Atw-Twuwr (52)


سُورَةُ  الطُّور
Atw-Twuwr (52)

(Imeteremka Makka)


Sura hii imeanza kwa kiapo cha watano katika bora wa viumbe kuwa adhabu itawateremkia hao wanao kanusha. Kisha ikafikia kusimulia kuwateremkia hiyo adhabu, na namna zake mbali mbali siku ya kufufuliwa na kulipwa. Na ikaingia kutaja mazungumzo juu ya neema za wachamngu na watakayo stareheshwa nayo katika Mabustani ya milele, na namna ya ukarimu watakao upata, na kisha yatakavyo tua macho yao kwa kuwa dhuriya zao watavyo wafuata, na kunyanyuliwa vyeo vyao wawafikie wao. Na baada ya hayo Sura inamuamrisha Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w. adumishe kukumbusha bila ya kujali wanayo mzulia makafiri kumpinga yeye, au kushughulika na wayasemayo juu ya Qur'ani tukufu, kwa vile inavyo onyesha kuwa wameshindwa kuleta maneno mfano wa Qur'ani.
Sura hii pia imekashifu maoni yao makafiri ya ufisadi ya kutangaza upotovu wao, na uovu wa kupima kwao. Kisha ikakhitimishia kwa kumuelekea Nabii s.a.w. na kumwambia awaachilie mbali mpaka watakapo ikuta siku yao watapo situshwa, naye akaamrishwa aistahamilie hukumu ya Mola wake Mlezi ya kuwapa muhula hao, kwani hayo hayatamdhuru kitu yeye kwa sababu yumo katika uhifadhi wa Mola wake Mlezi na ulinzi wake. Kadhaalika imemtaka amtakase Mwenyezi Mungu na katika nyakati zote, na katika kila msimamo atakao kuwamo kwa jambo lolote, na usiku zinapo tua nyota.

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

وَالطُّورِ ﴿١﴾

1. Naapa kwa (mlima wa) Twuwr.

وَكِتَابٍ مَّسْطُورٍ ﴿٢﴾
2. Na (Naapa kwa) Kitabu kilichoandikwa.

فِي رَقٍّ مَّنشُورٍ ﴿٣﴾

3. Katika (karatasi) ya ngozi iliyokunjuliwa.

وَالْبَيْتِ الْمَعْمُورِ ﴿٤﴾

4. Na (Naapa kwa) Nyumba inayozuriwa (na Malaika kwenye mbingu ya saba).

وَالسَّقْفِ الْمَرْفُوعِ ﴿٥﴾

5. Na (Naapa kwa) sakafu (za mbingu) zilizonyanyuliwa.

وَالْبَحْرِ الْمَسْجُورِ ﴿٦﴾

6. Na (Naapa kwa) bahari zilizojazwa (zitakazowashwa moto Siku ya Qiyaamah).

إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ لَوَاقِعٌ ﴿٧﴾

7. Hakika adhabu ya Rabb (Mola) wako bila shaka itatokea.

مَّا لَهُ مِن دَافِعٍ ﴿٨﴾

8. Hakuna wa kuizuia.

يَوْمَ تَمُورُ السَّمَاءُ مَوْرًا ﴿٩﴾

9. Siku zitakapotikisika mbingu mtikiso (mkubwa).

وَتَسِيرُ الْجِبَالُ سَيْرًا ﴿١٠﴾

10. Na majabali yatakwenda mwendo (mkubwa).

فَوَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿١١﴾

11. Basi ole Siku hiyo kwa wakadhibishao.

الَّذِينَ هُمْ فِي خَوْضٍ يَلْعَبُونَ ﴿١٢﴾

12. Ambao kwenye upuuzi wanatumbukia kucheza.

يَوْمَ يُدَعُّونَ إِلَىٰ نَارِ جَهَنَّمَ دَعًّا ﴿١٣﴾

13. Siku watakayosukumwa katika Moto wa Jahannam msukumo.

هَـٰذِهِ النَّارُ الَّتِي كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ ﴿١٤﴾

14. (Wataambiwa): “Huu ndio ule Moto ambao mlikuwa mkiukadhibisha.

أَفَسِحْرٌ هَـٰذَا أَمْ أَنتُمْ لَا تُبْصِرُونَ ﴿١٥﴾

15. “Je, hii ni sihiri au nyinyi hamuoni?

اصْلَوْهَا فَاصْبِرُوا أَوْ لَا تَصْبِرُوا سَوَاءٌ عَلَيْكُمْ ۖ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٦﴾

16. “Ingieni muungue humo, msubiri au msisubiri, ni sawasawa kwenu, hakika mnalipwa yale mliyokuwa mkiyatenda.”

إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَنَعِيمٍ ﴿١٧﴾

17. Hakika wenye taqwa watakuwa katika Jannaat za Na’iym.

فَاكِهِينَ بِمَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ وَوَقَاهُمْ رَبُّهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ ﴿١٨﴾

18. Wakifurahika kwa Aliyowapa Rabb (Mola) wao, na Akawakinga na adhabu ya (Moto wa) Al-Jahiym.

كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٩﴾

19. (Wataambiwa): “Kuleni na kunyweni kwa raha kwa yale mliyokuwa mnayatenda.”

مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ سُرُرٍ مَّصْفُوفَةٍ ۖ وَزَوَّجْنَاهُم بِحُورٍ عِينٍ ﴿٢٠﴾

20. Mkiegemea juu ya makochi ya fakhari yaliyopangwa safusafu, na Tutawaozesha huwrin-’iyn (wanawake wa Jannah wenye macho makubwa na mazuri).

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَاتَّبَعَتْهُمْ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَانٍ أَلْحَقْنَا بِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَمَا أَلَتْنَاهُم مِّنْ عَمَلِهِم مِّن شَيْءٍ ۚ كُلُّ امْرِئٍ بِمَا كَسَبَ رَهِينٌ ﴿٢١﴾

21. Na wale walioamini na wakafuatwa na dhuriya wao kwa iymaan, Tutawakutanisha nao dhuriya wao na Hatutawapunguzia katika ‘amali zao kitu chochote. Kila mtu atawekewa rehani kwa yale aliyoyachuma (alipwe).

وَأَمْدَدْنَاهُم بِفَاكِهَةٍ وَلَحْمٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ ﴿٢٢﴾

22. Na Tutawapa matunda (ya kila aina) na nyama watakazozitamani.

يَتَنَازَعُونَ فِيهَا كَأْسًا لَّا لَغْوٌ فِيهَا وَلَا تَأْثِيمٌ ﴿٢٣﴾

23. Watabadilishana humo gilasi (zenye mvinyo) visivyo (sababisha) maneno ya upuuzi na wala ya dhambi.

وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ غِلْمَانٌ لَّهُمْ كَأَنَّهُمْ لُؤْلُؤٌ مَّكْنُونٌ ﴿٢٤﴾

24. Na watawazungukia (watumishi) vijana (khaswa kwa ajili yao) kama kwamba ni lulu zilizohifadhiwa.

وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٢٥﴾

25. Na watakabiliana baadhi yao kwa wengineo wakiulizana.

قَالُوا إِنَّا كُنَّا قَبْلُ فِي أَهْلِنَا مُشْفِقِينَ ﴿٢٦﴾

26. Watasema: “Hakika sisi tulikuwa kabla kwenye ahli zetu Tukiogopa.

فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْنَا وَوَقَانَا عَذَابَ السَّمُومِ ﴿٢٧﴾

27. “Basi Allaah Akatufanyia ihsani, na Akatukinga na adhabu (ya Moto) unaobabua.

إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلُ نَدْعُوهُ ۖ إِنَّهُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ ﴿٢٨﴾

28. “Hakika sisi tulikuwa kabla Tunamuomba (Yeye Pekee), hakika yeye Ndiye Al-Barrur-Rahiym (Mwingi wa ihsani na kheri - Mwenye kurehemu).”

فَذَكِّرْ فَمَا أَنتَ بِنِعْمَتِ رَبِّكَ بِكَاهِنٍ وَلَا مَجْنُونٍ ﴿٢٩﴾

29. Basi kumbusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwani hakika wewe kwa neema ya Rabb (Mola) wako, si kuhani na wala si majnuni.

أَمْ يَقُولُونَ شَاعِرٌ نَّتَرَبَّصُ بِهِ رَيْبَ الْمَنُونِ ﴿٣٠﴾

30. Au wanasema (huyu Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم ni) mshairi, tunamtazamia kupatikana na (janga) mauti.

قُلْ تَرَبَّصُوا فَإِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُتَرَبِّصِينَ ﴿٣١﴾

31. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Ngojeeni muangaze, kwani hakika na mimi ni pamoja nanyi nangojea na kuangaza.”

أَمْ تَأْمُرُهُمْ أَحْلَامُهُم بِهَـٰذَا ۚ أَمْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ ﴿٣٢﴾

32. Au zinawaamrisha akili zao haya? Au wao ni watu wapotofu?

أَمْ يَقُولُونَ تَقَوَّلَهُ ۚ بَل لَّا يُؤْمِنُونَ ﴿٣٣﴾

33. Au wanasema ameibuni (hii Qur-aan)? Bali hawaamini.

فَلْيَأْتُوا بِحَدِيثٍ مِّثْلِهِ إِن كَانُوا صَادِقِينَ ﴿٣٤﴾

34. Basi walete hadiyth mfano wake, wakiwa ni wakweli.

أَمْ خُلِقُوا مِنْ غَيْرِ شَيْءٍ أَمْ هُمُ الْخَالِقُونَ ﴿٣٥﴾

35. Au wameumbwa pasipo na kitu chochote, au wao (wenyewe) ndio waumbaji?

أَمْ خَلَقُوا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۚ بَل لَّا يُوقِنُونَ ﴿٣٦﴾

36. Au wameumba mbingu na ardhi? Bali hawana yakini.

أَمْ عِندَهُمْ خَزَائِنُ رَبِّكَ أَمْ هُمُ الْمُصَيْطِرُونَ ﴿٣٧﴾

37. Au wanazo hazina za Rabb (Mola) wako, au wao ndio wenye mamlaka (nayo)?

أَمْ لَهُمْ سُلَّمٌ يَسْتَمِعُونَ فِيهِ ۖ فَلْيَأْتِ مُسْتَمِعُهُم بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ ﴿٣٨﴾

38. Au wanayo ngazi (wanayopandia mbinguni) kusikilizia (yanayozungumzwa huko)? Basi msikilizaji wao alete dalili bayana.

أَمْ لَهُ الْبَنَاتُ وَلَكُمُ الْبَنُونَ ﴿٣٩﴾

39. Au (Allaah) Ana mabanati, nanyi mna watoto wa kiume?

أَمْ تَسْأَلُهُمْ أَجْرًا فَهُم مِّن مَّغْرَمٍ مُّثْقَلُونَ ﴿٤٠﴾

40. Au unawaomba ujira (kwa ajili ya kuwalingania ujumbe), kwa hiyo wameelemewa (na) uzito wa gharama?

أَمْ عِندَهُمُ الْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ ﴿٤١﴾

41. Au wanayo (elimu ya) ghayb (yaliyofichikana), basi wao wanaandika?

أَمْ يُرِيدُونَ كَيْدًا ۖ فَالَّذِينَ كَفَرُوا هُمُ الْمَكِيدُونَ ﴿٤٢﴾

42. Au wanataka njama? Basi wale waliokufuru wao ndio watakaopangiwa njama.

أَمْ لَهُمْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٤٣﴾

43. Au wana ilaah (muabudiwa wa haki) asiyekuwa Allaah? Subhaana-Allaah (Utakasifu ni wa Allaah!) kutokana na yale (yote) wanayoshirikisha.

وَإِن يَرَوْا كِسْفًا مِّنَ السَّمَاءِ سَاقِطًا يَقُولُوا سَحَابٌ مَّرْكُومٌ ﴿٤٤﴾

44. Na hata wangeliona pande kutoka mbinguni linaanguka wangelisema:  “Mawingu yamepandiana,”

فَذَرْهُمْ حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي فِيهِ يُصْعَقُونَ ﴿٤٥﴾

45. Basi waachilie mbali mpaka wakutane na Siku yao ambayo humo   watakumbana na mngurumo angamizi (kwa kiwewe).

يَوْمَ لَا يُغْنِي عَنْهُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٤٦﴾

46. Siku ambayo njama zao hazitowafaa kitu chochote, na wala wao hawatonusuriwa.

وَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا عَذَابًا دُونَ ذَٰلِكَ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٤٧﴾

47. Na hakika wale waliodhulmu watapata adhabu nyingine isiyokuwa hiyo, lakini wengi wao hawajui.

وَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعْيُنِنَا ۖ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ حِينَ تَقُومُ ﴿٤٨﴾

48. Na subiri (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa hukumu ya Rabb (Mola) wako, kwani hakika wewe uko kwenye Macho Yetu. Na sabbih kwa Sifa njema za Rabb wako, wakati unapoinuka.

وَمِنَ اللَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَإِدْبَارَ النُّجُومِ ﴿٤٩﴾

49. Na katika usiku Msabbih na zinapokuchwa nyota.



Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com