (Mola) wake, ni sawa na ambaye amepambiwa uovu wa ‘amali zake na wakafuata hawaa zao?


مَّثَلُ الْجَنَّةِ الَّتِي وُعِدَ الْمُتَّقُونَ ۖ فِيهَا أَنْهَارٌ مِّن مَّاءٍ غَيْرِ آسِنٍ وَأَنْهَارٌ مِّن لَّبَنٍ لَّمْ يَتَغَيَّرْ طَعْمُهُ وَأَنْهَارٌ مِّنْ خَمْرٍ لَّذَّةٍ لِّلشَّارِبِينَ وَأَنْهَارٌ مِّنْ عَسَلٍ مُّصَفًّى ۖ وَلَهُمْ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَمَغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ ۖ كَمَنْ هُوَ خَالِدٌ فِي النَّارِ وَسُقُوا مَاءً حَمِيمًا فَقَطَّعَ أَمْعَاءَهُمْ﴿١٥﴾
15. Mfano wa Jannah ambayo wameahidiwa wenye taqwa; humo mna mito ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa haitaghayari ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywaji na mito ya asali iliyosafishwa. Tena watapata humo kila (aina ya) matunda na maghfirah kutoka kwa Rabb (Mola) wao. (Je, huyo ni) sawa na yule mwenye kudumu Motoni na wakinyweshwa maji yachemkayo yakikatakata machango yao?


وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ حَتَّىٰ إِذَا خَرَجُوا مِنْ عِندِكَ قَالُوا لِلَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مَاذَا قَالَ آنِفًا ۚ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ طَبَعَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُمْ﴿١٦﴾
16. Na miongoni mwao (wako) ambao wanakusikiliza kwa makini, mpaka wanapotoka kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) huwaambia wale waliopewa elimu: “Amesema nini sasa hivi?”  Hao ndio ambao Allaah Amepiga chapa juu ya nyoyo zao, na wakafuata hawaa zao.

وَالَّذِينَ اهْتَدَوْا زَادَهُمْ هُدًى وَآتَاهُمْ تَقْوَاهُمْ﴿١٧﴾
17. Na wale walioongoka, Anawazidishia Uongofu na Huwapa (tawfiyq ya) taqwa yao.


فَهَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً ۖ فَقَدْ جَاءَ أَشْرَاطُهَا ۚ فَأَنَّىٰ لَهُمْ إِذَا جَاءَتْهُمْ ذِكْرَاهُمْ﴿١٨﴾
18. Je, basi wanangojea nini isipokuwa Saa iwafikie ghafla? Na kwa yakini zimekwishakuja ishara zake (Qiyamaah). Basi kutoka wapi kutawafaa kukumbuka kwao itakapowajia (hiyo Saa)?


فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مُتَقَلَّبَكُمْ وَمَثْوَاكُمْ﴿١٩﴾
19. Basi jua kwamba laa ilaaha illa-Allaah (hapana muabudiwa wa haki ila Allaah), na omba maghfirah kwa dhambi zako na kwa ajili ya Waumini wa kiume na Waumini wa kike. Na Allaah Anajua harakati zenu huku na kule na pahala penu pa kupumzikia.


وَيَقُولُ الَّذِينَ آمَنُوا لَوْلَا نُزِّلَتْ سُورَةٌ ۖ فَإِذَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ مُّحْكَمَةٌ وَذُكِرَ فِيهَا الْقِتَالُ ۙ رَأَيْتَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ نَظَرَ الْمَغْشِيِّ عَلَيْهِ مِنَ الْمَوْتِ ۖ فَأَوْلَىٰ لَهُمْ﴿٢٠﴾
20. Na wanasema wale walioami: “Kwa nini isiteremshwe Suwrah?” Inapoteremshwa Suwrah iliyo wazi na ikatajwa humo (amri ya) kupigana vita; utawaona wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi wanakutazama mtazamo wa mwenye kughumiwa na mauti.  Basi ingalikuwa awla kwao (wamtii Allaah).


طَاعَةٌ وَقَوْلٌ مَّعْرُوفٌ ۚ فَإِذَا عَزَمَ الْأَمْرُ فَلَوْ صَدَقُوا اللَّـهَ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ﴿٢١﴾
21. Utiifu na kauli njema. Na likiazimiwa jambo (la kupigana); basi kama wangekuwa wakweli kwa Allaah, bila shaka ingalikuwa kheri kwao.


فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِن تَوَلَّيْتُمْ أَن تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ﴿٢٢﴾
22. Basi huenda nyinyi mkigeuka kwamba mfanye ufisadi katika ardhi na kukata (mawasiliano) jamaa zenu wa uhusiano wa damu?


أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَىٰ أَبْصَارَهُمْ﴿٢٣﴾
23. Hao ndio ambao Allaah Amewalaani; Akawafanya viziwi na Akawapofua macho yao.

أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ أَمْ عَلَىٰ قُلُوبٍ أَقْفَالُهَا﴿٢٤﴾
24. Je, hawaizingatii Qur-aan; au nyoyoni (mwao) mna kufuli?


إِنَّ الَّذِينَ ارْتَدُّوا عَلَىٰ أَدْبَارِهِم مِّن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْهُدَى ۙ الشَّيْطَانُ سَوَّلَ لَهُمْ وَأَمْلَىٰ لَهُمْ﴿٢٥﴾
25. Hakika wale walioritadi kurudi nyuma (ukafirini) baada ya kuwa imeshawabainika Uongofu, shaytwaan amewafanyia wepesi na akawarefushia matumaini ya uongo.


ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لِلَّذِينَ كَرِهُوا مَا نَزَّلَ اللَّـهُ سَنُطِيعُكُمْ فِي بَعْضِ الْأَمْرِ ۖ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ إِسْرَارَهُمْ﴿٢٦﴾
26. Hivyo kwa sababu wao wamewaambia wale waliokirihika yale Aliyoyateremsha Allaah: “Tutakutiini katika baadhi ya mambo.” Na Allaah Anajua kufanya siri kwao.


فَكَيْفَ إِذَا تَوَفَّتْهُمُ الْمَلَائِكَةُ يَضْرِبُونَ وُجُوهَهُمْ وَأَدْبَارَهُمْ﴿٢٧﴾
27. Basi itakuwa vipi pale Malaika watakapowafisha (huku) wakiwapiga nyuso zao na migongo yao?


ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اتَّبَعُوا مَا أَسْخَطَ اللَّـهَ وَكَرِهُوا رِضْوَانَهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ﴿٢٨﴾
28. Hivyo kwa sababu wao wamefuata ambayo yamemghadhibisha Allaah, na wakachukia radhi Zake, basi Akazibatilisha ‘amali zao.


أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ أَن لَّن يُخْرِجَ اللَّـهُ أَضْغَانَهُمْ﴿٢٩﴾
29. Je, wanadhania wale ambao nyoyoni mwao mna maradhi kwamba Allaah ka Hatafichua kamwe mafundo yao (ya chuki)?


وَلَوْ نَشَاءُ لَأَرَيْنَاكَهُمْ فَلَعَرَفْتَهُم بِسِيمَاهُمْ ۚ وَلَتَعْرِفَنَّهُمْ فِي لَحْنِ الْقَوْلِ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ أَعْمَالَكُمْ﴿٣٠﴾
30. Na lau Tungelitaka, Tungelikuonyesha hao, bila shaka ungeliwatambua kwa alama zao dhahiri. Na bila shaka utawatambua kwa lahani ya kauli (zao). Na Allaah Anajua ‘amali zenu.


وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ حَتَّىٰ نَعْلَمَ الْمُجَاهِدِينَ مِنكُمْ وَالصَّابِرِينَ وَنَبْلُوَ أَخْبَارَكُمْ﴿٣١﴾
31. Na bila shaka Tutakujaribuni mpaka Tutambue wenye kufanya jihaad miongoni mwenu na wenye kuvuta subira na tutazitahini habari zenu.


إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَشَاقُّوا الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْهُدَىٰ لَن يَضُرُّوا اللَّـهَ شَيْئًا وَسَيُحْبِطُ أَعْمَالَهُمْ﴿٣٢﴾
32. Hakika wale waliokufuru na wakazuia (watu) njia ya Allaah, na wakampinga kwa uadui Rasuli baada ya kuwabainikia Uongofu hawatoweza kumdhuru Allaah kwa kitu chochote na Atazibatilisha ‘amali zao.



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَلَا تُبْطِلُوا أَعْمَالَكُمْ﴿٣٣﴾
33. Enyi mloamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wala msibatilishe ‘amali zenu.


إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ثُمَّ مَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَهُمْ﴿٣٤﴾
34. Hakika wale waliokufuru wakazuia (watu) njia ya Allaah, kisha wakafa (hali) wakiwa ni makafiri, Allaah Hatowaghufuria kamwe.


فَلَا تَهِنُوا وَتَدْعُوا إِلَى السَّلْمِ وَأَنتُمُ الْأَعْلَوْنَ وَاللَّـهُ مَعَكُمْ وَلَن يَتِرَكُمْ أَعْمَالَكُمْ﴿٣٥﴾
35. Basi msinyong’onyee, mkaomba usalama kwani nyinyi ndio mko juu na Allaah Yu pamoja nanyi na Hatapunguza (thawabu za) ‘amali zenu.


إِنَّمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ ۚ وَإِن تُؤْمِنُوا وَتَتَّقُوا يُؤْتِكُمْ أُجُورَكُمْ وَلَا يَسْأَلْكُمْ أَمْوَالَكُمْ﴿٣٦﴾
36. Hakika uhai wa dunia ni mchezo na pumbao. Lakini mkiamini na mkawa na taqwa; (Allaah) Atakupeni ujira wenu na wala Hatokutakeni (mtoe) mali zenu.


إِن يَسْأَلْكُمُوهَا فَيُحْفِكُمْ تَبْخَلُوا وَيُخْرِجْ أَضْغَانَكُمْ﴿٣٧﴾
37. Akikutakeni hayo Akakukazanieni mtafanya ubakhili, na Atatoa vifundo vyenu (vya kukirihika).


هَا أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ تُدْعَوْنَ لِتُنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَمِنكُم مَّن يَبْخَلُ ۖ وَمَن يَبْخَلْ فَإِنَّمَا يَبْخَلُ عَن نَّفْسِهِ ۚ وَاللَّـهُ الْغَنِيُّ وَأَنتُمُ الْفُقَرَاءُ ۚ وَإِن تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُم﴿٣٨﴾
38. Ha! Nyinyi (ndio) hawa; mnaoitwa ili mtoe katika njia ya Allaah, basi miongoni mwenu ambaye anafanya ubakhili; na afanyaye ubakhili, basi hakika hapana ila anafanya ubakhili dhidi ya nafsi yake. Na Allaah ni Al-Ghaniyyu (Mkwasi) nanyi ni mafakiri. Na mkikengeuka Atabadilisha watu ghairi yenu kisha hawatokuwa mfano wenu.




Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com