Al-Zalzalah (99)


سُورَةُ  الزَّلْزَلَة
Al-Zalzalah (99)

(Imeteremka Madina)

 
Aya za Sura hii zote hazipindukii hali za Kiyama:-
Mtikisiko wa ardhi, na kutoka khazina na maiti walio zikwa chini, na kustaajabu kwa binaadamu na kuuliza kwake kwa yale yaliyo mkumba kwa ghafla, na kutoka watu makaburini mwao kwa mtafaruku wende kupokea malipo yao!

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

إِذَا زُلْزِلَتِ الْأَرْضُ زِلْزَالَهَا ﴿١﴾

1. Itakapotetemeshwa ardhi mtetemeko wake (mkubwa).

وَأَخْرَجَتِ الْأَرْضُ أَثْقَالَهَا ﴿٢﴾

2. Na itakapotoa ardhi mizigo yake.

وَقَالَ الْإِنسَانُ مَا لَهَا ﴿٣﴾

3. Na insani akasema: “Ina nini (ardhi leo)?”

يَوْمَئِذٍ تُحَدِّثُ أَخْبَارَهَا ﴿٤﴾

4. Siku hiyo itasimulia habari zake.

بِأَنَّ رَبَّكَ أَوْحَىٰ لَهَا ﴿٥﴾

5. Kwa kuwa Rabb (Mola) wako Ameifunulia ilhaam (kufanya hivyo).


يَوْمَئِذٍ يَصْدُرُ النَّاسُ أَشْتَاتًا لِّيُرَوْا أَعْمَالَهُمْ ﴿٦﴾

6. Siku hiyo watatoka watu (makaburini) makundi mbali mbali ili waonyeshwe (matokeo ya) ‘amali zao.

فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾

7. Basi yule atakayetenda kheri (hata kama ni) uzito wa chembe ya atomu (basi) ataiona.


وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ ﴿٨﴾

8. Na yule atakayetenda shari (hata kama ni) uzito wa chembe ya atomu (basi) ataiona.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com