Hadiyth Ya 20 - Malipo Ya Nia Ya Kufanya Vitendo Vyema Na Vibaya



عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيمَا يَرْوِي عَنْ رَبِّهِ عَزَّ وَجَلَّ قَال: ((إِنَّ اللَّهَ كَتَبَ الْحَسَنَاتِ وَالسَّيِّئَاتِ ثُمَّ بَيَّنَ ذَلِكَ فَمَنْ هَمَّ بِحَسَنَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللَّهُ لَهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً فَإِنْ هُوَ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللَّهُ لَهُ عِنْدَهُ عَشْرَ حَسَنَاتٍ إِلَى سَبْعِ مِائَةِ ضِعْفٍ إِلَى أَضْعَافٍ كَثِيرَةٍ وَمَنْ هَمَّ بِسَيِّئَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللَّهُ لَهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً فَإِنْ هُوَ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللَّهُ لَهُ سَيِّئَةً وَاحِدَةً)) البخاري و مسلم


Imetoka kwa Ibn ‘Abbaas رضي الله عنه   kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم kwamba katika maneno aliyoyaeleza kutoka kwa Mola wakeعَزَّ وَجَلَّ  ni kuwa Amesema: ((Allaah Ameviandika vitendo vyema na vibaya. Kisha Akavieleza (kwa kusema) yule anayekusudia kufanya kheri na asiifanye, Allaah Anaiandika kuwa ni tendo jema kamili. Lakini ikiwa aliazimia na akatekeleza, Allaah Anaiandika kuwa ni vitendo vyema kumi mpaka mara mia saba na ziada. Lakini anapokusudia kitendo kiovu na asikifanye Allaah Anakiandika kuwa ni jema moja kamili, lakini ikiwa amekusudia kutenda baya na akalitenda basi Mola anakiandika kama kitendo kimoja kiovu)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]