Adh-Dhaariyaat (51)

سُورَةُ  الذَّارِيَات
Adh-Dhaariyaat (51) 

(Imeteremka Makka)


Sura hii imeanza kwa kiapo cha ukweli wa kufufuliwa na kutokea malipo. Kisha ikafuatisha kwa kiapo kingine juu ya ubabaishi wa wanao kanya katika maneno yao juu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, na juu ya Qur'ani tukufu. Kisha ikaingia kuwaonya wanao kanya kuwa watapata mwisho muovu katika Akhera. Tena ikaeleza waliyo ahidiwa wachamngu katika malipo ya vitendo vyao vyema walivyo vitanguliza duniani. Kisha ikawazindua watu wazingatie Ishara za Mwenyezi Mungu katika kuumba kwake, na katika nafsi zao, na katika mambo ya ufundi wa ajabu na uzuri wa umbo alio uweka humo.
Na ikasimulia kisa cha Ibrahim na wageni wake Malaika, kisha ikaeleza hali za baadhi ya mataifa na maangamizo yaliyo wasibu kwa kuwakadhibisha Manabii wao. Kisha ikaashiria kwa jumla baadhi ya Ishara za uumbaji, na ikahimiza watu warejee kwa Mwenyezi Mungu, na wamuabudu Yeye peke yake, ambayo hayo ndio makusudi ya kuumbwa majini na watu. Na Sura imekhitimisha kwa kuwaonya wanao mkadhibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w. kuwa watapata adhabu iliyo kwisha wapata kaumu za kabla yao.

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

وَالذَّارِيَاتِ ذَرْوًا ﴿١﴾

1. Naapa kwa (pepo) zinopeperusha (vumbi) na zinazotawanya.

فَالْحَامِلَاتِ وِقْرًا ﴿٢﴾

2. Na (mawingu) yanayobeba mzigo (wa maji).

فَالْجَارِيَاتِ يُسْرًا ﴿٣﴾

3. Na kwa (merikebu) zinazotembea kwa wepesi.

فَالْمُقَسِّمَاتِ أَمْرًا ﴿٤﴾

4. Na (Malaika) wanaogawanya (kila) amri.

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٌ ﴿٥﴾

5. Hakika mnayoahidiwa bila shaka ni (ya) kweli.

وَإِنَّ الدِّينَ لَوَاقِعٌ ﴿٦﴾

6. Na hakika malipo bila shaka yatatokea.

وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْحُبُكِ ﴿٧﴾

7. Naapa kwa mbingu zilojaa njia.

إِنَّكُمْ لَفِي قَوْلٍ مُّخْتَلِفٍ ﴿٨﴾

8. Hakika nyinyi mko katika kauli inayokhitilafiana.

يُؤْفَكُ عَنْهُ مَنْ أُفِكَ ﴿٩﴾

9. Anageuzwa (mbali na haki) kwayo anayegeuzwa.

قُتِلَ الْخَرَّاصُونَ ﴿١٠﴾

10. Wameangamia wazushi.

الَّذِينَ هُمْ فِي غَمْرَةٍ سَاهُونَ ﴿١١﴾

11. Ambao wamo katika kufunikwa na ghafla, wamesahau (Aakhirah).

يَسْأَلُونَ أَيَّانَ يَوْمُ الدِّينِ ﴿١٢﴾

12. Wanauliza: “Lini (itakuwa) Siku ya malipo?”

يَوْمَ هُمْ عَلَى النَّارِ يُفْتَنُونَ ﴿١٣﴾

13. Siku wao watakapotiwa mtihanini Motoni.

ذُوقُوا فِتْنَتَكُمْ هَـٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تَسْتَعْجِلُونَ ﴿١٤﴾

14. (Wataambiwa): “Onjeni adhabu yenu, haya ndio yale mliyokuwa mkiyahimiza.

إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ ﴿١٥﴾

15. Hakika wenye taqwa (watakuwa) katika Jannaat na chemchemu.

آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ ﴿١٦﴾

16. Wenye kuchukua yale Atakayowapa Rabb (Mola) wao. Hakika wao walikuwa kabla ya hapo ni wenye kufanya ihsaan.

كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ ﴿١٧﴾

17. Walikuwa wakilala kidogo katika usiku (wakifanya ‘ibaadah).

وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ ﴿١٨﴾

18. Na kabla ya Alfajiri wakiomba maghfirah.

وَفِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ ﴿١٩﴾

19. Na katika mali zao (wanatoa) haki maalumu kwa muombaji (mhitaji) na asiyeomba.

وَفِي الْأَرْضِ آيَاتٌ لِّلْمُوقِنِينَ ﴿٢٠﴾

20. Na katika ardhi (kuna) Aayaat (ishara, dalili, zingatio n.k) kwa wenye yakini.

وَفِي أَنفُسِكُمْ ۚ أَفَلَا تُبْصِرُونَ ﴿٢١﴾

21. Na katika nafsi zenu (kuna Aayaat) je hamuoni?

وَفِي السَّمَاءِ رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ ﴿٢٢﴾

22. Na katika mbingu, kuna riziki zenu, na yale mnayoahidiwa.

فَوَرَبِّ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِنَّهُ لَحَقٌّ مِّثْلَ مَا أَنَّكُمْ تَنطِقُونَ ﴿٢٣﴾

23, Basi Naapa kwa Rabb (Mola) wa mbingu na ardhi, hakika hiyo ni Haki kama mnavyotamka.

هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ الْمُكْرَمِينَ ﴿٢٤﴾

24. Je, imekufikia hadiyth (simulizi) ya wageni watukufu wa Ibraahiym?

إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ ﴿٢٥﴾

25. Walipoingia (nyumbani kwake), wakasema: “Salaam (‘alaykum)!” (Ibraahiym) Akasema:  (‘Alaykumus) “Salaam watu wasiotambulikana.”

فَرَاغَ إِلَىٰ أَهْلِهِ فَجَاءَ بِعِجْلٍ سَمِينٍ ﴿٢٦﴾

26. Akaenda kwa ahli yake, akaleta ndama aliyenona (aliyechomwa).

فَقَرَّبَهُ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ ﴿٢٧﴾

27. Akawakurubishia; akasema: “Mbona hamli?”



فَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۖ قَالُوا لَا تَخَفْ ۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ ﴿٢٨﴾

28. Akawaogopa ndani ya nafsi yake. Wakasema: “Usikhofu!” na wakambashiria ghulamu mwenye elimu.

فَأَقْبَلَتِ امْرَأَتُهُ فِي صَرَّةٍ فَصَكَّتْ وَجْهَهَا وَقَالَتْ عَجُوزٌ عَقِيمٌ ﴿٢٩﴾

29.  Mkewe akawakabili kwa kilio (cha kushtuka), akijipiga usoni na akasema: “Kikongwe, tasa (vipi atazaa?)”

قَالُوا كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ ۖ إِنَّهُ هُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ ﴿٣٠﴾

30. Wakasema: “Hivyo ndivyo Alivyosema Rabb (Mola) wako, hakika Yeye Ndiye Al-Hakiymul-‘Aliym (Mwenye hikmah wa yote daima - Mjuzi wa yote daima).


قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ ﴿٣١﴾

31. (Ibraahiym) Akasema: “Basi nini jambo lenu enyi Wajumbe?”

قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ ﴿٣٢﴾

32. Wakasema: “Hakika sisi tumetumwa kwa watu wahalifu.”

لِنُرْسِلَ عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِّن طِينٍ ﴿٣٣﴾

33. “Ili Tuwapelekee mawe ya udongo (wa Motoni kuwaadhibu).”

مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلْمُسْرِفِينَ ﴿٣٤﴾

34. “Yaliyotiwa alama kutoka kwa Rabb (Mola) wako kwa wapindukao mipaka.”

فَأَخْرَجْنَا مَن كَانَ فِيهَا مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٣٥﴾

35. Basi Tukawatoa humo wale waliokuwa Waumini.

فَمَا وَجَدْنَا فِيهَا غَيْرَ بَيْتٍ مِّنَ الْمُسْلِمِينَ ﴿٣٦﴾

36. Lakini hatukukuta humo isipokuwa nyumba moja (tu) yenye Waislamu.

وَتَرَكْنَا فِيهَا آيَةً لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ الْعَذَابَ الْأَلِيمَ ﴿٣٧﴾

37. (Baada ya kuwaangamiza) Na Tukaacha humo Aayah (ishara, dalili) kwa wale wanaoiogopa adhabu iumizayo.

وَفِي مُوسَىٰ إِذْ أَرْسَلْنَاهُ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ ﴿٣٨﴾

38. Na kwa Muwsaa, Tulipomtua kwa Fir’awn na madaraka bayana.

فَتَوَلَّىٰ بِرُكْنِهِ وَقَالَ سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ ﴿٣٩﴾

39. Akakengeuka kwa (kudhani zitamfaa) nguvu zake akasema: “Mchawi au majnuni.”

فَأَخَذْنَاهُ وَجُنُودَهُ فَنَبَذْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٌ ﴿٤٠﴾

40. Tukamchukuwa (yeye) na jeshi lake, Tukawatupilia mbali katika bahari naye akiwa mwenye kulaumiwa.

وَفِي عَادٍ إِذْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الرِّيحَ الْعَقِيمَ ﴿٤١﴾

41. Na kwa kina ‘Aad, Tulipowapelekea upepo angamizi.

مَا تَذَرُ مِن شَيْءٍ أَتَتْ عَلَيْهِ إِلَّا جَعَلَتْهُ كَالرَّمِيمِ ﴿٤٢﴾

42. Haukuacha kitu (chochote) ulichokifika ila ulikifanya kama kilichosagika-sagika.

وَفِي ثَمُودَ إِذْ قِيلَ لَهُمْ تَمَتَّعُوا حَتَّىٰ حِينٍ ﴿٤٣﴾

43. Na kwa kina Thamuwd, walipoambiwa: “Stareheni mpaka muda (mfupi tu).”

فَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ فَأَخَذَتْهُمُ الصَّاعِقَةُ وَهُمْ يَنظُرُونَ ﴿٤٤﴾
44. Wakaasi amri ya Rabb (Mola) wao, ikawachukuwa asw-swaa’iqah (mngurumo angamizi), na huku wao wanatazama.

فَمَا اسْتَطَاعُوا مِن قِيَامٍ وَمَا كَانُوا مُنتَصِرِينَ ﴿٤٥﴾

45. Basi hawakuweza kusimama, na wala hawakuwa wenye kujinusuru.

وَقَوْمَ نُوحٍ مِّن قَبْلُ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ ﴿٤٦﴾

46. Na (Tuliwaangamiza) watu wa Nuwh kabla. Hakika wao walikuwa watu mafasiki.

وَالسَّمَاءَ بَنَيْنَاهَا بِأَيْدٍ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ ﴿٤٧﴾

47. Na mbingu Tumezijenga kwa nguvu na qudra na hakika Sisi ndio Wenye kuzipanua.

وَالْأَرْضَ فَرَشْنَاهَا فَنِعْمَ الْمَاهِدُونَ ﴿٤٨﴾

48. Na ardhi Tumeitandaza, basi Watandazaji wazuri walioje.

وَمِن كُلِّ شَيْءٍ خَلَقْنَا زَوْجَيْنِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ ﴿٤٩﴾

49. Na katika kila kitu Tumeumba jozi ili mpate kukumbuka.

فَفِرُّوا إِلَى اللَّـهِ ۖ إِنِّي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٥٠﴾

50. Basi kimbilieni kwa Allaah, hakika mimi kwenu ni mwonyaji bayana kutoka Kwake.   

وَلَا تَجْعَلُوا مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ ۖ إِنِّي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٥١﴾

51. Na wala msifanye pamoja na Allaah miungu wengineo, hakika mimi kwenu ni mwonyaji bayana kutoka Kwake.

كَذَٰلِكَ مَا أَتَى الَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُوا سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ ﴿٥٢﴾

52. Ndio kama hivyo, hawakuwafikia wale wa kabla yao Rasuli yeyote (yule) isipokuwa walisema: “Mchawi au majnuni.”

أَتَوَاصَوْا بِهِ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ ﴿٥٣﴾

53. Je, wameusiana kwalo (jambo hilo)?  Bali wao ni watu wenye kuasi.

فَتَوَلَّ عَنْهُمْ فَمَا أَنتَ بِمَلُومٍ ﴿٥٤﴾

54. Basi jitenge nao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), kwani wewe si wa kulaumiwa.

وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَىٰ تَنفَعُ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٥٥﴾

55. Na kumbusha, kwani hakika ukumbusho (mawaidha) unawafaa Waumini.

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾

56. Na Sikuumba majini na wanadamu isipokuwa waniabudu.

مَا أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ ﴿٥٧﴾

57. Sitaki kutoka kwao riziki yoyote, na wala (Sitaki) wanilishe.

إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ ﴿٥٨﴾

58. Hakika Allaah Ndiye Ar-Razzaaq (Mwenye kuruzuku vyote daima) Mwenye nguvu kali madhubuti.

فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذَنُوبًا مِّثْلَ ذَنُوبِ أَصْحَابِهِمْ فَلَا يَسْتَعْجِلُونِ ﴿٥٩﴾

59. Basi ama wale waliodhulumu watakuwa na sehemu ya adhabu kama sehemu ya adhabu ya watu wao (waliotangulia), basi wasihimize.

فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِن يَوْمِهِمُ الَّذِي يُوعَدُونَ ﴿٦٠﴾

60. Basi ole kwa wale waliokufuru kutokana na Siku yao waliyoahidiwa.



Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com