Abu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu 'Anhu)-Amebashiriwa Pepo
Linapotajwa jina la As-Swiddiyq tunapata tafakuri ya watu wenye mwenendo na maadili mema. Moyo utachangamka na kuvutiwa na As-Swiddiyq (mkweli).
Abu Bakr As-Swiddiyq alikuwa rafiki wa Mjumbe wa Allaah Muhammad tokea ujana wake mpaka alipozeeka. Alikuwa mwenza mwaminifu wakati wa raha na wakati wa shida. Alikuwa akiitwa ‘mwaminifu’ ambaye alimwamini Mtume wakati wengine wakimpa mgongo (wakimkana). Imani yake ilikuwa thabiti, na alifahamika kwa umbuji wa lugha na kwa kuamiliana vizuri na watu. Alifahamika sana kwa ukarimu wake; na utajiri wake ulikuwa wa jamii ya waumini.
Ilikuwa heshima kwake kwa Allaah kuteremsha aya hii;
“Ikiwa nyinyi hamtamnusuru Mtume , basi Allaah Alikwishamnusuru walipomtoa waliokufuru, naye ni wa pili katika wawili walipo kuwa katika pango, naye akamwambia sahibu yake: Usihuzunike. Hakika Allaah yu pamoja nasi. Allaah Akamteremshia utulivu Wake, na Akamuunga mkono kwa majeshi msioyaona, na akalifanya neno la waliokufuru kuwa chini, na Neno la Allaah kuwa ndilo juu. Na Allaah ndiye Mwenye nguvu Mwenye hikima.” (9: 40).
Kisa cha Hijrah na siku walizokaa pangoni ni mfano wa somo lililoonesha usuhuba unavyoweza kuwa na nguvu.
Alikuwa kiumbe wa Allaah aliyependwa sana na Mjumbe wa Allaah na alielezewa kama ifuatavyo:
“Alikuwa dhaifu kimwili lakini mwenye nguvu katika mambo ya Allaah , alikuwa mnyofu katika nafsi yake lakini aliyetukuka mbele za Allaah . Alitukuzwa mbele za watu, na alifadhilishwa katika mioyo yao.”
Wanyonge waliimarishwa kwa ushawishi wake. Abu Bakr alikuwa chimbuko la matumaini wakati wa hali ngumu. Alikuwa kimbilio na mhimili wa Waislamu wakati akiishi nao. Alidharau maisha ya dunia, na akajiweka mbali na jambo lolote ambalo halikuwamo katika mafundisho ya Mtume Alikuwa msomi mashuhuri wa dini ambaye alibadilishana mawazo na watu na alikuwa mcheshi. Alikuwa na imani thabiti kuliko watu wote, alikuwa na imani safi na alikuwa mkweli sana. Alikuwa rahimu kwa kila mtu, hasa kwa Waislamu. Kulipokuwa na kukengeuka dhidi ya Uislamu alilia; na Uislamu uliposhambuliwa aliunguruma kama simba tayari kuihami dini na watu aliowapenda sana. Endapo aliyedhalilishwa ni mwanamke au mtoto au mnyonge, alikuwa wa kwanza kukusanya watu kwenda kwenye mapambano.
Hebu fikiri, hadhi ya Uislamu ingekuwaje kama asingewahofisha wasaliti? Ujasiri wake na ulezi wake alivifanya kuwa umoja na nguvu. Alikuwa Zaydi ya mtu wa kawaida.
Huyu ndiye Abu Bakr aliyekuwa mbora wa Waislamu baada ya kurejea katika Uislamu, na alibakia hivyo mpaka Allaah Alipomukhitari (Alipotwaa roho yake).
Ni muhali kudhukuru mema yote na uadilifu wa Abu Bakr ndani ya kurasa chache. Kwa hiyo inatosheleza kutaja sifa chache kwa matarajio ya kuwa zitawahamasisha wale wanaotafuta ukweli.
Fadhila za Wahamaji (Muhajirina)
Kuna
Aayah na Hadiyth nyingi zinazotaja fadhila za wahamaji (Muhajirina)
Mmoja wao ni Abu Bakr ‘Abdullaah bin Abi Quhaafah Al-Taymy Kauli ya
Allaah inasema,
“Wapewe
mafakiri Wahajiri waliotolewa majumbani mwao na mali yao kwa ajili ya
kutafuta fadhila kutoka kwa Allaah na radhi Zake, na wanamsaidia Allaah
na Mtume Wake. Hao ndio wakweli.” (59: 8)
Na vile vile katika Kauli ya Allaah :
“Ikiwa
nyinyi hamtamnusuru Mtume, basi Allaah Alikwishamnusuru walipomtoa
waliokufuru, naye ni wa pili katika wawili walipo kuwa katika pango,
naye akamwambia sahibu yake: Usihuzunike. Hakika Allaah Yu pamoja nasi.
Allaah Akamteremshia utulivu Wake, na akamuunga mkono kwa majeshi
msiyoyaona, na akalifanya neno la waliokufuru kuwa chini, na Neno la
Allaah kuwa ndilo juu. Na Allaah ndiye Mwenye nguvu Mwenye hikima.” (9: 40)
‘Aaishah, Abu Sa’id na Ibn ‘Abbaas walisema; “Abu Bakr alikuwa pangoni na Mtume katika pango la Ath-Thawr, Makkah).” (Al-Bukhaariy).
Habari za Peponi Zinazofurahisha
Mtume asiyezungumza kwa utashi wake, alimletea Abu Bakr habari zinazofurahisha za Peponi zaidi ya mara moja.
Abu Muusa alisimulia.
Siku
moja, nilikuwa nimekaa katika bustani na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi
wa aalihi wa sallam) Al-Madiynah, alipokuja mtu na kuomba ruhusa ya
kuingia.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:
“Mfungulie
lango, na umbashirie Pepo.” Kwa hiyo nilimfungulia, alikuwa Abu Bakr,
nilimbashiria Pepo. Mtu mwingine alikuja na kuomba ruhusa ya kuingia.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: “Mfungulie
lango, na umbashirie Pepo.”Alikuwa ‘Umar. Nilimfungulia, na nikampa
habari njema za Peponi. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) alikuwa ameegemea kisha akasimama wima na kusema:
“Mfungulie lango, na mbashirie Pepo na utukufu utakaomshukia.” Alikuwa ‘Uthmaan. Nilimfungulia
lango na nikampa habari njema za Peponi, na nikamwambia aliyodhukuru
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Katika mapokezi mengine Anas alisema:
“Mjumbe
wa Allaah, Abu Bakr, ‘Umar na ‘Uthmaan walipanda Mlima Uhud. Mlima
ulipotetema, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:
“Nyamaza
(tulia) Ewe Uhud kwa sababu kuna Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam), mkweli na Mashahidi wawili juu yako.”
Hadiyth ya tatu iliyosimuliwa na Sa’iyd bin Zayd inaeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:-
“Abu
Bakr yumo Peponi. ‘Umar yumo Peponi. ‘Uthmaan yumo Peponi. ‘Aliy yumo
Peponi. Twalhah yumo Peponi. Az-Zubayr yumo Peponi. ‘Abdur-Rahmaan bin
‘Awf yumo Peponi, na Sa’d yumo Peponi.”
Sa’iyd aliongezea kusema:
“Na kama utapenda nikutajie mwingine, Nitakutajia.” Kisha akajitaja.”[‘Usudul Ghaabah 3/580]
Anas
bin Malik alisimulia: Hakika, Mtume, Abu Bakr ‘Umar na ‘Uthmaan
walipanda mlima Uhud wakati mlima ukitetema, na hapo Mjumbe wa Allaah
alisema: “Kuwa madhubuti ewe Uhud. Kuna Mtume, mtu mwaminifu mmoja, na
mashahidi wawili wamesimama juu yako.” (Al-Bukhaariy Hadiyth Na. 3675).
Bila
shaka yeyote alikuwa anamkusudia Abu Bakr kwa kauli yake: “Mtu
mwaminifu” Imeridhiwa kuwa waaminifu na wa kweli ni miongoni mwa wenye
haki ya kuwemo Peponi kwa mujibu wa maandiko ya Qur-aan kama Mola
Alivyosema:
“Na
wenye kumtii Allaah na Mtume , hao wa pamoja na wale aliowaneemesha
Allaah miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema.
Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao! “ (4: 69).
Abu
Hurayrah alisimulia kuwa Mjumbe wa Allaah alisema: “Yeyote atakayetoa
aina mbili ya vitu kama sadaka katika njia ya Allaah, ataitwa kwenye
lango la Peponi na ataambiwa: “Ewe mtumwa wa Allaah! Neema iko hapa’
Yeyote aliyekuwa miongoni waliokuwa wakisimamisha Swalah, ataitwa kwenye
lango la Swalah. Abu Bakr As-Swiddiyq na yeyote aliyekuwa miongoni mwa
walioshiriki katika Jihaad, ataitwa kwenye lango la Jihaad, na yeyote
ambaye alikuwa miongoni mwa wafungaji, ataitwa kwenye lango la
Ar-Rayyaan; yeyote aliyekuwa miongoni mwa waliokuwa wakitoa As-Swadaqah,
ataitwa kwenye, lango la As-Swadaqah.” Abu Bakr alisema: “Waruhusu
wazazi wangu watolewe muhanga kwa ajili yake, Ewe Mjumbe wa Allaah!
Hatopata dhiki yule atakayeitwa kwenye milango hiyo. Je, yupo
atakayeitwa kwenye milango yote hiyo?”Mtume alijibu, “Ndiyo, na nataraji
utakuwa mmoja wao.”
Siku ya Kutawafu Mtume
Waislamu
walipata majonzi makubwa siku alipofariki dunia Mtume ‘Umar bin
Al-Khattwaab aliathirika sana kiasi cha kuchomoa upanga wake na kusema:
“Iwapo nitamsikia yeyote akisema kuwa Mjumbe wa Allaah amefariki dunia,
nitakata shingo yake.”
Mjumbe
alitumwa kwa Abu Bakr Yule mtu alipomwona Abu Bakr, alilia. Abu Bakr
alimwuliza: “Una jambo gani? Mtume amefariki dunia?” Yule mtu alisema:
“’Umar bin Al-Khattwaab anasema: “Sitomsikia yeyote akisema Mjumbe wa
Allaah amefariki dunia bila kutaka kukata shingo yake.”
Abu Bakr aliingia ndani ya nyumba ambapo Mtume alilazwa na kufunikwa nguo. Alimbusu na alitoka nje na kuwasomea Aayah ifuatayo:-
“Na
Muhammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwishapita kabla yake Mitume. Je,
akifa au akauwawa ndiyo mtageuka mrudi nyuma? Na atakayegeuka akarudi
nyuma huyo hatamdhuru kitu Allaah. Na Allaah Atawalipa wanaomshukuru.” (3: 144)
Na Aayah:
“Ni nani itakayemfikia adhabu ya kumhizi, na itakayemshukia adhabu ya daima.” (39: 30).
Kisha
akasema: “Yeyote aliyekuwa akimwabudu Muhammad afahamu kuwa Muhammad
amefariki dunia. Na yeyote aliyekuwa anamwabudu Allaah, afahamu ya kuwa
Allaah ni wa milele na hatokufa.” ‘Umar alisema, “WaLlaahi! Inakuwa kama
sikuwahi kuzisoma Aayah hizi mpaka leo.”
Utume Wake
Mjumbe
wa Allaah hakuwahi kumteua kati ya Maswahaba zake kuwa Khalifa. Lakini
katika siku zake za mwisho, alisema kama ilivyoelezwa katika Hadiyth
ifuatayo:
“Amri aliyopewa Abu Bakr kuwaswalisha watu.”
‘Aaishah
alisema: “Kwa uhakika, Abu Bakr ana moyo laini na kila wakati hulia.
“Mjumbe wa Allaah alisema: “Mwamuru Abu Bakr awaswalishe watu.” Alijibu,
“Kwa hakika Abu Bakr ana moyo laini, na atakaposimama katika nafasi
yako, watu hawatomsikia: Akaendelea kusema: “Muamuru Abu Bakr
awaswalishe watu. Wewe ni sawa na mwanamke kwenye kisa cha Yuusuf.”
Kwa
hiyo, mjumbe (aliyetumwa kuwasilisha amri ya Mjumbe wa Allaah
kuwaongoza watu katika Swalah) alifika kwa Abu Bakr na kumfahamisha juu
ya suala lile. Hivyo ‘Abu Bakr ndiye aliyewaswalisha watu wakati wa uhai
wa Mtume.
Baadhi
ya Wanachuoni wamehitimisha kuwa kuanzia wakati ule na tukio lile la
Mjumbe wa Allaah alimpasisha Abu Bakr kuwa Khalifa, kwa kuwa
kuwaswalisha watu ni jukumu la kwanza na muhimu kwa Khalifa.
Baada
ya Mtume kufariki dunia Al-Answaar (Waungaji mkono watu wa Madiynah)
walijumuika chini ya kivuli cha Banu Saa’idah na kusema: “Sa’d bin
Ubaidah atapewa Ukhalifa.”
Al-Muhajirina
(Waliohamia Madiynah kutoka Makkah) walipata habari za mkusanyiko wa
kuchagua Khalifa, nao walikwenda kuhudhuria. Mmoja wa Answaar alitoa
hutuba. ‘Umar bin Al-Khattwaab alitaka kutoa hutuba, lakini Abu Bakr
alimwashiria akae kimya, na alifanya hivyo. Abu Bakr alisimama na
kuhutubia. Hakuzoza jambo juu ya mema ya Answaar.
Alisema:
“Mnafahamu ya kuwa Mjumbe wa Allaah alisema:
“Endapo
watu wangechukua bonde maalumu, na Answaar wakachukua jengine.
Ningechukua bonde la Answaar. Nilichosema kuhusiana nanyi ni maadili
yenu mema. Lakini Waarabu hawakujua kadhia hii isipokuwa Ma-Quraysh kwa
sababu wao ni bora kuliko Waarabu wengine kwa wema. Nimewachagua watu
hawa wawili kwa ajili ya kiapo cha utii. Kwa hiyo kuleni kiapo cha
utii.”
Aliushika mkono wa ‘Umar bin Al-Khatwab na Abu ‘Ubaydah bin Al-Jaraah
Abu
Bakr alipomaliza hatuba yake, Answaar walipendekeza kuwa na Ma-amir
wawili, mmoja kutoka ‘Answaar na mwingine kutoka Mahajirina.
‘Umar
alisema: “Mnajua ya kuwa Mjumbe wa Allaah alimuamuru Abu Bakr
awaswalishe watu? Wakasema, “Ndiyo, hapana shaka.” Kawaambia “Nani
atapewa kipaumbele; mtu mwingine asiyekuwa yule aliyetangulizwa na Mtume
? Wakajibu: “Hayupo: (hapana)”.
Abu
Bakr alisimama na kumwambia ’Umar Nyoosha mikono yako ili tule kiapo
cha kukukutii” Lakini ‘Umar alikataa, na mkono wa Abu Bakr ili kula
kiapo cha kumtii. Usayd bin Hudayr na Bashir bin Sa’d alimpa ahadi ya
utiifu Abu Bakr na watu wengine waliohudhuria walifanya hivyo pia. Kwa
hiyo wote Answaar na Muhajirina walichukua ahadi ya kumtii Abu Bakr Siku
iliyofuatia, watu walijumuika kwa ajili ya Swalah. Abu Bakr alipopanda
juu ya mimbari, kila mtu alikula kiapo cha kumtii.
Khutbah Yake Baada ya Kiapo Cha Utiifu
Abu
Bakr alipochaguliwa kuwa Khalifa, alipanda juu ya mimbari kutoa hotuba,
na alipokuwa akifanya hivyo, alionyesha mwenendo mwema. Aliheshimiwa
kama Swahaba mwenye cheo. Alionyesha heshima na kumcha Allaah.
Baada ya kumshukuru Allaah alisema:
“Enyi
watu! Nimechaguliwa kuwa Khalifa, hata hivyo mimi sio bora kuliko nyie.
Kwa hiyo, kama nikipatia katika hukumu, niungeni mkono; vinginevyo mna
haki ya kunikosoa. Ukweli ni uaminifu, na kuongopa ni uasi. Wadhaifu
miongoni mwenu watapata nguvu mpaka nitakapowapoka haki zao; ambao watu
wenye nguvu miongoni mwenu ni dhaifu kwangu mpaka nitakapowapoka haki
yao, Allaah akipenda. Msiache Jihaad (kupigana kwa ajili ya Allaah ).
Hapana watu waliacha Jihaad bila kughadhibikiwa na Allaah Nitiini wakati
namtii Allaah na Mjumbe Wake. Nikiwaasi, nami sina haki ya kutiiwa.”
Kisha aliwaamuru wasimame ili waswali kwa kusema: “Simameni kwa ajili ya Swalah, na Allaah Awanyeshee huruma zake.”
Abu
Bakr alihofia sana majukumu makubwa aliyobeba kama Khalifa, Qays bin
Abu Hazm alisema: Nilipokuwa nimekaa na Abu Bakr Khalifa wa Mjumbe wa
Allaah mwezi mmoja baada ya kutawafu Mtume . Kuliadhiniwa na watu
walijumuika. Ilikuwa mara ya kwanza kusomwa Adhaana. Abu Bakr alipanda
kweye mimbari, na akamtukuza Allaah. Kisha akasema:
“Enyi
watu natamani mtu mwingine angepewa haya madaraka. Kama mmenitaka
nitawale kama alivyofanya Mtume wenu, itakuwa nje ya uwezo wangu kwa
sababu yeye alikuwa amehifadhiwa, na muhimu Zaidi alikuwa akipokea
wahyi.”
Vita Dhidi Ya Walioritadi
Baada
ya kufariki dunia Mtume, makabila mengi ya Kiarabu katika sehemu nyingi
waliritadi (walibadili imani) isipokuwa Kaskazini mwa Madiynah ambapo
makabila yaliona jeshi la Usaamah walitanabahi kuwa kama Waislamu
wasinge kuwa na nguvu wasingeweza kusonga mbele umbali ule dhidi ya
jeshi kubwa kama Usaamah alivyofanya. Kwa Abu Bakr halikuwa na jambo la
muhimu zaidi ya mantiki. Ulikuwa ni uamuzi wa Mtume, na kwa hiyo ilikuwa
lazima uheshimiwe bila kujali matatizo au vikwazo. Maagizo yake
yalikuwa “Nilitumaini mbele jeshi la Usaamah. Naapa kwa Allaah iwapo
mbwa mwitu watanishambulia, sitosita kupeleka jeshi. Kwani sitobadilisha
maamuzi yaliyofanywa na Mjumbe wa Allaah .
Wartadi walikuwa makundi mawili.
· Kundi la kwanza liliritadi kwa hofu na waliwafuata Mitume wa uongo, kama vile Musaylimah, Tulayhah na kadhalika.
· Kundi
jengine halikuacha Uislamu na waliendelea kuamini ya kuwa: “Hapana
apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, na kuwa Muhammad ni mtumwa
Wake na Mjumbe wake. Hata hivyo, walikataa kutoa Az-Zakaah. Mgogoro wa
kundi hili ulipelekwa kusuluhishwa kwa Khalifa (Abu Bakr).
‘Umar bin Al-Khattwaab alikuwa mmoja na Maswahaba walioitwa kusikiliza mgogoro.
Abu Bakr alipinga kwa nguvu zake zote, alisimama imara kama jabali.
Hakuogopa Lolote na wakati huo alitoa hutuba yake maarufu:
“WaLlaahi, kama waliniamini hatamu ya mnyama waliyokuwa wakimpa Mjumbe wa Allaah , nitapigana mpaka waisalimishe,
‘Umar alimwambia:
“Unawapigaje
ambapo Mtume alisema: “Nimeamrishwa (na Allaah) kuwapiga wale
wanaopigana, mpaka waseme: La illaha illAllaah (hapana mwenye haki ya
kuabudiwa ila Allaah ). Na yeyote aliyesema, ataokoa maisha yake na mali
yake, kwa kutovunja shari’ah (haki na hali zitakazonifanya aadhibiwe
kwa haki (bila uonevu), na hesabu yake itakuwa kwa Allaah ”
Abu Bakr alisema:
“WaLlaahi!
Nitawapiga wale wanaotofautisha kati ya Swalah na Zakaah, kwa kuwa
Zakaah ni haki ya lazima kuchukuliwa kutokana na mali (kwa mujibu wa
Amri ya Allaah). WaLlaahi! Watakapokataa kunilipa hata ugwe waliokuwa
wakitoa zama za Mjumbe wa Allaah, nitawapiga mpaka watoe walichozuia.”
Maswahaba wa Mtume walikuwa na rai kuwa Abu Bakr aamiliane na makafiri kwa upole, ‘Umar alikuwa mmoja wao. Alimwambia:
“Ewe Khalifa wa Mjumbe wa Allaah ! Kuna mpole na mwenye huruma kwa watu.”
Abu Bakr alikasirika na kumwambia:
“Nilitarajia
msaada wako, lakini umeniacha mkono. Je, inafaa kuwa wakorofi katika
siku za ujahili na dhaifu katika Uislamu? Wahyi umesimama, na sasa Dini
imekamilika. Inahoofika wakati bado niko hai! Kama Mjumbe wa Allaah
asingesema: Isipokuwa lile lililofaradhishwa.’ Kwa hali hiyo,
tutasimamisha Swalah, na kuwalipa masikini haki yao. WaLlaahi, hata kama
watu wote wasinisaidie, nitapigana nao peke yangu.” Wasaidizi
wa waasi (murtadi) waliona uchache wa askari wa Kiislamu, Madiynah
baada ya kutoka kwa jeshi la Usaamah. Hali hii iliwafanya washambulie.
Abu
Bakr alikuwa amechukua tahadhari, hivyo aliwatuma baadhi ya Maswahaba
kwa makabila yaliyokuwa jirani ambao wangeshambulia Madiynah, na
makabila hayo yalipigwa.
Abu
Bakr aliongeza jeshi lililokuwa na Answaar na Muhajirina mpaka
alipofika Naq (kauli ya Najd). Wakazi wa jangwani walikimbia pamoja na
watoto wao. Watu walimtaka Abu Bakr arejee Madiynah na ateue kamanda
mpya wa jeshi. Alimteua Khalid bin Al-Waliyd na akamwambia:
“Watu watakaporejea kwenye Uislamu na wakalipa haki za masikini, iwapo mmoja wenu anataka kurejea na arejee.”
Abu
Bakr alirejea Madiynah wakati jeshi la Usaamah lilikuwa limepata
ushindi. Jeshi la Usaamah lilipopumzika, Abu Bakr alikusanya vikosi kumi
na moja chini ya Khaalid bin Al-Waliyd, ‘Ikrimah bin Abu Jahl., ‘Amr
bin Al-‘As, Sawayd bin Maqrin, Al-‘Ala Bin al-Haddramiy na wengineo.
Vita Vya Buzaakhah
Vita
vya Buzaakhah vilikuwa vita maarufu dhidi ya makafiri. Abu Bakr
alimuelekeza Khalid bin Al-Waliyd kupigana dhidi ya Mtume mwingine na
bandia aliyeitwa Tulayhah bin Khuwaylid Al-Asadi.
Abu
Bakr alimwamuru ‘Adiy bin Haatim aende Tay (kabla ya kumwamuru Khaalid
bin Al-Waliyd Alimwamuru ‘Adiy aanzie Tay, kisha aelekee Buzaakhah na
kisha Al-Batah. Aliambiwa hata kama alipata ushindi, hakutakiwa kuondoka
mpaka apewe rukhsa na Abu Bakr Ki-istratejia, Abu Bakr alisema watoke
na jeshi wakakabiliane na jeshi pinzani lililoongozwa na Khaalid bin
Al-Waliyd kama njia ya kuwahofisha.
Vita Ya Al-Yamaamah
Al-Yamaamah
ilikuwa nchi ya asili ya Banu Haniyfah iliyopo katikati ya Rasi ya
Arabia, Kaskazini ya Najraan. Lilikuwa eneo lenye mimea mingi na mitende
mingi na hapo ndipo Khaalid bin Al-Waliyd alipigana dhidi ya
Musaylimah, mzandiki mkubwa. Musaylimah alikuwa miongoni mwa
wasaidizi wa Banu Haniyfah ambao walikwenda kwa Mjumbe wa Allaah (mwaka
wa makaimu). Aliporejea, alijidai kuwa mwenza wa Mjumbe na akawaongeza
watu wake kwenye bid’ah na kuwaweka mbali na Uislamu.
Baada
ya kifo cha Mtume , Abu Bakr alimtuma ‘Ikrimah bin Abi Jahl na kisha
akamtuma Shurahbiyl bin Hasanah kupigana na Musaylimah, lakini Ikrimah
alishindwa. Abu Bakr alimuelekeza Shurahbiyl kwa watu wa Oman, na
alimwamuru akae mpaka Khaalid atakapoungana naye wampige Musaylimah kwa
pamoja.
Jeshi
la Waislamu lilipokabiliana na jeshi la Musaylimah, Zayd bin
Al-Khattwaab alikuwa upande wa kulia kwa Khaalid na Abu Hadhayfah bin
‘Utbah alikuwa upande wa kushoto. Bendera la Answaar lilibebwa na
Thaabit bin Qays bin Shammar bendera la Muhajirina lilibebwa na Saalim
(mtumwa aliyeachwa huru na Abu Hadhayfah) Wafuasi wa Musaylimah walikuwa
elfu kumi ambao walipigana kwa nguvu.
Waislamu
walipigana mpaka wakakaribia kushindwa. Baadhi ya Waislamu walihisi
hatari ya kushindwa kutokana na ukubwa wa jeshi la adui, kwa hiyo
wakapeana moyo kuwa imara katika mapambano. Thaabit bin Qays alisema:
“Ee Allaah! Nakanusha yale wayafanyayo (yaani watu wa Al-Yamaamah) na nakuomba msamaha kwa yote wayafanyayo (yaani Waislamu).
Kisha alimshambulia adui na kumuua. Zayd bin Al-Khattwaab alisema:
“WaLlaahi, sitozungumza tena mpaka nimshinde.” Vita iliendelea kuwa kali na Saalim, Abu Hudhayfah na Zayd bin Al-Khattwaab waliuawa.
Khaalid
bin Al-Waliyd alitanabahi ya kuwa kusingekuwa na ushindi wa uhakika
mpaka wamwue Musaylimah. Kwa hiyo alishambulia huku akipiga ukulele…
Kila mtu aliyejitokeza aliuawa. Musaylimah na aliokuwa nao baada ya
kuona hali ile walikimbilia bustanini. Al-Bara’ bin Maalik alisema:
“Enyi
Waislamu! Nitupeni ndani ya bustani. Waislamu walisita kwa kumwogopa,
lakini walifuata amri yake, na alitupwa ndani ya bustani mpaka akapigana
vita kali Musaylimah aliuawa. ‘Wahshi (mtumwa aliyeachwa huru na
Jubayr, aliyemuua Hamzah ‘ami yake Mtume, siku ya Uhud) alimuua
Musaylimah waliuawa kwa sababu jeshi la Waislamu lilikuwa imara. Allaah
Aliwasaidia mpaka wakamshinda adui.
Ukusanyaji Wa Qur-aan Tukufu Kuwa Mus-haf Mmoja
Matokeo
ya vita vilivyopiganwa kati makafiri na Waislamu, Maswahaba maarufu wa
Mtume waliuawa. Miongoni mwao ni wale waaminifu waliohifadhi Qur-aan
Takatifu. ‘Umar alichelea kuwa maandishi ya Qur-aan yangepotea kama vifo
hivyo vingeendelea, na alimtaka Abu Bakr atoe amri ya kukusanywa kwa
Qur-aan Tukufu ambako kutafanywa mara moja. Abu Bakr hakupenda kufanya
jambo ambalo Mtume hakulifanya mwenyewe, lakini alijua ya kuwa ‘Umar
alikuwa sahihi, vinginevyo Qur-aan ingeweza kupotea baada ya muda. Abu
Bakr alikubaliana na fikra za ‘Umar hivyo alimuamuru Zayd bin Thaabit
akusanye matini ya Qur-aan.
Alisimulia Zayd bin Thaabit (mwandishi wa Qur-aan Tukufu). “Abu
Bakr As-Swiddiyq aliniita wakati watu wa Yamaamah walipouawa (yaani
Maswahaba wengi wa Mtume waliopigana na Musaylimah). Nilikwenda kwake na
nilimkuta ‘Umar bin Al-Khattwaab amekaa naye. Abu Bakr aliniambia,
“‘Umar alikuja kwangu na kuniambia:
“Qur-aan
wengi walifariki dunia (yaani waliohifadhi Qur-aan) siku ya vita ya
Yamaamah na nachelea wengi wao wanaweza kuwa mashahidi katika vita
vingine na sehemu kubwa ya Qur-aan hupotea. Kwa hiyo, nakushauri wewe
(Abu Bakr) utoe amri Qur-aan ikusanywe.” Nilimwambia ‘Umar: ‘Unawezaje
kufanya jambo ambalo Mjumbe wa Allaah hakulifanya?” ‘Umar alijibu:
‘WaLlaahi, hili jambo zuri la kufanywa, “‘Umar aliendelea kunishawishi
nikubali pendekezo lake mpaka Allaah Alipofungua kifua changu na kuanza
kuona uzuri wa rai ya ‘Umar. “Kisha Abu Bakr aliniambia, “Wewe ni kijana
mwerevu, na hatuna shaka nawe. Ulikuwa ukiandika Ufunuo Mtakatifu kwa
kuongezwa na Mjumbe wa Allaah kwa hiyo tafuta maandiko ya Qur-aan na
yakusanye yawe kitabu kimoja.”
WaLlaahi!
Kama wangeniamuru kuhamisha moja ya milima, isingekuwa mizito katika
ombi hili. Kisha nilimwambia Abu Bakr,” Utafanyaje jambo ambalo Mtume
hakulifanya?” Abu Bakr aliendelea kunishawishi nikubaliane na rai yake
mpaka Allaah Alipofunua kifua changu kwa kile alichofunua kifua cha Abu
Bakr na ‘Umar Kwa hiyo nilianza kuitafuta Qur-aan na kuikusanya
kutokana (na yale yaliyoandikiwa juu yake) makuti ya mtende, mawe meupe
membamba na kutoka kwa watu waliojua kwa moyo, mpaka nilipoipata ayah ya
mwisho ya Surat Al-Tawbah kwa Abi Khuzaimah Al-Answaari, na Aya hiyo
niliikuta kwake tu. Aya yenyewe ni hii:
“Hakika
amekwishakujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha
yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana. Kwa Waumini ni mpole na
mwenye huruma.
Basi
wakigeuka, wewe sema: Allaah Ananitosheleza. Hapana mungu isipokuwa
Yeye tu. Mimi namtegemea Yeye, na Yeye ndiye Mola Mlezi wa Kiti Kikuu
cha Enzi.” (9: 128,129).
Muswada
kamili na Qur-aan ulibaki kwa Abu Bakr mpaka alipofariki dunia, kisha
akawa kwa ‘Umar mpaka alipofariki dunia, kisha kwa Hafswah, binti ya
‘Umar. (Al-Bukhaariy, Hadiyth Na. 4986).
Ilisimuliwa kwa mamlaka ya ‘Aliy:
“Malipo bora juu ya (ukusanyaji wa) Mushaf yamwendee Abu Bakr Alikuwa na mwanzo kurekodi Qur-aan Tukufu.”
Hadhi Yake
Hapana
shaka kuwa Abu Bakr alikuwa na hadhi ya kipekee miongoni mwa Maswahaba
wa Mjumbe Kuna Hadiyth nyingi zinazothibitisha ya kuwa alikuwa anapendwa
Zaidi na Mtume Kuna Hadiyth nyingi zinazothibitisha ya kuwa alikuwa
anapendwa Zaidi na Mtume na alikuwa rafiki yake kabla na baada ya
kutangaza Uislamu. Mtume hatosahau kuwa alikuwa wa mwanzo kusilimu.
Maswahaba walijua hadhi yake kwa Mtume na walijua alivyotumia kwa ajili
ya Dini. Ni kwa sababu hii walimheshimu sana na wakaweka hadhi yake
kwenye ndimi na mioyo yao. Wakati wote alikumbukwa na kusemwa kwa
heshima na uchaji wake. Alimpenda kwa sababu mbili. Ya kwanza, kwa
sababu ya tabia yake kama vile ukarimu, wema, ukweli, msafi (asiye na
dhambi kubwa) na kuwa wa kwanza katika Uislamu na ya pili mapenzi kwa
Mtume
Amr bin Al-‘Aas alisema:
“Mtume
alinitumia kamanda wa jeshi aliyeitwa Dhatus–Salaasil. Nilimwuliza:
“Nani unayempenda zaidi? Akajibu, ‘Aaishah. Nikamwambia, ‘Katika
wanaume’ Akajibu “Baba Yake.” Kisha nikasema: ‘Kisha nani? Akajibu:
‘‘Umar bin Al-Khattwaab . Kisha Mtume aliwataja wanaume wengine.”
Mtume katika Hadiyth nyingi anawafafanulia Maswahaba sababu ya kumpenda zaidi Abu Bakr. Msikilize asemavyo.
“Kwa
uhakika Allaah alinituma kwenu. Mkaniambia: ‘Unasema uongo’, ambapo Abu
Bakr (aliniamini na) akawambia watu, ‘Anasema kweli, na akanifariji.”
Kisha alisema mara mbili, “Basi hamuachi kumdhuru mwenzangu?” Baada ya pale hapana aliye mdhuru Abu Bakr. (Al-Bukhaariy 2661.)
Shukrani za Mtume zinaweza kuonekana katika kauli yake:
“Abu
Bakr amenipendelea kwa mali yake na usuhuba wake. Kama ningetakiwa kuwa
na Khaliyl miongoni mwa binaadamu, bila shaka ningemchukua Abu Bakr
lakini udugu wa Kiislamu na urafiki unatosha. Fungeni milango yote ya
Msikiti isipokuwa ule wa Abu Bakr.” (Al Bukhaariy 3654.)
Kwa mamlaka ya ‘Abdullaah bin Shaqiyq ambaye alisema ya kuwa alimwambia ‘Aaishah:
“Nani
kati ya Maswahaba wa Mjumbe wa Allaah alipendwa sana naye?” Alijibu,
“Abu Bakr” Nilisema, “Kisha nani?” Alijibu “‘Umar” Nikasema “Kisha
nani?” Alijibu, “Abu ‘Ubaydah” nilimwambia kisha nani?” Alinyamaza
kimya. (Sunan At-Tirmidhiy 3657.)
Daraja ya Abu Bakr ilikuwa ya juu baada ya Mitume (kwa ubora).
“Alisimulia
Ibn ‘Umar. Tulikuwa tukiwalinganisha watu kuona ni yupi bora wakati wa
uhai wa Mjumbe wa Allaah Tulimwona Abu Bakr kuwa bora zaidi, kisha ‘Umar
na kisha ‘Uthmaan ”
Inafahamika
ya kuwa Mtume alipenda na kuchukia kwa ajili ya Allaah. Kwa hiyo
mfahamu ya kuwa hadhi ya Abu Bakr ilipokuwa ya juu mbele ya Allaah kwa
kuwa ilikuwa juu kwa Mtume
Mjumbe wa Allaah alisema:
“Kwa
hakika watu wenye daraja la chini watawaona wale wenye daraja la juu
kama muonavyo nyota zing’arazo upeo wa macho. Na kwa hakika, Abu Bakr na
‘Umar ni miongoni mwa hao.”
Imani Naye
Kutokana
na kuwa karibu na Mtume tunaona tabia ya Abu Bakr ilikuwa uaminifu
wake, ukweli na kupenda haki. Alitegemewa kwa masuala ya sekula na Dini
na aliamuru Abu Bakr aongoze Swalah alipokuwa mgonjwa sana. Watu wote
walichukulia tukio hilo kuwa Abu Bakr atakuwa Khalifa, kwa kuwa
kuswalisha watu ni jukumu la Khalifa. Hili linathibitishwa na maneno ya
Mtume:
“Sijui
nitakuwa nanyi kwa muda gani, kwa hiyo fuateni mwongozo wa watu wawili
watakaochukua uongozi baada yangu”, na akamnyooshea kidole Abu Bakr na
‘Umar.” (At- Tirmidhiy 3664.)
Hivi Mjumbe wa Allaah anawaamuru watu wafuate uongozi wa mtu yeyote isipokuwa yule mwenye kuaminika.
‘Aaishah amesema kuwa Mtume alisema,
“Hainipitikii akilini ya kuwa mtu mwingine angekuwa Imaam katika Swalah, wakati Abu Bakr alikuwa miongoni mwao.”
Ibn ‘Abbaas alisimulia ya kuwa Mtume alisema:
“Kama ningetakiwa kuwa na Khalili, ningemchukua Abu Bakr, lakini yeye ni ndugu yangu na mwenzangu (katika Uislamu)” (Al-Bukhaariy).
Na Ayyuub alisimulia ya kuwa Mtume alisema,
“Kama ningetakiwa kumchagua Khalili, ningemchukua yeye (yaani Abu Bakr) kuwa Khalili, lakini udugu wa Kiislamu ni bora.” (Al-Bukhaariy).
Kuna Hadiyth nyingine inayothibitisha uaminifu huu. Jubayr bin Mut’im alisimulia.
Mwanamke
alifika kwa Mjumbe wa Allaah na kuzungumza naye. Alimtaka aseme hoja
yake, na alisema; “Nitafanya nini. Ewe Mjumbe na Allaah, nitakapokuja
nikakukosa?” (kama alikuwa na maana, “Nikikuta umefariki dunia) Alimjibu
“Usiponikuta, nenda kwa Abu Bakr.” (Al-Bukhaariy Hadiyth Na. 3659)
Uaminifu
huu wa Mjumbe wa Allaah ulipenya nyoyo za Waislamu. Kutokana na hali
hiyo watu wengi walikuta kigogo cha utii na akapata uungwaji mkono, na
maazimio ambayo yaliathiri kwa kiasi kikubwa kukua kwa dola ya Kiislamu.