Abasa (80)


سُورَةُ  عَبَسَ
‘Abasa (80)

(Imeteremka Makka)

Sura hii imeanza kwa kumlaumu Nabii Muhammad s.a.w. kwa kumpuuza Ibnu Ummi Maktoum alipo mjia kutafuta ilimu na uwongofu. Naye Nabii s.a.w. alikuwa kashughulika kuwalingania Dini baadhi ya mabwana wa Kikureshi kwa kutaraji watamwitikia, ili kwa kusilimu kwao wange silimu watu wengi. Kisha Sura inamkumbusha binaadamu kwa neema alizo pewa na Mwenyezi Mungu tangu kuumbwa kwake mpaka kufufuliwa kwake. Na ikakhitimisha kwa kusimulia khabari za Siku ya Kiyama, ikibainisha kwamba watu siku hiyo ni makundi mawili, kundi la Waumini lenye furaha, na kundi la makafiri wapotovu.


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١﴾

1. Alikunja kipaji na akageuka.

أَن جَاءَهُ الْأَعْمَىٰ ﴿٢﴾

2. Alipomjia kipofu.

وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّىٰ ﴿٣﴾

3. Na nini kitakachokujulisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) huenda akatakasika?

أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ الذِّكْرَىٰ ﴿٤﴾

4. Au atakumbuka, umfae ukumbusho (mawaidha).

أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَىٰ ﴿٥﴾

5. Ama yule ajionaye amejitosheleza (hana haja ya Uislamu).

فَأَنتَ لَهُ تَصَدَّىٰ ﴿٦﴾

6. Nawe unamshughulikia.

وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ ﴿٧﴾

7. Na si juu yako asipotakasika.

وَأَمَّا مَن جَاءَكَ يَسْعَىٰ ﴿٨﴾

8. Ama yule aliyekujia kwa kukimbilia.

وَهُوَ يَخْشَىٰ ﴿٩﴾

9. Naye anakhofu.

فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ ﴿١٠﴾

10. Basi wewe humshughulikii.

كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ ﴿١١﴾

11. Sivyo katu! Hakika hiyo ni tadhkirah (ukumbusho).

فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ ﴿١٢﴾

12. Basi atakaye ataikumbuka.

فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ ﴿١٣﴾

13. (Zimeandikwa) Katika swahifa zilizokirimiwa.

مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ ﴿١٤﴾

14. Zimetukuzwa na zimetwaharishwa.

بِأَيْدِي سَفَرَةٍ ﴿١٥﴾

15. (Zinazobebwa) Katika mikono ya (Malaika) waandishi.

كِرَامٍ بَرَرَةٍ ﴿١٦﴾

16. Watukufu (na) watiifu.

قُتِلَ الْإِنسَانُ مَا أَكْفَرَهُ ﴿١٧﴾

17. Ameangamia insani namna gani anavyokufuru?

مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ ﴿١٨﴾

18. Kutoka kitu gani (Allaah) Amemuumba?

مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُ فَقَدَّرَهُ ﴿١٩﴾

19. Kutoka tone la manii, Amemuumba, Akamkadiria.

ثُمَّ السَّبِيلَ يَسَّرَهُ ﴿٢٠﴾
20. Kisha Akamuwepesishia njia.

ثُمَّ أَمَاتَهُ فَأَقْبَرَهُ ﴿٢١﴾

21. Kisha Akamfisha, na Akamfanyia kaburi.

ثُمَّ إِذَا شَاءَ أَنشَرَهُ ﴿٢٢﴾

22. Kisha Atakapotaka, Atamfufua.

كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَا أَمَرَهُ ﴿٢٣﴾

23. Sivyo katu! Hakutimiza Aliyomuamuru (Muumba wake).

فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ إِلَىٰ طَعَامِهِ ﴿٢٤﴾

24. Basi atazame insani chakula chake.

أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاءَ صَبًّا ﴿٢٥﴾

25. Kwamba Sisi Tumemimina maji kwa mmimino.

ثُمَّ شَقَقْنَا الْأَرْضَ شَقًّا ﴿٢٦﴾

26. Kisha Tukaipasua ardhi mpasuo.

فَأَنبَتْنَا فِيهَا حَبًّا ﴿٢٧﴾

27. Tukaotesha humo nafaka.

وَعِنَبًا وَقَضْبًا ﴿٢٨﴾
28. Na mizabibu na (mimea ya) mboga.

وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا ﴿٢٩﴾

29. Na mizaituni na mitende.

وَحَدَائِقَ غُلْبًا ﴿٣٠﴾

30. Na mabustani yaliyosongamana.

وَفَاكِهَةً وَأَبًّا ﴿٣١﴾

31. Na matunda na (majani ya) malisho (ya wanyama).

مَّتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ ﴿٣٢﴾

32. (Kuwa ni) Manufaa kwenu na kwa wanyama wenu wa mifugo.

فَإِذَا جَاءَتِ الصَّاخَّةُ ﴿٣٣﴾

33. Basi itakapokuja Asw-Swaakhkhah (ukelele mkali wa kugofya wa baragumu).

يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ ﴿٣٤﴾

34. Siku mtu atakapomkimbia ndugu yake.

وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ ﴿٣٥﴾

35. Na (na pia atakapomkimbia) mama yake na baba yake.

وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ ﴿٣٦﴾

36. Na mkewe na wanawe.

لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ ﴿٣٧﴾

37. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na hali ya kumtosheleza.

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌ ﴿٣٨﴾

38. (Baadhi ya) Nyuso siku hiyo zitanawiri.

ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌ ﴿٣٩﴾

39. Zikicheka na kufurahi.

وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ ﴿٤٠﴾

40. Na (baadhi ya) nyuso siku hiyo zitakuwa na vumbi juu yake.

تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ ﴿٤١﴾

41. Zitafunikwa na giza totoro.

أُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَفَرَةُ الْفَجَرَةُ ﴿٤٢﴾

42. Hao ndio makafiri waovu.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com