At-Takaathur (102)


سُورَةُ  التَّكَاثُر
At-Takaathur (102)

(Imeteremka Makka)


 

Sura hii inawaibisha wale ambao kushindania wingi kumewashughulisha na kutimiza yaliyo ya waajibu. Na inawaonya kwamba hakika watakuja jua mwisho wa taksiri yao hiyo, na inawakhofisha watu kuwa watakuja uona Moto na watakuja ulizwa neema walizo kuwa nazo.

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُرُ ﴿١﴾

1. Kumekughafilisheni (kushindana) kukithiri (anasa na mapato ya dunia)

حَتَّىٰ زُرْتُمُ الْمَقَابِرَ ﴿٢﴾

2. Mpaka mkazuru (mkaingia) makaburini.

كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٣﴾

3. Hapana! Mtakuja kujua.

ثُمَّ كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٤﴾

4. Kisha Hapana! Mtakuja kujua.


كَلَّا لَوْ تَعْلَمُونَ عِلْمَ الْيَقِينِ ﴿٥﴾

5. Hapana! Lau mngelijua ujuzi wa yakini.

لَتَرَوُنَّ الْجَحِيمَ ﴿٦﴾

6. Bila shaka mngeuona (Moto wa) Al-Jahiym.

ثُمَّ لَتَرَوُنَّهَا عَيْنَ الْيَقِينِ ﴿٧﴾

7. Kisha kwa hakika mtauona (huo Moto wa Al-Jahiym) kwa jicho la yakini.

ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ ﴿٨﴾

8. Kisha bila shaka mtaulizwa siku hiyo kuhusu (kila) neema (mmezitumiaje duniani?).





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com