Al-Infitwaar (82)


سُورَةُ  الإِنْفِطَار
Al-Infitwaar (82)

(Imeteremka Makka)

Sura hii imeeleza baadhi ya vitisho vya Saa ya Kiyama kwa njia ya kutangaza kuwa hakika litatokea jambo katika siku ambayo kila mtu atajua nini alilo litanguliza na nini alilo liakhirisha. Tena Aya zikaingia kumhadharisha mwanaadamu aliye danganyika na Mola wake Mlezi aliye muumba akamweka sawa, akamjenga kwa namna ya pekee, na kwa umbo bora kabisa. Inathibitisha Sura kuwa huyo mtu anaikadhibisha Siku ya Malipo, na inatilia mkazo kuwepo Malaika juu yake, walinzi mahashumu, waandishi. Na ikamalizia kusema kuwa watu wema watapata neema. Na wapotovu hawatapata ila Jahannamu, watakayo iingia Siku ya Kiyama, siku ambayo nafsi haitoweza kuimilikia nafsi nyengine chochote. Na amri yote itakuwa ni ya Mwenyezi Mungu tu.


بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

إِذَا السَّمَاءُ انفَطَرَتْ ﴿١﴾

1. Mbingu zitakapopasuka.

وَإِذَا الْكَوَاكِبُ انتَثَرَتْ ﴿٢﴾

2. Na sayari zitakapoanguka na kutawanyika.

وَإِذَا الْبِحَارُ فُجِّرَتْ ﴿٣﴾

3. Na bahari zitakaporipuka.

وَإِذَا الْقُبُورُ بُعْثِرَتْ ﴿٤﴾

4. Na makaburi yatakapopinduliwa chini juu na kufukuliwa.

عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ ﴿٥﴾

5. (Hapo kila) Nafsi itajua yale iliyoyakadimisha na iliyoyaakhirisha.

يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ ﴿٦﴾

6. Ee insani! Nini kilichokughuri kuhusu Rabb (Mola) wako Al-Kariym (Mkarimu)?

الَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّاكَ فَعَدَلَكَ ﴿٧﴾

7. Ambaye Amekuumba Akakusawazisha na Akakulinganisha sawa.

فِي أَيِّ صُورَةٍ مَّا شَاءَ رَكَّبَكَ ﴿٨﴾

8. Katika sura Aliyotaka Akakutengeneza.

كَلَّا بَلْ تُكَذِّبُونَ بِالدِّينِ ﴿٩﴾

9. Hapana! Bali mnakadhibisha (siku ya) Malipo.

وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ ﴿١٠﴾

10. Na hakika juu yenu bila shaka (kuna) wenye kulinda.  

كِرَامًا كَاتِبِينَ ﴿١١﴾

11. Watukufu wanaoandika.

يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ ﴿١٢﴾

12. Wanajua yale myafanyayo.

إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ ﴿١٣﴾

13. Hakika Al-Abraar (watendao wema) bila shaka (watakuwa) katika neema.

وَإِنَّ الْفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ ﴿١٤﴾

14. Na hakika waovu bila shaka (watakuwa) katika (Moto wa) Jahiym.

يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ الدِّينِ ﴿١٥﴾

15. Watauingia waungue siku ya Malipo.


وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَائِبِينَ ﴿١٦﴾

16. Nao hawatokosa kuweko humo.

وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿١٧﴾

17. Na nini kitakachokujulisha siku ya Malipo?

ثُمَّ مَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿١٨﴾

18. Kisha nini kitakachokujulisha siku ya Malipo?

يَوْمَ لَا تَمْلِكُ نَفْسٌ لِّنَفْسٍ شَيْئًا ۖ وَالْأَمْرُ يَوْمَئِذٍ لِّلَّـهِ ﴿١٩﴾

19. Siku ambayo nafsi yoyote (ile) haitoimilikia nafsi (nyingine) kitu chochote; na amri siku hiyo ni ya Allaah Pekee.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com