Al-Fiyl (105)


سُورَةُ  الْفِيل
Al-Fiyl (105)

(Imeteremka Makka)

 
Mwenyezi Mungu anampa khabari Mtume wake s.a.w. kisa cha Watu wa Tembo (Ndovu) walio kusudia kuivunja Nyumba ya Mwenyezi Mungu ya Al-Kaa'ba, na anakionyesha kisa hichi kuwa ni dalili ya uweza wake Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kujilipizia kwake juu ya hao wanao vunja vitu vyake vitakatifu. Mwenyezi Mungu hakika aliwasalitishia majeshi yalio wang'oa mizizi yao, na wasibakie kitu ila kama nazi iliyo liwa na mwezi.

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصْحَابِ الْفِيلِ ﴿١﴾

1. Je, huoni jinsi Rabb (Mola) wako Alivyowafanya watu wa ndovu?

أَلَمْ يَجْعَلْ كَيْدَهُمْ فِي تَضْلِيلٍ ﴿٢﴾

2. Je, Hakujaalia mbinu zao kwenye kupotea?

وَأَرْسَلَ عَلَيْهِمْ طَيْرًا أَبَابِيلَ ﴿٣﴾

3. Na Akawatumia juu yao ndege makundi kwa makundi?

تَرْمِيهِم بِحِجَارَةٍ مِّن سِجِّيلٍ ﴿٤﴾

4. Wakiwarembea kwa mawe ya udongo uliookwa (motoni).

فَجَعَلَهُمْ كَعَصْفٍ مَّأْكُولٍ ﴿٥﴾

5. Akawafanya kama nyasi zilizoliwa.





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com