Hadiyth Ya 34
 Mwenye Kufurahi Na Kuchukia Kukutana Na Allaah



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:  ((قَالَ اللَّهُ إِذَا أَحَبَّ عَبْدِي لِقَائِي أَحْبَبْتُ لِقَاءَهُ وَإِذَا كَرِهَ لِقَائِي كَرِهْتُ لِقَاءَهُ))
البخاري و مالك

Kutoka kwa Abu Hurayrahرضي الله عنه  ambaye amesema kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: ((Allaah سبحانه وتعالى Amesema: Mja wangu akipenda kukutana na Mimi, Nami hupenda kukutana naye; na akiwa hapendi kukutana na Mimi, basi nami sipendi kukutana naye)) [Al-Bukhaariy na Maalik]