Hadiyth Ya 11 Watu Wa Mwanzo Kuulizwa Qiyaamah: Shahidi, ‘Aalim Na Mtoaji Mali

Hadiyth Ya 11

Watu Wa Mwanzo Kuulizwa Qiyaamah: Shahidi, ‘Aalim Na Mtoaji Mali

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: (( إِنَّ أَوَّلَ النَّاسِ يُقْضَى يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَيْهِ رَجُلٌ اسْتُشْهِدَ فَأُتِيَ بِهِ فَعَرَّفَهُ نِعَمَهُ فَعَرَفَهَا قَالَ فَمَا عَمِلْتَ فِيهَا قَالَ قَاتَلْتُ فِيكَ حَتَّى اسْتُشْهِدْتُ قَالَ كَذَبْتَ وَلَكِنَّكَ قَاتَلْتَ لِأَنْ يُقَالَ جَرِيءٌ فَقَدْ قِيلَ ثُمَّ أُمِرَ بِهِ فَسُحِبَ عَلَى وَجْهِهِ حَتَّى أُلْقِيَ فِي النَّارِ . وَرَجُلٌ تَعَلَّمَ الْعِلْمَ وَعَلَّمَهُ وَقَرَأَ الْقُرْآنَ فَأُتِيَ بِهِ فَعَرَّفَهُ نِعَمَهُ فَعَرَفَهَا قَالَ فَمَا عَمِلْتَ فِيهَا قَالَ تَعَلَّمْتُ الْعِلْمَ وَعَلَّمْتُهُ وَقَرَأْتُ فِيكَ الْقُرْآنَ قَالَ كَذَبْتَ وَلَكِنَّكَ تَعَلَّمْتَ الْعِلْمَ لِيُقَالَ عَالِمٌ وَقَرَأْتَ الْقُرْآنَ لِيُقَالَ هُوَ قَارِئٌ فَقَدْ قِيلَ ثُمَّ أُمِرَ بِهِ فَسُحِبَ عَلَى وَجْهِهِ حَتَّى أُلْقِيَ فِي النَّارِ. وَرَجُلٌ وَسَّعَ اللَّهُ عَلَيْهِ وَأَعْطَاهُ مِنْ أَصْنَافِ الْمَالِ كُلِّهِ فَأُتِيَ بِهِ فَعَرَّفَهُ نِعَمَهُ فَعَرَفَهَا قَالَ فَمَا عَمِلْتَ فِيهَا قَالَ مَا تَرَكْتُ مِنْ سَبِيلٍ تُحِبُّ أَنْ يُنْفَقَ فِيهَا إِلَّا أَنْفَقْتُ فِيهَا لَكَ قَالَ كَذَبْتَ وَلَكِنَّكَ فَعَلْتَ لِيُقَالَ هُوَ جَوَادٌ فَقَدْ قِيلَ ثُمَّ أُمِرَ بِهِ فَسُحِبَ عَلَى وَجْهِهِ ثُمَّ أُلْقِيَ فِي النَّارِ)) مسلم و الترمذي والنسائي

Kutoka kwa Abu Hurayrahرضي الله عنه    ambaye alisema: Nilimsikia Mjumbe wa Allaah صلى الله عليه وسلم akisema: ((Mtu wa kwanza atakayehukumiwa siku ya Qiyaamah ni mtu aliyekufa shahidi. Ataletwa na Allaah Atamjulisha neema Zake kwake na atazifahamu. (Mola) Atasema: Je, ulizitumia vipi? Atasema (yule mtu): Nilipigana kwa ajili Yako mpaka nikafa shahidi. (Mola) Atasema: Umesema uongo, ulipigana ili uambiwe shujaa. Na kwa hivyo ukaambiwa (shujaa). Hapo itaamriwa abururwe kifudifudi mpaka atiwe motoni. Mtu mwengine aliyesoma dini na kuisomesha na ambaye akisoma Qur-aan ataletwa na Allaah, Atamfahamisha neema Zake (kwake) na atazikumbuka. (Allaah) Atasema: Umezifanyia nini? Atajibu: Nilisoma dini na nikaisomesha. Nilisoma Qur-aan kwa ajili Yako. (Mola) Atasema: Umesema uongo, ulisoma dini ili uambiwe ni mwanachuoni ('Aalim) ulisoma Qur-aan ili uambiwe kuwa ni msomaji (Qaari mzuri). Na kwa hivyo uliambiwa. Tena itaamrishwa abururwe kifudifudi mpaka motoni. Mtu mwengine ni ambaye Allaah Alimkirimu utajiri na ambaye Alimpa kila namna ya mali. Ataletwa na Allaah Atamtajia neema Zake (kwake) na atazitambua. (Mola) Atasema: Na ulizifanyia nini?  Atasema: Sikuacha chochote kile Ulichotaka pesa zitumiwe kwa ajili Yako nilitumia kwa ajili Yako. (Mola) Atasema: Umesema uongo. Ulitumia ili uambiwe (usifiwe) kuwa ni karimu. Na kwa hivyo ukaambiwa. Tena itaamrishwa abururwe kifudifudi mpaka motoni)) [Muslim na At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy].