Ash-Shams (91)


سُورَةُ  الشَّمْس
Ash-Shams (91)

(Imeteremka Makka)

 
Mwenyezi Mungu Mtukufu ameapa kuanzia Sura hii kwa vitu kadhaa wa kadhaa miongoni mwa viumbe vyake vitukufu, vyenye kueleza utimilivu wa uweza wake Mwenyezi Mungu Mtukufu na Upweke wake, juu ya kufuzu kwa mwenye kuisafisha nafsi yake kwa Imani na ut'iifu, na kukhasiri kwa kupinga mwenye kuidhoofisha kwa ukafiri na maasi. Kisha ikaingilia mfano wa Thamudi, kaumu ya Saleh, na yaliyo wafika hao, ili apate kuzingatia kila mwenye inda mwenye kukadhibisha. Kwani hakika wao walipo mkadhibisha Mtume wao, na wakamuuwa yule ngamia, Mwenyezi Mungu aliwaangamiza wote, na Yeye hakhofu matokeo ya kuwaangamiza hao, na aliyo wateremshia, kwani Yeye hasailiwi kwa anayo yatenda, na hakika amewateremshia wanayo stahiki.

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا ﴿١﴾

1. Naapa kwa jua na (kwa) mwangaza wake.


وَالْقَمَرِ إِذَا تَلَاهَا ﴿٢﴾

2. Na (Naapa kwa) mwezi unapoliandama (hilo jua).

وَالنَّهَارِ إِذَا جَلَّاهَا ﴿٣﴾

3. Na (Naapa kwa) mchana unapolidhihirisha (hilo jua).

وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَاهَا ﴿٤﴾

4. Na (Naapa kwa) usiku unapolifunika (hilo jua).

وَالسَّمَاءِ وَمَا بَنَاهَا ﴿٥﴾

5. Na (Naapa kwa) mbingu na Aliyezijenga.

وَالْأَرْضِ وَمَا طَحَاهَا ﴿٦﴾

6. Na (Naapa kwa) ardhi na Aliyeitandaza.

وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّاهَا ﴿٧﴾

7. Na (Naapa kwa) nafsi na Aliyeisawazisha.

فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا ﴿٨﴾

8. Kisha Akaitia ilhamu (ya kuelewa) uovu wake na taqwa yake.

قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا ﴿٩﴾

9. Kwa yakini amefaulu yule aliyeitakasa.

وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّاهَا ﴿١٠﴾
10. Na kwa yakini amefeli yule aliyeiviza.

كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَاهَا ﴿١١﴾

11. Kina Thamuwd walikadhibisha (Mtume wao) kwa upindukaji mipaka kwao.

إِذِ انبَعَثَ أَشْقَاهَا ﴿١٢﴾

12. Walipotuma muovu wao.

فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّـهِ نَاقَةَ اللَّـهِ وَسُقْيَاهَا ﴿١٣﴾

13. Rasuli wa Allaah (Swaalih عليه السلام) aliwaambia: “(Msimdhuru) Ngamia wa Allaah, na (msimzuie) kinywaji chake.”

فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُم بِذَنبِهِمْ فَسَوَّاهَا ﴿١٤﴾

14. (Lakini) Walimkadhibisha, na wakamkata ukano wa mvungu wa goti (wakamchinja); basi Rabb (Mola) wao Akawateketeza kwa dhambi zao, kisha Akayasawazisha (mateketezi) kwa wote.

وَلَا يَخَافُ عُقْبَاهَا ﴿١٥﴾

15. Na wala Hakhofu matokeo yake.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com