Hadithi Ya 06: Hakika Halali Iko Wazi Na Haramu Iko Wazi

الحديث السادس
"إن الحلال بين وإن الحرام بين"

عَنْ أبي عَبْدِ اللهِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُما قَالَ : سمعتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: 
(( إن الْحَلالَ بَيِّنٌ وَإنَّ الْحَرَامَ بَيِّنٌ وَبَيْنَهُما أمورٌ مُشْتَبِهَاتٌ لا يَعْلَمُهُنَّ كَثيِرٌ مِنَ الناسِ، فَمَنِ اتَّقَى الشُّبُهَاتِ فَقَد اسْتَبْرَأَ لِدِينِهِ وَعِرْضِهِ، وَمَنْ وَقَعَ في الشَّبُهاتِ وَقَعَ في الْحَرَامِ، كالرَّاعِي يَرْعَى حَوْلَ الْحِمَى يُوشِكُ أَنْ يَرْتَعَ فِيهِ، أَلا وَإنَّ لِكُلِّ مَلِكٍ حِمىً أَلا وَإنَّ حِمَى الله مَحَارِمُه، أَلا وَإنَّ في الجَسَدِ مُضْغَةً إذَا صَلَحَتْ صَلَحَ الْجَسَدُ كُلُّهُ وإذَا فَسَدَتْ فَسَدَ الْجَسَدُ كُلُّهُ، أَلا وَهِيَ الْقَلْبُ))

 رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ  وَمُسْلِمٌ

HADITHI YA 6
HAKIKA HALALI IKO WAZI NA HARAMU IKO WAZI

Kutoka kwa  Abu Abdullah An-Nu’uman Ibn Bashiyr  رضي الله عنه  ambaye alisema: Nilimsikia Mtume صلى الله عليه وسلم  akisema:
Halali iko wazi na haramu iko wazi, baina yao ni vitu vyenye shaka ambavyo watu wengi hawajui.   Kwa hivyo, yule anayeepuka vyenye shaka  anajisafisha nafsi yake kwenye dini yake na heshima yake, lakini yule anayetumbukia katika mambo yenye shaka, huanguka katika haramu, kama mchunga anayechunga pembezoni mwa mpaka, mara  huingia ndani (ya shamba la mtu).  Hakika kila mfalme ana mipaka yake, na mipaka ya Allaah سبحانه وتعالى  ni makatazo Yake. Na hakika katika kiwiliwili kuna kipande cha nyama kikitangamaa, kiwiliwili chote kitakua kizima, kikharibika kiwiliwili chote huharibika. Basi jua (kipande hicho cha nyama) ni moyo.
Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim