HADITHI YA 19 MUHIFADHI ALLAAH سبحانه وتعالى ATAKUHIFADHI

الحديث التاسع عشر
" احفظ الله يحفظك"

 عن أبي العَبَّاس عَبْدِ اللهِ بنِ عَبَّاسٍ رَضي اللهُ عنهما قال: كُنْتُ خَلْفَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم يًوْماً، فقال: (( يا غُلامُ، إنِّي أُعَلِّمُكَ كلِماتٍ: احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ تُجاهَك، إذا سأَلْتَ فاسْأَلِ اللهَ، وإذا اسْتَعنْتَ فاسْتَعِنْ باللهِ، واعْلَمْ أنَّ الأُمَّة  لَوِ اجْتَمَعَتْ على أَنْ يَنْفَعُـوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إلا بِشَيْءٍ قدْ كَتَبَهُ اللهُ لَكَ، وإن اجْتَمَعُوا على أن يَضُرَّوكَ بِشيءٍ لَمْ يَضُروكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبهُ اللهُ عَلَيْكَ، رُفِعَتِ الأقْلامُ وَجَفَّتِ الصُّحُفُ ))

  رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ    وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
وَفِي رِوَايَةِ غَيْرِ التِّرْمِذِيِّ:

 (( احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ أَمَامَكَ تَعَرَّفْ إِلى اللهِ فِي الرَّخَاءِ يَعْرِفْكَ فِي الشِّدَّةِ واعْلَمْ أَنَ مَا أَخْطَأَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُصِيبَكَ وَما أَصَابَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُخْطِئَكَ وَاعْلَمْ أنَ النَّصْرَ مَعَ الصَّبْرِ وَأَنَّ الفَرَجَ مَعَ الكَرْبِ وَ أَنَّ مَعَ العُسْرِ يُسْرَاً ))

HADITHI YA 19
MUHIFADHI ALLAAH سبحانه وتعالى ATAKUHIFADHI
Kutoka kwa Abul ‘Abbaas Abdullah Ibn ‘Abbaas رضي الله عنهما  ambaye alisema:
Siku moja nilikuwa nyuma ya Mtume صلى الله عليه وسلم akaniambia: Kijana nitakufundisha maneno (ya kufaa); Mhifadhi Allaah سبحانه وتعالى (fuata maamrisho Yake na chunga Mipaka Yake) Atakuhifadhi.  Muhifadhi Allaah سبحانه وتعالى na utamkuta mbele yako.  Ukiomba, muombe Allaah سبحانه وتعالى, ukitafuta msaada tafuta kwa Allaah سبحانه وتعالى.  (lazima) ujue kuwa ikiwa taifa zima litaungana kukunufaisha wewe kwa kitu, basi hutonufaika ila tu kwa kile alichokwishakuandikia Allaah سبحانه وتعالى na wakikusanyika kukudhuru kwa chochote, hotodhurika ila tu kwa kile Allaah سبحانه وتعالى alichokwishakuandikia (kuwa kitakudhuru) .  Kwani Kalamu zimeshanyanyuliwa (kila kitu kishaandikwa) na sahifa zimeshakauka (Hakuna kupangwa tena wala kupanguliwa).
 Imesimuliwa na At-Tirmidhi akasema kuwa ni hadithi Hasan Sahihi.
Na kwa mapokezi mengine yasiyokuwa ya At-Tirmidhi inasema:
Muhifadhi Allaah سبحانه وتعالى utakuta katangulia mbele yako (kwa ulinzi Wake, himaya na msaada Wake).  Mjue Mola wako katika   neema (muombe, mche, mtii) Atakujua katika shida (unapokuwa katika dhiki Naye Atakusaidia). Jua kuwa yaliyokukosa hayakuwa        yakupate na yaliokupata hayakuwa yakukose.  Jua kuwa ushindi uko pamoja na subira, na faraja iko pamoja na dhiki, na raha iko pamoja na shida (haviachani).