Hadiyth Ya 15 - Suratul Faatihah - Nimeigawa Swalah Baina Yangu Na Mja Wangu Nusu Mbili



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَنْ صَلَّى صَلَاةً لَمْ يَقْرَأْ فِيهَا بِأُمِّ الْقُرْآنِ فَهِيَ خِدَاجٌ)) ثَلَاثًا غَيْرُ تَمَامٍ فَقِيلَ لِأَبِي هُرَيْرَةَ إِنَّا نَكُونُ وَرَاءَ الْإِمَامِ فَقَالَ اقْرَأْ بِهَا فِي نَفْسِكَ فَإِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:  ((قَالَ اللَّهُ تَعَالَى قَسَمْتُ الصَّلَاةَ بَيْنِي وَبَيْنَ عَبْدِي نِصْفَيْنِ وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ فَإِذَا قَالَ الْعَبْدُ (الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ) قَالَ اللَّهُ تَعَالَى حَمِدَنِي عَبْدِي وَإِذَا قَالَ (الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ)  قَالَ اللَّهُ تَعَالَى أَثْنَى عَلَيَّ عَبْدِي وَإِذَا قَالَ (مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ) قَالَ مَجَّدَنِي عَبْدِي وَقَالَ مَرَّةً فَوَّضَ إِلَيَّ عَبْدِي فَإِذَا قَالَ (إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ) قَالَ هَذَا بَيْنِي وَبَيْنَ عَبْدِي وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ)) مسلم, مالك, الترمذي, أبو داود, النسائي وابن ماجه

Kutoka kwa Abu Hurayrahرضي الله عنه   kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: ((Atakayeswali Swalah bila ya kusoma humo Mama wa Qur-aan (Suratul-Faatihah) huwa haikutimia (kasoro) [na alikariri mara tatu] haikutimia. Mtu mmoja alimwambia Abu Hurayrah: (Hata) tukiwa nyuma ya Imaam? Akasema: Isome mwenyewe (kimya kimya) kwani nilimsikia Mtume صلى الله عليه وسلم akisema: ((Allaah سبحانه وتعالى Amesema: Nimeigawa Swalah baina Yangu na mja Wangu nusu mbili, mja Wangu atapata yale aliyoyaomba. Mja anaposema (Al-HamduliLlaahi Rabbil-'Aalamiyn) Allaah  سبحانه وتعالىHusema: Mja Wangu kanihimidi (kanisifu). Na anaposema (Ar-Rahmaanir-Rahiym) Allaah سبحانه وتعالى Husema: Mja wangu kanitukuza, na anaposema (Maaliki Yaumid-Diyn) Allaah سبحانه وتعالى Husema: Mja wangu kanipa heshima. Na mara moja alisema: Mja wangu kazikubali nguvu Zangu. Na anaposema (Iyyaaka Na’budu wa Iyyaaka Nasta’iyn) Husema: Hii ni baina Yangu na mja Wangu na mja Wangu atapata kile alichokiomba. Na anaposema: (Ihdinas-Swiraatwal-Mustaqiym Swiraatwal-Lladhiyna An’amta ‘Alayhim Ghayril-Maghdhwuubi ‘Alayhim Wala-Dhwaalliyn) Husema: Hii ni ya mja Wangu na mja Wangu atapata kile alichokiomba)) [Muslim, Maalik, At-Tirmidhiy, Abu Daawuud, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]