Hadiyth Ya 16 - Kitu Cha Kwanza Kinachohesabiwa Katika ‘Amali Za Mja Ni Swalah



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ َقَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ ((إِنَّ أَوَّلَ مَا يُحَاسَبُ بِهِ الْعَبْدُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنْ عَمَلِهِ صَلاتُهُ فَإِنْ صَلُحَتْ فَقَدْ أَفْلَحَ وَأَنْجَحَ وَإِنْ فَسَدَتْ فَقَدْ خَابَ وَخَسِرَ فَإِنْ انْتَقَصَ مِنْ فَرِيضَتِهِ شَيْءٌ قَالَ الرَّبُّ عَزَّ وَجَلَّ انْظُرُوا هَلْ لِعَبْدِي مِنْ تَطَوُّعٍ فَيُكَمَّلَ بِهَا مَا انْتَقَصَ مِنْ الْفَرِيضَةِ ثُمَّ يَكُونُ سَائِرُ عَمَلِهِ عَلَى ذَلِكَ)) الترمذي و أبوا داود والنسائي وابن ماجه وأحمد


Imepokelewa na Abu Hurayrahرضي الله عنه  ambaye alisema kwamba: Mjumbe wa Allaah صلى الله عليه وسلم alisema ((Kitu cha kwanza kinachohesabiwa katika ‘amali za mja wa Allaah siku ya Qiyaamah ni Swalah zake. Zikiwa zimetimia, hapo tena atakuwa kaneemeka na kafuzu, na zikiwa zina kasoro atakuwa kaanguka na kala khasara. Ikiwa pana upungufu katika Swalah zake za fardhi Allaah عَزَّ وَجَلَّ Atasema: Angalia ikiwa mja wangu ana Swalah zozote za Sunnah ambazo zinaweza kufidia zile zilizopungua, hapo tena amali yake iliyobaki itaangaliwa hivyo hivyo)) [At-Tirmidhiy, Abu Daawuud, An-Nasaaiy, Ibn Maajah na Ahmad]