الحديث الثاني
والأربعون
"يا ابن آدم إنك ما
دعوتني ورجوتني"
عن أنس رضي الله عنه قَالَ:
سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وآله
وسلم
يَقُولُ: ((قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ مَا
دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ مِنْكَ وَلاَ أُبَالِي.
يَا ابْنَ آدَمَ لَوْ بَلَغَتْ ذُنُوبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ ثُمَّ
اسْتَغْفَرْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ . يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ لَوْ أَتَيْتَنِي
بِقُرَابِ الأَرْضِ خَطَايَا ثُمَّ لَقِيتَنِي لاَ تُشْرِكُ بِي شَيْئًا
لاَتَيْتُكَ بِقُرَابِهَا مَغْفِرَةً))
رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ:
حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
HADITHI
YA 42
EWE MWANA WA ADAM,
UTAKAPONIOMBA NA KUWEKA MATUMAINI
KWANGU BASI NITAKUSAMEHE
Kutoka kwa Anas رضي الله عنه ambaye
alisema : Nilimsikia Mtume صلى الله عليه وسلم
akisema :
Mwenyeezi Mungu amesema : Ewe Mwana wa Adam utakaponiomba na
kuweka matumaini kwangu, basi nitakusamehe makosa uliyoyafanya na
sitojali. Ewe Mwana wa Adam kama dhambi zako zingefika mawingu ya mbingu na
wewe ukaomba msamaha kwangu, ningekusamehe. Ewe Mwana Wa Adam kama
ungelinijia na dhambi kubwa kama dunia na ukanikabili bila ya kunishirikisha
nitakupa maghfira.
Imesimuliwa na Tirmidhi na asema ni hadithi Hasan Sahihi