Ni Wajibu kwa Mwanamke Kusali Ijumaa?
JAWABU
Sala
ya Ijumaa si wajibu kwa mwanamke kwa mujbu wa makubaliano (ijmaa) ya maulamaa
na kwa dalili ifuatayo:
حديث
طارق بن شهاب رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال :
الجُمُعَةُ حَقٌّ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُسلِمٍ فِي جَمَاعَةٍ إِلاَّ أَربَعَة :
عَبدٌ مَملُوكٌ ، أَو امرَأَةٌ ، أَو صَبِيٌّ ، أَو مَرِيضٌ
رواه
أبو داود) وقال النووي في "المجموع") : إسناده صحيح على شرط الشيخين ، ،
وصححه الألباني في صحيح الجامع.
Hadithi ya Twaariq ibn Shihaab
Allah amuwie radhi : Kwamba Mtume (Salla llahu ’Alayhi Wasallam) amesema:
“ (Sala ya) Ijumaa ni haki
iliyo wajibu kwa kila muislamu kwa (kusaliwa) jamaa isipokuwa watu wane.
Mtumwa, au mwanamke au mtoto au mgonjwa.”
Imesimuliwa na Abu Daaud na anasema
Imamu Nnawawiy katika Al Majmuu kwamba Isnaad ( mlolongo wa wapokezi)
yake ni sahihi kwa sharti ya mashekhe wawili (Bukhari na Muslim) na anasema Sh.
Albaani ni sahihi katika Sahihul Jaami’i
Hii ndiyo hukmu ya kisheria. Na kama
wanawake watasali Ijumaa basi pia sala yao ni sahihi ikiwa mwanamke atazingatia
na kutimiza masharti yaliyowekwa kuweza kwenda msikitini na kusali. Miongoni
mwao ni kutojipamba ,
Anasema Ibnu Qudaamah katika Al
Mughni :
ولكنها تصح منها - أي الجمعة - ؛
لصحة الجماعة منها ، فإن النساء
كن يصلين صلى الله عليه وسلم في الجماعة
“Lakini sala yao inasihi
(yaani ijumaa) kwa sababu ya kusihi sala yao ya jamaa kwani wanawake walikuwa
wakisali na Mtume (Salla Llahu ’Alayhi Wasallam) jamaa”.
Na pia kwa sababu sala ya ijumaa
imefaradhiswa kuweza kukusanyika waislamu na kusikiliza khutba na kunufaika
nayo na kusali pamoja.
Hata hivyo ni bora kwa mwanamke
kusali adhuhuri nyumbani badala ya Ijumaa kwa mujibu wa hadithi maarufu ya
Mtume (Salla Llahu ’Alayhi Wasallam)
( لا تمنعوا نساءكم المساجد ، وبيوتهن خير لهن )
داود وصححه الألباني في
صحيح أبي داود رواه أبو
“Msiwakataze wanawake zenu
(kuhudhuria) misikitini na (wakisali) majumbani kwao ni kheri kwao.”
Imesimuliwa na Abu
Daaud na ameisahihisha Sh. Albaani katika Sahihi Abu Daaud.