Al-Maa’uwn (107)

سُورَةُ  الْمَاعُونAl-Maa’uwn (107)

(Imeteremka Makka)


 
Sura hii inahadithia khabari za mwenye kukadhibisha malipo ya Akhera. Ikataja katika sifa zake kuwa yeye anamdhalilisha yatima, na anamkemea kwa ukali, si kwa kumtengeza. Na kwamba yeye hamhimizi mtu yeyote, la kwa kauli wala kwa kitendo, kuwalisha masikini; kwa sababu huyo ni mchoyo kwa mali yake, bakhili kwa alicho nacho mkononi. Kisha Sura imewataja watu wa kikundi kingine wanao shabihiana na hawa wanao kadhibisha malipo. Hawa ni wale wanao ghafilika na Sala zao, ambao hawasali kama itakikanavyo, na ambao husimama kwa hayo kwa dhaahiri tu si kwa hakika. Ni wenye kuonyesha tu a'mali zao, wenye kuzuia msaada wao wasiwape wanao hitajia. Na Sura inawaahidi hao kuwa watapata misiba na maangamio, ili waache uasi wao.

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

أَرَأَيْتَ الَّذِي يُكَذِّبُ بِالدِّينِ ﴿١﴾

1. Je, umemuona yule anayekadhibisha Malipo?

فَذَٰلِكَ الَّذِي يَدُعُّ الْيَتِيمَ ﴿٢﴾

2. Basi huyo ndiye anayemsukuma yatima.

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ ﴿٣﴾

3. Na wala hahamasishi kulisha maskini.

فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ ﴿٤﴾

4. Basi Ole kwa wanaoswali.

الَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ ﴿٥﴾

5. Ambao wanapuuza Swalaah zao.

الَّذِينَ هُمْ يُرَاءُونَ ﴿٦﴾

6. Ambao wanajionyesha.

وَيَمْنَعُونَ الْمَاعُونَ ﴿٧﴾

7. Na wanazuia misaada ya matumizi ya kawaida.



سُورَةُ  الْكَوْثَر
Al-Kawthar (108)
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ ﴿١﴾

1. Hakika Sisi Tumekupa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Al-Kawthar (mto katika Jannah).

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ ﴿٢﴾

2. Basi swali kwa ajili ya Rabb (Mola) wako na chinja (kwa ajili Yake).

إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الْأَبْتَرُ ﴿٣﴾

3. Hakika (adui yako) anayekuchukia yeye ndiye atakayekatiliwa mbali (kizazi na kila kheri).





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com