Al-Buruwj (85)

سُورَةُ  الْبُرُوج
Al-Buruwj (85)  

(Imeteremka Makka)

 
Sura hii ni ya maliwaza na kuwapa mawaidha Waumini, na kuwatisha na kuwaonya wenye inadi. Imeanzia kwa kiapo chake Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa madhaahiri yanayo onekana ya uweza wake ya kwamba wapinzani wanao waudhi Waumini watafukuzwa kwenye uwanja wa rehema, kama walivyo fukuzwa walio kwenda mwendo wao katika mataifa yaliyo tangulia. Na Sura ikaingia kusimulia kisa cha hao majabari walivyo watendea Waumini, na ikafuatiza kwa kuwapa ahadi Waumini na kuwakhofisha majeuri, na kwamba Haki katika kila zama hupingwa na wapinzani. Na kwamba Qur'ani, ambayo ndiyo mwega wa Haki, na wangaikadhibisha watu fulani, lakini hiyo iko mbali kabisa na shaka, kwa sababu hakika hiyo iko katika Lauh'un Mahfuudh, Ubao Ulio Hifadhiwa ulioko kwa Mwenyezi Mungu.

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْبُرُوجِ ﴿١﴾

1. Naapa kwa mbingu zenye buruji.

وَالْيَوْمِ الْمَوْعُودِ ﴿٢﴾

2. Na siku iliyoahidiwa (kuwa itafika tu nayo ni siku ya Qiyaamah).

وَشَاهِدٍ وَمَشْهُودٍ ﴿٣﴾

3. Na shahidi na kinachoshuhudiwa.

قُتِلَ أَصْحَابُ الْأُخْدُودِ ﴿٤﴾

4. Wamelaaniwa watu wa handaki.

النَّارِ ذَاتِ الْوَقُودِ ﴿٥﴾

5. Moto wenye kuni (nyingi).

إِذْ هُمْ عَلَيْهَا قُعُودٌ ﴿٦﴾

6. Walipokuwa wamekaa hapo (karibu na huo moto).

وَهُمْ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ بِالْمُؤْمِنِينَ شُهُودٌ ﴿٧﴾

7. Nao walikuwa juu ya yale waliyowafanyia Waumini (kuwatumbukiza katika handaki la moto) ni mashahidi.

وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَن يُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ ﴿٨﴾

8. Na hawakuwachukia isipokuwa kwa vile wamemwamini Allaah Al-‘Aziyzil-Hamiyd (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye kustahiki kuhimidiwa daima).

الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿٩﴾

9. Ambaye Pekee Ana Ufalme wa mbingu na ardhi; na Allaah juu ya kila kitu ni Shahiyd (Mwenye kushuhudia).

إِنَّ الَّذِينَ فَتَنُوا الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ الْحَرِيقِ ﴿١٠﴾

10. Hakika wale waliowafitini Waumini wa kiume na Waumini wa kike (kwa kuwatesa na kisha kuwasukumiza kwenye handaki lenye moto); kisha hawakutubu, watapata adhabu ya Jahannam, na watapata adhabu ya kuunguza.

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْكَبِيرُ ﴿١١﴾

11. Hakika wale walioamini na wakatenda mazuri, watapata Jannaat zipitazo chini yake mito. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

إِنَّ بَطْشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ ﴿١٢﴾

12. Hakika mteko wa (kuadhibu wa) Rabb (Mola) wako ni shadidi.

إِنَّهُ هُوَ يُبْدِئُ وَيُعِيدُ ﴿١٣﴾

13. Hakika Yeye (Allaah) Ndiye Anayeanzisha (uumbaji) na (Ndiye) Atayerudisha.


وَهُوَ الْغَفُورُ الْوَدُودُ ﴿١٤﴾

14. Naye ni Al-Ghafuwrul-Waduwd (Mwingi wa kughufuria - Mwenye mapenzi halisi).

ذُو الْعَرْشِ الْمَجِيدُ ﴿١٥﴾

15. Mwenye ‘Arsh Al-Majiyd (Mtukufu, Mwingi mno wa ukarimu).

فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ ﴿١٦﴾

16. Afanyaye Alitakalo.

هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْجُنُودِ ﴿١٧﴾

17. Je, imekujia hadiyth ya majeshi?

فِرْعَوْنَ وَثَمُودَ ﴿١٨﴾

18. Fir’awn na (kina) Thamuwd?

بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي تَكْذِيبٍ ﴿١٩﴾

19. Bali wale waliokufuru wamo katika kukadhibisha.

وَاللَّـهُ مِن وَرَائِهِم مُّحِيطٌ ﴿٢٠﴾

20. Na Allaah Amewazunguka nyuma yao.

بَلْ هُوَ قُرْآنٌ مَّجِيدٌ ﴿٢١﴾

21. Bali hii ni Qur-aan tukufu.

فِي لَوْحٍ مَّحْفُوظٍ ﴿٢٢﴾

22. (Iliyoko) Katika Lawhim-Mahfuudhw (ubao Uliohifadhiwa).





Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com