1. Al-Faatiha



1. SURAT AL-FAATIH'A
(Imeteremka Makka)
Sura hii iliteremka Makka kabla ya Hijra, kuhamia Mtume s.a.w. Madina. Imeitwa Al-Faatih'a, yaani Kifungulio kwa kuwa ndiyo sura ya mwanzo katika mpango wa Msahafu Mtukufu, nayo ni sura ya mwanzo iliyo teremka kwa utimilivu wake. Na sura hii inakusanya jumla ya yaliyomo katika Qur'ani na kama kwamba huu ni mukhtasari wake, na baadaye yatakuja mambo kwa tafsili, babu-babu.
Na makusudio ya Qur'ani ni: Kubainisha Tawhid, Upweke wa Mwenyezi Mungu; na kubainisha ahadi na bishara kwa Muumini mtenda mema; na kubainisha ahadi na onyo kwa kafiri na mtenda maovu; na kubainisha ibada; na kubainisha njia ya kufanikiwa duniani na Akhera; na hadithi za walio mt'ii Mwenyezi Mungu wakafuzu, na hadithi za walio muasi wakaangamia.
Sura  Al-Faatih'a inakusanya kwa ufupi na kwa kuashiria makusudio haya, na kwa hivyo ndio ikaitwa pia "Ummul Kitaab" yaani "Msingi wa Kitabu".
 

الْفَأتِحَة
Al-Faatihah (1)
  بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿١﴾
1. Kwa Jina la Allaah Ar-Rahmaanir-Rahiym (Mwingi wa Rahmah - Mwenye kurehemu).
 الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٢﴾
2. AlhamduliLLaahi (Sifa njema zote ni za Allaah) Mola wa  walimwengu.
 الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿٣﴾
3. Ar-Rahmaanir-Rahiym (Mwingi wa Rahmah-Mwenye kurehemu).
  مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ ﴿٤﴾
4. Maalik (Mfalme) wa siku ya malipo.
 إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾
5. Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada.
اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿٦﴾
6. Tuongoze njia iliyonyooka.
صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ ﴿٧﴾
7. Njia ya wale Uliowaneemesha, si (ya wale) walioghadhibikiwa wala waliopotea.


Ukitaka kusoma Sura nyengine Rejeauliko toka
Ukiwa una shauri au maelezo juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii falhaqqiy@gmail.com