Hadithi Ya 28: Nakuusieni Kumcha Allaah Na Tabia Njema



الحديث الثامن والعشرون



"أوصيكم بتقوى الله وحسن الخلق"


عن أبي نَجيحٍ الْعِرْباضِ بنِ سارِيَةَ رضي اللهِ عنه قال: وَعَظَنَا رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم مَوْعِظَةً وَجِلَتْ مِنها الْقُلُوبُ، وذَرَفَتْ منها الْعُيُونُ، فَقُلْنا: يا رسول اللهِ، كأَنَّهَا مَوْعِظَةُ مُوَدِّعٍ، فأَوْصِنا. قال:
((أُوصِيكُمْ بِتَقْوَى اللهِ عَزَّ وَجَلَّ، والسَّمْعِ والطَّاعَةِ، وإن تَأَمَّرَ عَلَيْكُمْ عَبْدٌ، فإنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيَرَى اخْتِلافاً كَثِيراً، فَعَليْكُمْ بِسُنَّتي وسُنَّةِ الخُلفَاءِ الرَّاشِدِينَ المَهْدِيِّينَ، عَضُّوا عَلَيْها بالنَّواجِذِ، وإيَّاكُمْ ومُحْدَثاتِ الأُمُورِ، فإنَّ كلَّ مُحْدَثَةٍ  بِدْعَةٌ وَ كُلَّ  بِدْعَةٍ ضَلاَلَةٌ  وَكُلَّ ضَلاَلَةٍ فِي النَّارِ))  
رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ. 
 
HADITHI YA. 28
NAKUUSIENI KUMCHA ALLAAH NA TABIA NJEMA
Kutoka kwa Abu Najiih Al 'Irbaadh Ibn Saariyah رضي الله عنه  ambaye alisema kwamba:
Mtume صلى الله عليه وسلم alituhutubia hutuba ambayo nyoyo zetu zilijaa hofu na macho yetu yalitutoka machozi.  Tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu!, inaonyesha kama kwamba hii ni hutuba  ya kuaga, kwa hivyo tuusie.  Akasema (Mtume صلى الله عليه وسلم  )  nakuusieni kumcha Allaah سبحانه وتعالى  na kumtii kiongozi wenu hata akiwa mtumwa.  Yule atakayeishi (muda mrefu) ataona ikhtilaaf nyingi (migongano), kwa hivyo fuateni mwendo wangu (Sunnah) na mwendo wa Makhalifa walioongoka (Makhalifa wanne). Shikamaneni nazo kwa magego (kwa nguvu).  Na tahadharini na mambo mapya yanayozuliwa kwani kila jambo jipya ni uzushi, na kila uzushi ni upotofu, na  kila upotofu unapeleka motoni.

Imesimuliwa na Abu Dawuud na At Tirmidhi na wamesema ni Hadithi Hasan na Sahihi.